Tathmini ya Mtalaa wa Isimu Jamii wa Shule za Upili Nchini Kenya
Loading...
Date
2008
Authors
Ngugi, Mwangi Boniface
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia kutathmini mtalaa wa Isimujamii wa shule za upili nchini
Kenya. Utafiti huu ulidhamiria kutathrriini na kuimarisha mtalaa wa Isimujamii katika
lugha ya Kiswahili kama chombo cha mawasiliano kwa kuongozwa na misingi ya
nadharia za ufundishaji wa Lugha ya Pili na Isimujamii. Utafiti huu pia ulibainisha
changamoto zinazowakumba walimu wanapofundisha Isimujamii iliyojumuishwa katika
silabasi ya mtalaa wa sasa. Wilaya ya Thika ilichaguliwa kama eneo la utafiti kwa vile
ina shule za Taifa, Mkoa, Wilaya na za Kibinafsi zilizohitajika kufanyia utafiti.
Ukusanyaji wa data ulifanywa kupitia mahojiano ya walimu, watalaamu wa elimu na
kuchunguza ratiba ya vipindi vya masomo kutoka kidato cha kwanza hadi cha nne.
Dhana ya mitalaa pamoja na uandalizi wa mitalaa imepitiwa kwa vile ni muhimu katika
utekelezaji wa mtalaa wowote mpya. Maoni ya walimu na wakuza mitalaa kuhusu dhana
ya mtalaa na maandalizi yake yamewasilishwa kwa njia ya mjadala. Vile vile,
uchanganuzi wa maoni ya walimu na wakuza mitalaa kuhusu mawanda ya Isimujamii
umeshughulikiwa. Hatimaye matokeo ya utafiti huu pamoja na mapendekezo
yameshughulikiwa ambapo imebainika kuwa, mtalaa wa Isimujamii una udhaifu katika
kumwongoza mwalimu ili aimarishe kiwango cha mawasiliano cha wanafunzi. Walimu
wengi wanasisitiza miundo ya lugha badala ya uamilifu wa lugha. Jambo jingine
linalotinga utekelezaji wa mtalaa wa Isimujamii ni ukosefu wa vifaa vya kufundishia.
Utafiti huu utafaidi sera na upangaji wa lugha. IIi kuimarisha uhusiano mwema katika
jamii yenye lugha nyingi, lugha moja inahitajika. Lugha kama hiyo itapatikana kwa
kuifunza shuleni.
Description
Tasnifu Hii Imewasilishwa katika Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, 2008