MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Issue Date
Now showing 1 - 20 of 258
Results Per Page
Sort Options
Item Maendeleo ya kimaudhui katika tamthilia tano za Ebrahim N. Hussein(1985) Mutegi, Mukobwa J. N.; Kitsao, Jay; Bakari, MuhamedItem Usawiri wa wahusika makahaba katika riwaya za Said Ahmed Mohammed(Kenyatta University, 1990) Muindi, Augustine; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti wetu unahusu suala la ukahaba katika riwaya nne za Said Ahmed Mohamed. Tunahakiki usawiri wa wahusika makahaba kwa madhumuni ya kubainisha sababu za kuwepo kwa ukahaba katika jamii. Aidha, tunatilii namna ambavyo mwandishi anawabadilisha wahusika wake kutoka kwa maisha ya ukahaba na kama mabadiliko hayo yanatoasuluhisho halisi kwa jamii ya makahaba. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa ndipo tunapojadili tasnifu kwa jumla, mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti wetu, upeo wa utafiti wetu. Vile vile, tunajadili baadhi ya kazi nyingine zilizowahi kuandikwa na ambazo kwa namna fulani, zinahusiana na utafiti wetu. Aidha, tutasema machache kuhusu nadharia tunayotumia katika utafiti wetu. Kisha tutatazama sababu za kuchagua mada hii na njia tutakazofuata katika kutafiti juu ya mada yetu. Katika sura ya pili na ambayo ndiyo nguzo ya tafiti, tunaelezea dhana na nadharia za ukahaba. Dhana na nadharia hizi zinatusaidia katika kubainisha vigezo mbalimbali vinavyotambulisha kahaba katika jamii. Tunafikia upeo wa utafiti wetu katika sura ya tatu na nne. Katika sura ya tatu, tunanuia kubainisha sababu mbalimbali ambazo zimewavuta baadhi ya wahusika katika maisha ya ukahaba. Sura ya nne, tunajadili namna ambavyo mwandishi anawaondoa wahusika wake kutoka kwa maisha hayo. Sura ya tano ni ya hitimisho. Tunatoa muhtasari wa kazi tuliyoifanya. Kisha, tunatathmini kama tumefikia malengo ya utafiti wetu. Mwisho-kabisa, tunatoa marejeleo ya utafiti wetu.Item Uchanganuzi wa usemi katika sajili ya dini: sifa bainifu za lugha ya mahubiri(2001) King'ei, Kitula Osore, MiriamKatika tasnifu hii, tumechunguza sifa bainifu za lugha ya mahubiri kama zinavyojitokeza katika sajili ya dini katika lugha ya Kiswahili. Tumetumia data kutokana na mahubiri mbalimbali na kuyachanganua ili kudhihirisha sifa zake. Utafiti huu ulikuwa na malengo mawili ambayo ulitekeleza. Kulikuwa na utambuzi wa sifa bainifu za lugha ya mahubiri na utambuzi wa aina za mshikamano na jinsi zinavyounganisha. mahubiri. Katika kufanya hivi, mtazamo wa kimtindo na wa mshikamano katika nadharia ya uamilifu wa lugha ilitumika. Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi wa tasnifu imeshughulikia swala la utafiti, sababu za kuchagua swala lenyewe, madhumuni ya utafiti, upeo wa utafiti, misingi ya kinadharia, yaliyoandikwa kuhusu somo lile na mbinu za utafiti. Ni katika sura ya pili ambapo tumejishughulisha na baadhi ya sifa bainifu katika lugha ya mahubiri kama vile jinsi wahubiri wanavyoanza mahubiri yao, njia wanazoturnia kuendeleza ujumbe, na namna wanavyohitimisha. Kutokana na uchunguzi wetu tuligundua ya kwamba kuna mianzo maalum ya kuanza mahubiri. Kwa jumla wahubiri huanza kwa maamkuzi na pia kutaja kiini cha ujumbe wao.Wahubiri hutumia njia nyingi kuendeleza ujumbe kama vile matumizi ya mifano takriri, kubadilisha sauti, maswali na kadhalika. Pia, kuna njia maalum za kutamatisha mahubiri. Katika kila ruwaza iliyojadiliwa, maelezo ya kiisimu yametolewa. Sura ya tatu yaonyesha kuwa mahubiri yana sifa ya kuchanganya msimbo. Kuchanganya msimbo kumeshughulikiwa kama mojawapo ya sifa bainifu katika kuendeleza ujumbe. viii • Aina muhimu za kuchanganya msimbo na JlOS1 zinavyojitokeza katika matini za uchanganuzi zimejadiliwa. Sura ya nne yaonyesha kuwa lugha ya mahubiri ina aina mbalimbali za mshikamano. Kwa mfano, kuna mshikamano wa kimsamiati, urejeshi, uunganishi, ubadilishaji na udondoshi. Sura ya tano na ya mwisho inajumuisha muhstasari na matokeo ya utafiti kwa jumla. Mapendekezo ya utafiti mwingine unaoweza kufanywa katika uwanja huu pia yamewekwa katika sura hiiItem Mielekeo kuhusu taarifa va habari: uchunguzi katika mtaa wa Komarock jijini Nairobi.