Taathira ya dhamira kwa mtindo katika hadithi fupi teule za Kiswahili
Loading...
Date
2011-04
Authors
Ntiba, Onesmus Gitonga
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Katika tasnifu hii tumechunguza athari ya dhamira katika uteuzi wa mtindo katika hadithi
fupi teule za Kiswahili. Tumetumia diwani one za mwaka wa 2007. Diwani hizo ni Damu
Nyeusi no Hadithi Nyingine (2007), Likizo ya Mauti no Hadithi Nyingine (2007), Kurudi
Nyumbani no Hadithi Nyingine (2007) na Alidhani Kapata no Hadithi Nyingine (2007).
Malengo ya tasnifu hii yalikuwa ni kuainisha maswala wanayoshughulikia waandishi wa
hadithi fupi za 2007 katika diwani zao, kudhihirisha dhamira katika hizo hadithi, kubainisha
ni vipi dhamira hizo zinavyouathiri uteuzi wa mitindo wanayoituIDia kuziwasilisha na
mwisho kuangazia jinsi mazingira huathiri utunzi wao. Katika utafiti huu, tuliongozwa na
Nadharia Changamano inayofumbata baadhi ya mihimili kutoka Nadharia ya Uchanganuzi
Saikolojia na Nadharia ya Mtindo. IIi kuipata data faafu, tulitumia mbinu kusudio. Hii ni kwa
sababu huu ni utafiti wa kifasihi unaoziJenga diwani teule. Kutokana na utafiti huu,
tumelipinga wazo kwamba mwandishi wa hadith fupi hana wakati wa kutosha na hivyo basi
anatumia ubanaji unaoathiri dhamira yake. KuJingana na utafiti huu, i1iibuka kuwa
mwandishi ana wakati wa kutosha; ni kuamua tu ameamua kuwasilisha dhamira yake kupitia utanzu wa hadithi fupi. Dhamira ya mwandishi huibua uteuzi wa mtindo unaomwezesha
kuiwasilisha dhamira yake kikamilifu. Pia ilibainika kuwa maswala wanayoshugbulikia
waandishi wa hadithi fupi ni mambo yanayoiathiri jamii ya kisasa.
Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi imeshughulikia maswala ya kikaida kwa mujibu wa
matakwa y~ Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, Chuo Kikuu cha Kenyatta kama vile
swala la utafiti, sababu za kuchagua mada, malengo ya utafiti, misingi ya nadharia,
yaliyoandikwa kuhusu mada hii na mbinu za utafiti.
Katika sura ya pili, chimbuko na maendeleo ya utanzu huu wa hadithi fupi yameangaziwa.
Pia fasili, muundo na sifa zake utanzu huu zimeangaliwa. Katika sura ya tatu, tumeanza
kwa kuyashughulikia mazingira ya waandishi wa hadithi tunazochunguza katika utafiti we.tu .
Pia, tumeshughulikia dhamira za dawa za kulevya, ukiukaj i wa haki za mtoto na swala la
Ukimwi. Haya tumeyashughulikia kupitia hadithi nane. Sura ya one nayo imeangalia
dhamira za kutowajibika kwa viongozi wa kisiasa, migogoro katika ndoa na tamaa ya pesa.
Hapa, dhamira hizi zimeangaliwa katika jumla ya hadithi mahsusi kenda. Namna dhamira
hizi zinavyoathiri uteuzi wa mitindo imechunguzwa katika sura hizi mbili.
Sura ya tano ambayo ni ya mwisho ni hitimisho na matokeo ya utafiti kwa jumla. Pia, imetoa
mapendekezo ya utafiti wa baadaye. Utafiti wetu ulifanikiwa na tuna uhakika kuwa umetoa
mchango wake katika upanuaji wa welewa wa utanzu huu ambao kwa ulinganifu ndio una
historia fupi zaidi katika fasihi ya Kiswahili.
Description
Tasnifu hii imewasilishwa katika idara ya kiswahili na lugha za kiafrika va Chuo Kikuu Cha Kenyatta ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili. Aprili 2011, PL 8704 .N78T3