Uchanganuzi wa usemi katika sajili ya dini: sifa bainifu za lugha ya mahubiri
Loading...
Date
2001
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Katika tasnifu hii, tumechunguza sifa bainifu za lugha ya mahubiri kama zinavyojitokeza
katika sajili ya dini katika lugha ya Kiswahili. Tumetumia data kutokana na mahubiri
mbalimbali na kuyachanganua ili kudhihirisha sifa zake. Utafiti huu ulikuwa na malengo
mawili ambayo ulitekeleza. Kulikuwa na utambuzi wa sifa bainifu za lugha ya mahubiri
na utambuzi wa aina za mshikamano na jinsi zinavyounganisha. mahubiri. Katika kufanya
hivi, mtazamo wa kimtindo na wa mshikamano katika nadharia ya uamilifu wa lugha
ilitumika.
Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi wa tasnifu imeshughulikia swala la utafiti, sababu
za kuchagua swala lenyewe, madhumuni ya utafiti, upeo wa utafiti, misingi ya
kinadharia, yaliyoandikwa kuhusu somo lile na mbinu za utafiti. Ni katika sura ya pili
ambapo tumejishughulisha na baadhi ya sifa bainifu katika lugha ya mahubiri kama vile
jinsi wahubiri wanavyoanza mahubiri yao, njia wanazoturnia kuendeleza ujumbe, na
namna wanavyohitimisha. Kutokana na uchunguzi wetu tuligundua ya kwamba kuna
mianzo maalum ya kuanza mahubiri. Kwa jumla wahubiri huanza kwa maamkuzi na pia
kutaja kiini cha ujumbe wao.Wahubiri hutumia njia nyingi kuendeleza ujumbe kama vile
matumizi ya mifano takriri, kubadilisha sauti, maswali na kadhalika. Pia, kuna njia
maalum za kutamatisha mahubiri. Katika kila ruwaza iliyojadiliwa, maelezo ya kiisimu
yametolewa.
Sura ya tatu yaonyesha kuwa mahubiri yana sifa ya kuchanganya msimbo. Kuchanganya
msimbo kumeshughulikiwa kama mojawapo ya sifa bainifu katika kuendeleza ujumbe.
viii
•
Aina muhimu za kuchanganya msimbo na JlOS1 zinavyojitokeza katika matini za
uchanganuzi zimejadiliwa.
Sura ya nne yaonyesha kuwa lugha ya mahubiri ina aina mbalimbali za mshikamano.
Kwa mfano, kuna mshikamano wa kimsamiati, urejeshi, uunganishi, ubadilishaji na
udondoshi.
Sura ya tano na ya mwisho inajumuisha muhstasari na matokeo ya utafiti kwa jumla.
Mapendekezo ya utafiti mwingine unaoweza kufanywa katika uwanja huu pia
yamewekwa katika sura hii
Description
Idara ya kiswaillli na lugha za kiafrika Chuo Kikuu cha Kenyatta tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili (Master of Arts) katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. 2001