(Kenyatta University, 2002) Namulanda, Duncan Kizito; King'ei, Kitula Osore, MiriamItem Uhalisiajabu katika riwaya ya babu alipofufuka (2001) ya S.A mohamed na bina-adamu! (2002) yA K.W Wamitila(Kenyatta University, 2004-08) Magaju, Jacinta Kagendo; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu umeshughulikia swala la uhalisiajabu katika riwaya teule za fasihi ya Kiswahili. Riwaya zilizohakikiwa ni Babu Alipofufuka (2001) ya S.A. Mohamed na Bina-Adamu! (2002) ya K.W. Wamitila. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni kitengo kimoja cha mwelekeo wa usasaleo. Hii ni nadharia ya uhalisiajabu. Katika nadharia ya uhalisiajabu, matukio yanasawiriwa kiajabuajabu, ni ya kuogofya na kutisha. Matukio haya huashiria hali halisi ya maisha katika jamii. Uhalisiajabu ni mtindo wa riwaya wa hivi majuzi unaopiku njia za kimapokeo za uandishi wa fasihi ya Kiswahili na usawiri wa jamii. Kimapokeo, riwaya inapaswakujengeka katika misingi ya uhalisia. Tasnifu hii ina jumla ya sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa ndipo tumeshughulikia mada ya utafiti, malengo ya utafiti, sababu za kuchagua mada na yaliyoandikwa kuhusu hii mada. Aidha, tumejadili upeo wa utafiti huu na misingi ya nadharia iliyouongoza. Mwisho, mbinu za utafiti zimeelezwa. Sura ya pili imejadili maisha ya waandishi S.A. Mohamed na K.W. Wamitila. Tumeonyesha vipindi mbalimbali vya uandishi wao. Uchunguzi huu umedhamiria kuonyesha mitindo waliyoitumia tangu waanze kuandika na pia kuonyesha ni kwenye kipindi gani cha uandishi waliingilia uandishi wa kihalisiajabu na kwa nini walifanya hivyo. Sura ya tatu na nne zinachunguza jinsi riwaya za Babu Alipofufuka na Bina-Adamu! zimetumia uhalisiajabu katika kuwasilisha ujumbe. Tumeonyesha mihimili ya nadharia ya uhalisiajabu waliyoitumia. Mihimili hii ni pamoja na matukio ya kiajabuajabu, ndoto na uhalisia, uduara wa wakati, visaasili, uvunjwaji wa mipaka ya mahali na upekee wa mtindo wa riwaya ya kihalisiajabu. ,;~ Sura ya tano imehusika na kulinganisha na kulinganua riwaya zote mbili kwa mujibu wa mada husika. Aidha, matokeo ya utafiti, matatizo yaliyokabiliwa katika utafiti na mapendekezo yametolewa katika sura hii. Kutokana na utafiti huu, imebainika wazi kwamba Mohamed na Wamitila wanatumia uhalisiajabukimakusudi. Mihimili mikuu ya uhalisiajabu imo katika kazi zao. La maana zaidi ni kwamba wanatumia uhalisiajabu kama mkakati unaowawezesha kujadili maswala yanayousibu ujirani wetu. S.A. Mohamed anatumia mkakati huu kumulika rnatatizo ya kiuchumi na ya kijamii yanayowakabili Waafrika kutokana na utawala finyu wa viongozi wao. K.W. Wamitila anatumia mtindo huo huo kuupiga vita utandaradhi na ubepari wa kimataifa. Pamoja na kuonyesha matatizo yanayoyakabiliwa na Waafrika, Mohamed na Wamitila wana imani kwamba matatizo ya Waafrika yanaweza kutatuliwa si kwa kutafuta tiba huko nje katika mataifa ya Kimagharibi, bali kwa kuyatafuta humuhumu barani Afrika kihalisiajabu.Item Hadithi fupi za kisasa za kisw ahili kama utanzu mahuluti.(Kenyatta University, 2005) Mukopi, Lilian Makonjio; King'ei, Kitula Osore, MiriamItem Uwiano wa picha na matini katika mabango ya matangazo ya ukimwi: mtazamo wa Kisemiotiki(2006) Kimani, Hellen Wanjlku; Ndungo C. M.; Mwihaki A. N.Lengo la kazi hii ni kuchanganua uwiano wa maana za picha na matini katika mabango ya matangazo ya UKIMWI kwa kuzingatia tathmini za wapokezi. Watafitiwa ambao walishirikishwa katika utafiti huu waliteuliwa kutoka maeneo ya Githurai na Kiandutu katika wilaya ya Thika, Vitengo vya watu wenye umri, kazi, elimu, tajriba, falsafa na mielekeo tofauti vilihusika. Kwa kurejelea misimbo ya nadharia ya Semiotiki kwa mujibu wa Barthes uchanganuzi wa ishara zote za kisanaa na kiisimu katika mabango thelathini na matano yanayohusu ugonjwa hatari wa UKIMWI yamechanganuliwa. Kazi hii imegawanyika katika sehemu tano. Sura ya kwanza imetanguliza kazi yote kwa kuangazia mada ya utafiti, maswali, malengo, upeo na mipaka ya utafiti. Mengine yaliyoshughulikiwa katika sura hii ni misingi