Athari ya duksi katlka ufunzaji na ujifunzaji wa kiswahili: mtazamo wa uchanganuzi linganishi tasnifu
Loading...
Date
2007
Authors
Wenyaa, Nasaba Salome
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Kazi hii imekusudia kuchanganua athari ya elimu ya Duksi katika ufunzaji na
ujifunzaji wa sarufi ya lugha ya Kiswahili kwa mujibu wa mtazamo wa nadharia ya
Uchanganuzi Linganishi. Vipengele vya kisarufi yaani abjadi, maendelezo, msamiati,
mtindo wa kuandika, mpangilio wa maneno katika sentensi ndivyo vilivyochunguzwa
katika utafiti huu.
Sampuli mseto ndiyo iliyochaguliwa na kuhusishwa. Watafiti walioshirikishwa
walitoka katika wilaya ya Garissa, mjini pamoja na viunga vyake. Tajriba, imani,
elimu, mielekeo na maoni ya wanajamii wa viwango mbalimbali yalizingatiwa. Kazi
hii pia ilizingatia mbinu za kufunzia Kiswahili madhumuni yakiwa ni kuboresha na
kuimarisha ufunzaji na ujifunzaji wa lugha hii katika mkabala wa mazingira ambapo
lugha ya Kiarabu inazingatiwa. Yaani hutumiwa kwa kuendeshea shughuli za kidini.
Kutokana na utafiti huu ilibainika kuwa elimu ya Duksi ina athari chanya na hasi.
'Mbinu za kufunzia zimedhihirisha njia tofauti tofauti zinazoweza kusaidia kuinua
kiwango cha kufunza lugha. Papo hapo kutokana na ukinzano kati ya vipengele vya
kisarufi vya (Kiarabu na Kiswahili), imetambulikana kuwa wanafunzi hupata shida
zinazohusiana na abjadi, maendelezo, hijai, msamiati na maana ya sentensi.
Utafiti huu umependekeza kuwa bado Kuna haja ya kuendeleza elimu jumuifu.
ambapo mbinu changamano zinaweza kutumika. Hii ni kwa sababu mafunzo hayo
yote ya kidini na ya kimagharibi yana manufaa kwa maisha ya wanafunzi wakiwa
shuleni na hata baada ya masomo shuleni.
Description
Iliyotolewa kwa madhumuni ya kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katlka chuo kikuu cha Kenyatta, 2007