ya nadharia, tahakiki za maandishi yanayohusiana na mada hii, ukusanyaji na uwasilishaji wa data. Sura ya pili imeshughulikia viunzi vya matangazo kwa nia ya kupata maana msingi katika mabango ya UKIMWI, kwa kutalii yale yanayojidhihirisha wazi pasi kuhusisha tajriba, mielekeo na falsafa za mtu binafsi na za kijamii. Sura ya tatu, imeangazia ujumbe katika mabango ya matangazo ya UKIMWI pamoja na kuhakiki dhamira za miguso tofauti. Uhakiki huo uliegemea upande wa yaliyomo kwenye tangazo kama vile: mada, maudhui, wahusika, pamoja na msuko wa picha na matini kwa kurejelea maoni ya watafitiwa. Kwenye sura ya nne, vigezo vya uwiano wa maana na ujumbe katika picha na matini vimeshughulikiwa. Tumechunguza namna picha na matini zinavyohimiliana, kutegemeana na kuathiriana katika kumwelekeza mpokezi kufasiri maana na ujumbe. Tumeangazia pia mchango wa usanii wa picha na matumizi ya lugha kwenye matini katika kufanikisha uwiano wa maana na ujumbe unaofikia hadhira. Sura ya tano imetoa muhtasari wa kazi yote. Aidha, sura hii imeshughulikia matokeo, mahitimisho pamoja na mapendekezo ya utafiti wa baadaye kwa azima ya upanuzi wa mawasiliano ya ishara za kisanaa katika hatua za kuboresha uwasilishaji wa maana na ujumbe, ili yaende sambamba na yale ya ishara za kiisimu.Item Athari ya duksi katlka ufunzaji na ujifunzaji wa kiswahili: mtazamo wa uchanganuzi linganishi tasnifu(2007) Wenyaa, Nasaba Salome; King'ei, Kitula; Osore, MiriamKazi hii imekusudia kuchanganua athari ya elimu ya Duksi katika ufunzaji na ujifunzaji wa sarufi ya lugha ya Kiswahili kwa mujibu wa mtazamo wa nadharia ya Uchanganuzi Linganishi. Vipengele vya kisarufi yaani abjadi, maendelezo, msamiati, mtindo wa kuandika, mpangilio wa maneno katika sentensi ndivyo vilivyochunguzwa katika utafiti huu. Sampuli mseto ndiyo iliyochaguliwa na kuhusishwa. Watafiti walioshirikishwa walitoka katika wilaya ya Garissa, mjini pamoja na viunga vyake. Tajriba, imani, elimu, mielekeo na maoni ya wanajamii wa viwango mbalimbali yalizingatiwa. Kazi hii pia ilizingatia mbinu za kufunzia Kiswahili madhumuni yakiwa ni kuboresha na kuimarisha ufunzaji na ujifunzaji wa lugha hii katika mkabala wa mazingira ambapo lugha ya Kiarabu inazingatiwa. Yaani hutumiwa kwa kuendeshea shughuli za kidini. Kutokana na utafiti huu ilibainika kuwa elimu ya Duksi ina athari chanya na hasi. 'Mbinu za kufunzia zimedhihirisha njia tofauti tofauti zinazoweza kusaidia kuinua kiwango cha kufunza lugha. Papo hapo kutokana na ukinzano kati ya vipengele vya kisarufi vya (Kiarabu na Kiswahili), imetambulikana kuwa wanafunzi hupata shida zinazohusiana na abjadi, maendelezo, hijai, msamiati na maana ya sentensi. Utafiti huu umependekeza kuwa bado Kuna haja ya kuendeleza elimu jumuifu. ambapo mbinu changamano zinaweza kutumika. Hii ni kwa sababu mafunzo hayo yote ya kidini na ya kimagharibi yana manufaa kwa maisha ya wanafunzi wakiwa shuleni na hata baada ya masomo shuleni.Item Usambamba katlka ushairi-huru(2007) Mwania, James M.; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu umeshughulikia usambamba katika ushairi hum wa . Kiswahili. Lengo la utafiti huu ni kudhihirisha namna mshairi wa kisasa anavyotumia uhuru wake wa utunzi katika kujadili maswala mbalimbali yanayoikumba jamii. Utafiti huu umetumia usambamba katika kuzihakiki diwani za Kichomi, Mchezo wa Karata na Chembe cha Mayo. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni nadharia ya semiotiki. Nadharia hii huzingatia zaidi ishara na uashiriaji katika kazi za fasihi. Hivyo \ humsaidia mhakiki kuchunguza ujumbe unaowasilishwa na msann katika kazi zake. Kazi hii imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti pamoja na sababu za kuchagua mada. Hali kadhalika, udurusu wa maandishi yanayohusu mada ya utafiti pamoja na msingi wa nadharia iliyoongoza utafiti huu ni baadhi ya mambo ambayo yameshughulikiwa. Pia imeshughulikia mbinu za utafiti, sampuli, ukusanyaji pamoja na uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Sura ya pili imeshughulikia historia fupi ya ushairi pamoj a na dhana ya ushairi, ushairi hum na historia fupi ya ushairi hum. Kadhalika, mazingira ya msanii, enzi ya ukoloni katika Afrika Mashariki na kuchipuka kwa usambamba nchini Tanzania na Kenya ni baadhi ya yaliyojadiliwa. Pia imeshughulikia maisha ya wasanii tuliochunguza kazi zao Kezilahabi, Mberia na Mazrui.Item Matumizi ya sitiari katika vitendawili vya abanyala (k): mtazamo unganishi na vitendawiu vya waswahili(2007) Meble, BarasaThe purpose of the study is to investigate the use of metaphor in the Abanyala and Swahili riddle. The researcher was inspired by the fact that even though the writers and researchers of riddles did a lot in collecting, classifying and giving functions of riddles, the aspect of the use of metaphor in riddles was overlooked. More so in the specified communities. Most riddles are in fact metaphors for this reason the researcher looked into the use of the metaphor in the Abanyala and Swahili riddle. The researcher based on the principles laid out in the Semiotic Theory which was found by Ferd inand de Saussure in the year 1906. The theory was later developed by Charles Pierce and Roland Barthes who had a different view from Ferdinand de Saussure. Pierce and Barthes associated sign and meaning in relation to the context. Pierce believed that sign as an object, can be classified as an icon, an index, or a symbol. Barthes is associated with the code which he believes that it can be used in analyzing literature, he further divided the code as follows: proairetic, hermeneutic, semic, symbolic and referential codes. These principles were used in establishing types of metaphors in the Abanyala and Swahili riddles. The importance of metaphors in the Abanyala and Swahili riddles. The principles also guided the researcher in finding out why the Abanyala and Swahili use riddles. The research started from the library in which information pertaining riddles and metaphors were found. Thereafter the researcher went Into the field for data collection. Purposive sampling was used during data collection whereby !lve .standard six pupils in five primary schools, five old men and five old women were sampled f t i- basihg on their knowledge and experience in the targeted community. Questionnaire, discussion and observation methods were used during data collection. The research report is divided into five chapters. Chapter one deals with introductory issues. Chapter two deals with types of metaphors used in Abanyala and Swahili riddles. Chapter three metaphors and their uses, chapter four why the Abanyala and Swahili use riddles. Chapter five conclusions research findings and recommendations. The findings of the study will benefit the society as a whole.Item Usawiri wa wahusika ka tika dafina ya Umalenga (H.M Mbega) na jiero la ndani (S.A Mohamed)(2008) M' garuthi, Timothy Kinoti; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu umeshughulikia swala la usawm wa wahusika katika mashairi ya Kiswahili. Mtafiti ameyahakiki mashairi teule ya washairi .wawili kwa lengo la kutathmini jinsi washairi hawa walivyowateua wahusika wao, aina za wahusika na jinsi wahusika hawa walivyotumiwa kutolea hisia za w,ashairi. Diwani zilizochaguliwa ni mbili; moja ya Hassan Mwalimu Mbega Dafina ya Umalenga (1984) na nyingine ya Said Ahmed Mohamed Jicho la Ndani (2002). Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ile ya Ulimbwende ambayo hujaribu kueleza umuhimu wa wahusika katika ushairi, hasa katika kutolea hisia za mshairi badala ya kujifunga na arudhi. Nadharia hii pia hueleza umuhimu wa kuzin tia mazingira ya aina mbalimbali katika utunzi wa mashairi. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti ambapo mtafiti ameifafanua mada ya utafiti, sababu za kuchagua mada na upeo wa utafiti. Sura hii pia inao ufafanuzi juu ya udurusu wa maandishi yanayohusu mada hii pamoja na nadharia iliyoongoza utafiti. Hatimaye pana maelezo juu ya mbinu za utafiti zilizotumika. Katika sura ya pili pamejadiliwa vigezo vinavyozingatiwa na washairi katika uteuzi wa wahusika wao. Mtafiti ameshughulikia aina mbalimbali za mazingira ambayo huchangia katika uteuzi wa wahusika. Sura ya tatu imejadili aina za wahusika wanaopatikana katika mashairi teule na jinsi washairi walivyowaunga kwa ubunifu wa hali ya juu kwa lengo la kuuwasilisha ujumbe wao kikamilifu. Vlll Mtafiti ameangaha jinsi wahusika hawa wanavyohusiana na kuathiriana na hivyo kusaidia katika ujenzi wa maudhui. Katika sura ya nne mtafiti amejadili jinsi washairi walivyowatumia wahusika kudhihirishahisia mbalimbali. Sura ya tano ni hitimisho linalotoa muhtasari na matokeo ya utafiti, pamoja na mapendekezoya mtafiti. Mwishonimwa tasnifu kuna marejeleo ya utafiti huu.Item Tathmini ya Mtalaa wa Isimu Jamii wa Shule za Upili Nchini Kenya(Kenyatta University, 2008) Ngugi, Mwangi Boniface; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu umeshughulikia kutathmini mtalaa wa Isimujamii wa shule za upili nchini Kenya. Utafiti huu ulidhamiria kutathrriini na kuimarisha mtalaa wa Isimujamii katika lugha ya Kiswahili kama chombo cha mawasiliano kwa kuongozwa na misingi ya nadharia za ufundishaji wa Lugha ya Pili na Isimujamii. Utafiti huu pia ulibainisha changamoto zinazowakumba walimu wanapofundisha Isimujamii iliyojumuishwa katika silabasi ya mtalaa wa sasa. Wilaya ya Thika ilichaguliwa kama eneo la utafiti kwa vile ina shule za Taifa, Mkoa, Wilaya na za Kibinafsi zilizohitajika kufanyia utafiti. Ukusanyaji wa data ulifanywa kupitia mahojiano ya walimu, watalaamu wa elimu na kuchunguza ratiba ya vipindi vya masomo kutoka kidato cha kwanza hadi cha nne. Dhana ya mitalaa pamoja na uandalizi wa mitalaa imepitiwa kwa vile ni muhimu katika utekelezaji wa mtalaa wowote mpya. Maoni ya walimu na wakuza mitalaa kuhusu dhana ya mtalaa na maandalizi yake yamewasilishwa kwa njia ya mjadala. Vile vile, uchanganuzi wa maoni ya walimu na wakuza mitalaa kuhusu mawanda ya Isimujamii umeshughulikiwa. Hatimaye matokeo ya utafiti huu pamoja na mapendekezo yameshughulikiwa ambapo imebainika kuwa, mtalaa wa Isimujamii una udhaifu katika kumwongoza mwalimu ili aimarishe kiwango cha mawasiliano cha wanafunzi. Walimu wengi wanasisitiza miundo ya lugha badala ya uamilifu wa lugha. Jambo jingine linalotinga utekelezaji wa mtalaa wa Isimujamii ni ukosefu wa vifaa vya kufundishia. Utafiti huu utafaidi sera na upangaji wa lugha. IIi kuimarisha uhusiano mwema katika jamii yenye lugha nyingi, lugha moja inahitajika. Lugha kama hiyo itapatikana kwa kuifunza shuleni.Item Maigizo kama mbinu ya maudhui katika riwaya mbili za Ken Walibora(Kenyatta University, 2008-04) Ochenja, Rajab; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu umeshughulikia maigizo kama mbinu ya maudhui katika riwaya mbili za Ken Walibora. Riwaya zilizoshughulikwa ni Ndoto ya Amerika, (2001) na Kufa Kuzikana, (2003). Utafiti huu uliongozwa na nadharia mseto za uhalisia na uigizaji. Nadharia hizi zilifaa katika utafiti huu hasa ikizingatiwa ya kwamba riwaya zilizotafitiwa zimesheheni matukio mengi ambayo yanaakisi mambo yanayotokea katika maisha ya kawaida. Kutokana na utafiti huu, imebainika kuwa riwaya za Walibora zilizotafitiwa zina sifa za kitamthilia. Mwandishi ametumia mbinu mahsusi za maigizo ambazo zimezifanya riwaya hizi kubainika kama tamthilia. Kwanza, mwandishi amewashirikisha wahusika wake zaidi katika kutenda na kusema, kuliko kusema pekee. Vitendo vyao vimeandamana na mazungumzo. Haya yanaonekana kupitia wahusika kama Isaya, Madoa na 'Rock Mwamba' au Zablon Okutoyi katika Ndoto ya Amerika (2001); na Akida, Tim na Tamari katika Kufa Kuzikana (2003). Utafiti pia umebainisha kuwa katika kuzifanya riwaya zake zibainike kama tamthilia, Walibora amewafanya wahusika wake wote kuwa binadamu halisi wanaowasiliana moja kwa moja. Jambo hili limeyapa masimulizi yake uhai na uhalisi zaidi kiasi cha kuonekana kama maigizo. Katika matukio mengi, mwandishi amewafanya wahusika wake wawasiliane wakitumia wakati uliopo, jambo ambalo linatoa taswira ya uigizaji. Kupitia utafiti, imebainika pia kuwa riwaya za Walibora zilizotafitiwa zimebeba wahusika wa kila umri na jinsia; hili ni jambo la kawaida katika maisha halisi kwa sababu linaakisi hali inayopatikana katika maisha ya kila siku; na maisha ni maigizo. Utafiti pia umebainisha kuwa mwandishi ametumia mabadiliko ya mandhari katika riwaya zilizohakikiwa ili kujenga taswira ya uigizaji. Mandhari yamebadilishwa ili kuafiki mada iliyohusishwa katika mazungurnzo baina ya wahusika. Kupitia riwaya hizi, kuna mandhari ya shule, ofisi, mahakama, sokoni na hata kituo cha polisi. Hili ni sawa na jukwaa ambalo hupatikana katika maigizo. Kubadilika kwa mandhari kila mara kunaweza kukamithilishwa na mabadiliko yanayotokea jukwaani katika michezo ya kuigiza ili kuashiria kumalizika kwa onyesho moja na kuanza kwa onyesho lingine. Utafiti umebainisha vile vile kuwa maudhui yanayoshughulikiwa katika kazi za Walibora yamechangia pakubwa kuzifanya zikaonekana kama maigizo. Maudhui ya uhalifu, ukabila, ubinafsi na ukatili yamewasilishwa kwa hadhira kupitia maigizo ya moja kwa moja ya wahusika mbalimbali. Utafiti huu utakuwa na mchango ufuatao; kwanza, umetuonyesha kuwa inafaa tuwe na mtazamo tofauti na vigezo vingine vya kuzihakiki riwaya badala ya kuselelea katika mitazamo ya kijadi iliyokuwa ikichukulia riwaya kama utanzu mahsusi unaojitosheleza. Kupitia utafiti hull, imebainika kuwa riwaya za WaIibora zilizotafitiwa zina pia sifa za kitamthilia. Mchango mwmgme ni kuwa, baada ya utafiti, imebainika kuwa riwaya yoyote inaweza pia ikawa na sifa za kitamthilia kama ilivyobainika katika riwaya za Walibora zilizotafitiwa. Utafiti huu pia ni miongoni mwa kazi chache ambazo zimewahi kuhakiki baadhi ya kazi za Walibora kwa mtazamo tofauti. Kazi hizo zimehakikiwa kama zinazobeba sifa mseto za tanzu mbaIimbali na kutofautiana na mitazamo ya awali iliyochukulia tanzu tofauti za fasihi andishi kama zinazojitosheleza. Kwa hivyo, utafiti huu utawapatia wasomi wengine wa kazi za fasihi ya Kiswahili barabara tofauti za kufuata wakiwa katika safari ya kusaka mengi zaidi katika taaluma hii.Item Utohozi fonolojia wa maneno - mkopo ya dholuo kutoka kwa Kiswahili(Kenyatta University, 2008-11) Omondi, Olal Anne; King'ei, Kitula Osore, MiriamKazi hii inatekeleza madhumuni ya kuchambua maneno-mkopo ya Dholuo yanayotokana na lugha ya Kiswahili. Kuwepo kwa maneno mageni yanayoshabihiana na Kiswahili kulizua haja ya kueleza vipi Dholuo inavyoyaruhusu maneno hayo kutumika sawia na leksia zake asilia. Tatizo hili ndilo linaloshughulikiwa katika uchanganuzi wetu kama namna ya kuangaza jinsi Dholuo inavyoelekeza fonolojia yake kudhihirisha ukubalifu na usarufi wa utohozi ndanimwe. IIi kufanikisha uchambuzi wa mantiki ya mada yetu, tumeteua nadharia inayoafiki malengo ya utafiti wetu. Nadharia tulizotambua kutufaa ni Fonolojia Tenganishi na Fonolojia Mizanishi. Hali kadhalika tumewajibika kutumia mbinu husishi zitakazowajumuisha watafitiwa na mtafiti na kufanikisha utambuzi wa maneno-mkopo kutoka kwa Kiswahili yanayotumika katika uzungumzaji Dholuo. Mbinu hizo ni uchunguzi-ushiriki na mahojiano. Kijumla, mpangilio wa kazi hii umewasilishwa kwenye sura nne. Sura ya kwanza inatanguliza usuli wa mada pamoja na nyenzo za kimsingi zinazodhibiti kaida za uchanganuzi. Sura ya pili inaingilia vigezo vya Fonolojia ya Dholuo kwa maksudi ya kuangaza kanuni zinazoongoza lugha hii, ili kumulika jinsi zinavyoweza kuathiri maneno kutoka kwa lugha nyingine. Kitovu cha mada yetu kinashughulikiwa katika sura ya tatu ambapo uchambuzi unazingatia utohozi kifonolojia. Hapa ndipo panapo maelezo ya maumbo mbalimbali yanayotokana na utohozi pamoja na usawiri wa vielelezo vya sura dhahiri za maneno-mkopo. Sura ya nne ni tamati inayotoa muhtasari wa kazi yote.Item Dhima ya utawala wa nabongo mumia katika maenezi ya lugha ya kiswahili ubukusuni, Mkoani Magharibi (Kenya)(Kenyatta University, 2009) Nakhisa, Andrew W.; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu umeeleza na kuchanganua dhima ya utawala wa Nabongo Mumia katika maenezi ya lugha ya Kiswahili Ubukusuni, Magharibi mwa Kenya. Utafiti huu ulijikita katika kipindi cha utawala wa Nabongo Mumia tangu kutawazwa kwake kama Chifu Mkuu, mnamo mwaka wa 1910 hadi kifo chake katika mwaka wa 1949. Katika utafiti huu, tutalenga kuainisha, kueleza kuchunguza na kuchanganua mikakati iliyotumiwa na Nabongo Mumia kuchangia maenezi ya lugha ya Kiswahili. Katika kulifafanua swala la utawala, misingi iliyowekwa ili kufanikisha maenezi ya lugha ya Kiswahili iliangaliwa. Maendeleo na mabadiliko yaliyojikita katika asasi muhimu kama dini ,biashara, ndoa na maingiliano ya kijamii kwa kuitumia mizani ya mifanyiko ya kijamii yalichangia maenezi ya lugha ya Kiswahili Ubukusuni. Lugha ya Kiswahili ilipata hadhi kubwa katika kipindi hiki kwa sababu iliendesha shughuli nyingi za Nabongo Mumia ambaye alikuwa mshiriki wa karibu wa mkoloni. Utafiti huu basi umebainisha nafasi muhimu ya utawala wa Nabongo Mumia katika kuwekea lugha ya Kiswahili msingi thabiti wa kuenea Ubukusuni. Tasnifu hii imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi imeshughulikia swala la utafiti, sababu zakuichagua mada, upeo wa utafiti, madhumuni ya utafiti, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za mtafiti. Sura ya pili imechunguza historia ya jamii mbili - Ababukusu na Abawanga - hasa jinsi walivyoingiliana na kuathiriana. Sura ya tatu inaangalia dhima ya utawala wa Nabongo Mumia katika maenezi ya Kiswahili. Sura ya nne imeangazia asasi nyinginezo kama dini, mahakama, ndoa miongoni mwa nyingine. Mwisho, sura ya tano ni hitimisho. Mtafiti arnetoa muhtasari, matokeo kuhusu utafiti, mapendekezo ya utafiti zaidi na matatizo yaliyokumba utafiti huu. Kutokana na utafiti huu imedhihirika kwamba utawala ulichukua nafasi muhimu zaidi katika maenezi ya lugha ya Kiswahili Ubukusuni. Pili, utafiti huu umeonyesha kwamba Babukusu walikuwa wategemezi kwa kuwa katika kuitumia lugha ya Kiswahili, walianza kuunga mkono utamaduni wa kigeni. Mwisho, asasi kama ndoa, dini, biashara, mahakama za Kiafrika, elimu, muziki, michezo na miundo misingi ilifanikiwa Ubukusuni kwa sababu ya kutumia lugha ya Kiswahili. Kwa kiasi kikubwa asasi hizi zilifanikishwa na utawala wa Nabongo Mumia.Item Uamilifu wa Tonisho Katika Sentensi za Kikamba(Kenyatta University, 2009) Muinde, Sarah Nthenya; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu ulitekelezwa kwa madhumuni ya kuchambua na kujadili ruwaza za tonisho katika sentensi za Kikamba, ili kubainisha muundo na uamilifu katika nyanja za sintaksia na pragmatiki. Uchanganuzi ulitegemea mihimili ya Sarufi Amilifu Mfumo, hasa amali za lugha, tanzu za kisarufi na mitazamo ya kishazi. Nadharia ya Sarufi Amilifu Mfumo ilishirikisha misingi ya kimuundo ya Sarufi Zalishi. Swala la utafiti lilikuwa kudhihirisha uamilifu wa tonisho katika sentensi za Kikamba kupitia dhima za kisintaksia na kipragmatiki. Mbinu za utafiti zilijumuisha nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yaliwakilishwa kwa njia ya maelezo katika sura nne. Sura ya kwanza ilichambua usuli wa mada na kubainisha suala la utafiti, malengo na tahakiki za utafiti, misingi ya kuchagua mada, tahakiki ya maandishi, misingi ya kinadharia na mbinu za utafiti. Sura ya pili ilifafanua muundo wa sentensi za Kikamba. Dhima kuu ya sura hii ilikuwa kutambulisha maneno na kuchanganua miundo virai vyake, kwa madhumuni ya kuwakilisha sentensi za Kikamba. Uchanganuzi wa kishazi ulifanywa kupitia mitazamo mitatu ya kishazi. Ruwaza za tonisho katika hivi vishazi zilibainishwa kwa mujibu wa maana na uamilifu wake katika sura ya tatu. Tonisho ni kigezo muhimu katika sarufi ya Kikamba na ina mchango katika uwanja wa sintaksia kwa jumla pamoja na utumikizi katika ufundishaji wa lugha.Item Mabadiliko ya maudhuikiwakati katika nyimbo za harusi za jamii ya waembu(2009) Mbogo, Njeru S.; King'ei, Kitula Osore, MiriamMalengo ya utafiti huu yalikuwa kuonyesha j insi maudhui katika nyimbo za harusi miongoni mwa watu wajamii ya Waembu yalivyobadilika kiwakati tangu kabla na baada ya maingilio ya Wakoloni. Aidha, utafiti huu umechunguza na kueleza matukio ya kijamii yaliyochangia mabadiliko haya. Bali na hayo, utafiti huu umelenga kueleza mabadiliko haya ya maudhui kinadharia. Kwa kuzingatia nadharia ya uhalisia iliyoasisiwa kwa pamoja na Gustav Flaubert (1850), Rene Wellek na wengine kati ya kame ya 19 na 20, ilibainika kwamba maudhui katika nyimbo kama utanzu wa fasihi simulizi hubadilika kusadifu matukio ya kihistoria ya kipindi fulani katika jamii. Kipindi cha kabla ya maingilio ya wakoloni katikajamii ya Waembu kilikuwa na nyimbo anuwai za harusi zilizobeba maudhui mahususi. Baada ya maingilio ya wakoloni, maudhui katika nyimbo hizi yalibadilika kwa kiasi kikubwa ingawa kuna machache yaliyoendelea. Kwa sababu ya mabadiliko hayo, kumezuka mitazamo miwili ya kuangalia maudhui katika nyimbo za harusi za j amii ya Waembu ambayo ni maudhui ya nyimbo za kabla ya maingilio ya wakoloni na ya zile za baada ya maingilio hayo. Utafiti huu umeonyesha jinsi maudhui katika nyimbo za harusi zajamii ya Waembu yalivyobadilika kutoka kipindi kimoja hadi kingine.Item Maono ya jamii katika tamthilia za Chacha nyaigotti chacha: swala la uongozi(Kenyatta University, 2010) Gichuru, Tirus Mutwiri; King'ei, Kitula Osore, MiriamItem Mtazamo Mpya wa Usawiri wa Mwanamke katika Utendi wa Maisha ya Adamu na Hawaa na Paradise Lost(Kenyatta University, 2011) Muli, David Kiamba; King'ei, Kitula Osore, MiriamItem Taathira ya dhamira kwa mtindo katika hadithi fupi teule za Kiswahili(Kenyatta University, 2011-04) Ntiba, Onesmus Gitonga; King'ei, Kitula Osore, MiriamKatika tasnifu hii tumechunguza athari ya dhamira katika uteuzi wa mtindo katika hadithi fupi teule za Kiswahili. Tumetumia diwani one za mwaka wa 2007. Diwani hizo ni Damu Nyeusi no Hadithi Nyingine (2007), Likizo ya Mauti no Hadithi Nyingine (2007), Kurudi Nyumbani no Hadithi Nyingine (2007) na Alidhani Kapata no Hadithi Nyingine (2007). Malengo ya tasnifu hii yalikuwa ni kuainisha maswala wanayoshughulikia waandishi wa hadithi fupi za 2007 katika diwani zao, kudhihirisha dhamira katika hizo hadithi, kubainisha ni vipi dhamira hizo zinavyouathiri uteuzi wa mitindo wanayoituIDia kuziwasilisha na mwisho kuangazia jinsi mazingira huathiri utunzi wao. Katika utafiti huu, tuliongozwa na Nadharia Changamano inayofumbata baadhi ya mihimili kutoka Nadharia ya Uchanganuzi Saikolojia na Nadharia ya Mtindo. IIi kuipata data faafu, tulitumia mbinu kusudio. Hii ni kwa sababu huu ni utafiti wa kifasihi unaoziJenga diwani teule. Kutokana na utafiti huu, tumelipinga wazo kwamba mwandishi wa hadith fupi hana wakati wa kutosha na hivyo basi anatumia ubanaji unaoathiri dhamira yake. KuJingana na utafiti huu, i1iibuka kuwa mwandishi ana wakati wa kutosha; ni kuamua tu ameamua kuwasilisha dhamira yake kupitia utanzu wa hadithi fupi. Dhamira ya mwandishi huibua uteuzi wa mtindo unaomwezesha kuiwasilisha dhamira yake kikamilifu. Pia ilibainika kuwa maswala wanayoshugbulikia waandishi wa hadithi fupi ni mambo yanayoiathiri jamii ya kisasa. Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi imeshughulikia maswala ya kikaida kwa mujibu wa matakwa y~ Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, Chuo Kikuu cha Kenyatta kama vile swala la utafiti, sababu za kuchagua mada, malengo ya utafiti, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada hii na mbinu za utafiti. Katika sura ya pili, chimbuko na maendeleo ya utanzu huu wa hadithi fupi yameangaziwa. Pia fasili, muundo na sifa zake utanzu huu zimeangaliwa. Katika sura ya tatu, tumeanza kwa kuyashughulikia mazingira ya waandishi wa hadithi tunazochunguza katika utafiti we.tu . Pia, tumeshughulikia dhamira za dawa za kulevya, ukiukaj i wa haki za mtoto na swala la Ukimwi. Haya tumeyashughulikia kupitia hadithi nane. Sura ya one nayo imeangalia dhamira za kutowajibika kwa viongozi wa kisiasa, migogoro katika ndoa na tamaa ya pesa. Hapa, dhamira hizi zimeangaliwa katika jumla ya hadithi mahsusi kenda. Namna dhamira hizi zinavyoathiri uteuzi wa mitindo imechunguzwa katika sura hizi mbili. Sura ya tano ambayo ni ya mwisho ni hitimisho na matokeo ya utafiti kwa jumla. Pia, imetoa mapendekezo ya utafiti wa baadaye. Utafiti wetu ulifanikiwa na tuna uhakika kuwa umetoa mchango wake katika upanuaji wa welewa wa utanzu huu ambao kwa ulinganifu ndio una historia fupi zaidi katika fasihi ya Kiswahili.