MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Title
Now showing 1 - 20 of 258
Results Per Page
Sort Options
Item Athari ya duksi katlka ufunzaji na ujifunzaji wa kiswahili: mtazamo wa uchanganuzi linganishi tasnifu(2007) Wenyaa, Nasaba Salome; King'ei, Kitula; Osore, MiriamKazi hii imekusudia kuchanganua athari ya elimu ya Duksi katika ufunzaji na ujifunzaji wa sarufi ya lugha ya Kiswahili kwa mujibu wa mtazamo wa nadharia ya Uchanganuzi Linganishi. Vipengele vya kisarufi yaani abjadi, maendelezo, msamiati, mtindo wa kuandika, mpangilio wa maneno katika sentensi ndivyo vilivyochunguzwa katika utafiti huu. Sampuli mseto ndiyo iliyochaguliwa na kuhusishwa. Watafiti walioshirikishwa walitoka katika wilaya ya Garissa, mjini pamoja na viunga vyake. Tajriba, imani, elimu, mielekeo na maoni ya wanajamii wa viwango mbalimbali yalizingatiwa. Kazi hii pia ilizingatia mbinu za kufunzia Kiswahili madhumuni yakiwa ni kuboresha na kuimarisha ufunzaji na ujifunzaji wa lugha hii katika mkabala wa mazingira ambapo lugha ya Kiarabu inazingatiwa. Yaani hutumiwa kwa kuendeshea shughuli za kidini. Kutokana na utafiti huu ilibainika kuwa elimu ya Duksi ina athari chanya na hasi. 'Mbinu za kufunzia zimedhihirisha njia tofauti tofauti zinazoweza kusaidia kuinua kiwango cha kufunza lugha. Papo hapo kutokana na ukinzano kati ya vipengele vya kisarufi vya (Kiarabu na Kiswahili), imetambulikana kuwa wanafunzi hupata shida zinazohusiana na abjadi, maendelezo, hijai, msamiati na maana ya sentensi. Utafiti huu umependekeza kuwa bado Kuna haja ya kuendeleza elimu jumuifu. ambapo mbinu changamano zinaweza kutumika. Hii ni kwa sababu mafunzo hayo yote ya kidini na ya kimagharibi yana manufaa kwa maisha ya wanafunzi wakiwa shuleni na hata baada ya masomo shuleni.Item Athari ya mazingira ya kihistoria na kijamii katika uwasilishaji wa maudhui ya dhifa (E. Kezilahabi)(Kenyatta University, 2016) Nasimiyu, Christine M.; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu ulichunguza athari ya mazingira ya kihistoria na kijamii katika uwasilishaji wa maudhui ya diwani ya Dhifa ya E. Kezilahabi (2008). Malengo yalikuwa, kubainisha maudhui yaliyowasilishwa na mtunzi wa Dhifa, kubainisha narnna maudhui haya yalivyowasilishwa na kueleza narnna maudhui haya yalivyoibua mazingira ya kijamii na kihistoria. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Uhistoria Mpya ambayo huangalia umuhimu wa muktadha katika utunzi na uhakiki wa kazi za kifasihi. Pia, huonyesha ya kwamba kadiri jamii zinavyoendelea, utamaduni hubadilika kiwakati na jambo hili huathiri utunzi, uwasilishaji na uhakiki wa kazi za kifasihi. Utafiti huu ulizingatia muundo wa kimaelezo kuhusu suala la utafiti, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Utafiti huu ulifanywa maktabani. Sampuli iliteuliwa kimakusudi ambapo mashairi ishirini na moja yaliteuliwa ili saba yashughulikie kipengele cha siasa, uchumi na masuala ya kijamii. Data ilikusanywa kutokana na usomaji wa kina wa mashairi teule. Uchanganuzi wa data ulizingatia uainishaji wa aina ya maudhui, uwasilishaji wake pamoja na matukio ya kihistoria. Aidha, ulizingatia chimbuko la maudhui, namna yalivyowasilishwa, dhamira na falsafa ya mtunzi. Hayo yote yalifanywa kwa kuzingatia pengo lililonuiwa kujazwa na utafiti huu kwa kuongozwa na nadharia ya utafiti. Utafiti ulibaini na kutambua kwamba, siasa ya Tanzania, baada ya Azimio la Arusha ilichukuwa rnkondo mpya. Aidha, mazingira mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi yalichangia pakubwa katika kuwasilisha maudhui ya diwani ya Dhifa. Inatarajiwa kuwa utafiti huu utawafaa wanafunzi wa shule za upili, vyuo, watafiti wa ushairi na wakuza mitalaa. Tasnifu hii iligawanywa katika sura sita. Sura ya kwanza ilishughulikia mada ya utafiti, maswali ya utafiti, malengo ya utafiti, upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusu mad a, sababu za kuchagua mada na misingi ya nadharia. Sura ya pili ilichunguza historia na falsafa ya mtunzi. Sura ya tatu iliangazia maudhui ya kisiasa. Sura ya nne ilichambua maudhui ya kiuchumi. Sura ya tano iliangalia maudhui ya kijamii. Sura ya sita ilijumuisha muhtasari, hitimisho,matokeo ya utafiti na mapendekezo.Item Athari ya mbinu rejeshi katika hadithi fupi za Kiswahili(Kenyatta University, 2015-11) Musili, Lucia Muli; King'ei, Kitula; Maitara, Joseph N.; Masinde, Edwin W.; Osore, MiriamUtafiti huu ulishughulikia athari ya mbinu rejeshi katika hadithi fupi za Kiswahili. Diwani zilizoshughulikiwa ni za miaka ya elfu mbili nazo ni Mwendawazimu na Hadithi Nyingine (2000) na Kunani Merikani na Hadithi Nyingine (2011). Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya eilmumtindo. Nadharia hii ilimfaa mtafiti katika utafiti huu maana diwani hizi ambazo zimeteuliwa zimesheheni matumizi ya mtindo wa mbinu rejeshi. Utafiti huu umegawanywa katika sura nne. Sura ya kwanza ilitupa mwelekeo wa utafiti wetu. Katika sura hii tumejadili swala la utafiti, malengo ya utafiti na sababu za kuchangua mada. Pia katika sura hii tumejadili misingi ya nadharia, upeo wa mipaka na yalioandikwa kuhusu mada. Mwisho mbinu za utafiti, uteuzi wa sampuli, ukusanyaji wa data uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa data zimeangaziwa, Sura ya pili nayo imejadili matumizi ya mbinu rejeshi katika diwani ya Mwendawazimu na hadithi Nyingine. Katika sura hii mtafiti amebainisha matumizi ya mbinu rejeshi katika diwani hii na athari ya mtindo huu. Sura ya tatu imezingatia matumizi ya mbinu rejeshi na athari yake katika diwani ya Kunani Merikani na Hadithi Nyingine. Sura ya nne ambayo ni hitimisho imekuwa muhtasari, matatizo na mapendekezo ya mtafiti. Utafiti huu unanuia kuwafaidi wahakiki wengine, wasomi na waandishi wa kazi za fasihi. Pia utafiti huu utawasaidia wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vikuu katika kuhakiki kazi zao.Item Athari ya Utenzi Katika Uandishi wa Riwaya Teule ya Kiswahili.(Kenyatta University, 2017-06) Nabangi, Judith Khasoa; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu umejikita katika kuonyesha athari ya utenzi katika uandishi wa riwaya teule ya Kiswahili. Matumizi ya utenzi katika uandishi wa riwaya ni mojawapo ya mbinu za kimtindo za uandishi. Kwa hivyo, utafiti huu umefanywa kwa kuongozwa na malengo matatu ambayo ni: Kudhihirisha jinsi utenzi umechangia uandishi wa riwaya kimaudhui. Pili, kuonyesha mtindo ulivyochangiwa na utenzi katika kuandika riwaya teule. Tatu, kubainisha jinsi wahusika wa riwaya teule wamechangiwa na utenzi. Utafiti ulifanywa ili kuonyesha usemezano wa utenzi na riwaya teule ya Kiswahili. Utafiti huu ulifuata muundo wa kimaelezo na ulifanyiwa maktabani. Utafiti uliongozwa na nadharia ya usemezo ya Mikhail Bakhtin, ambayo inashikilia kwamba tanzu za fasihi husemezana. Sampuli lengwa katika utafiti huu ilikuwa riwaya tatu ambazo ziliteuliwa kimaksudi; Kasri ya Mwinyi Fuad, Msimu wa Vipepeo na Walenisi. Data ilikusanywa kwa kusoma riwaya hizo tatu kwa kina na kunukuu mambo muhimu yanayohusiana na utafiti huu. Mambo haya ni maudhui, mtindo wa uandishi wa riwaya na wahusika wa riwaya teule. Data hiyo ilichanganuliwa kwa kuzingatia maswali ya utafiti. Utenzi unawiana vipi na uandishi wa riwaya kimaudhui? Pili, utenzi unawiana vipi na riwaya teule kimtindo? Tatu, je, kuna uwiano upi baina ya wahusika wa utenzi na wale wa riwaya teule? Aidha, data ilichanganuliwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti, pia, iliongozwa na mihimili ya nadharia ya usemezo. Matokeo ya utafiti huu yamewasilishwa kwa njia ya maelezo na utoaji wa mifano mwafaka. Utafiti huu uligundua kwamba athari za utenzi katika uandishi wa riwaya ni mojawapo ya mbinu za kimtindo za uandishi. Kwa hivyo, kipengele cha utanzu mmoja kinaweza kutumiwa kama mbinu ya kimtindo katika uandishi wa utanzu mwingine.Item Athari za Ekegusii Katika Matumizi ya Kiimbo cha Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Upili Kaunti ya Kisii, Kenya(Kenyatta University, 2023-11) Nyougo, Christine; Peter GithinjiUtafiti huu ulichunguza matumizi ya kiimbo cha Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wanaozungumza Ekegusii kama lugha ya kwanza. Shule tatu zilihusishwa katika utafiti huu: Shule ya upili ya Senior Chief Musa Nyandusi, Nyamondo na Nyabisia. Malengo ya utafiti huu yalikuwa: Kutathmini utamkaji na ufasili wa kiimbo cha Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wanaozungumza Ekegusii kama lugha ya kwanza, kuchunguza jinsi viarudhi vya lugha ya Ekegusii vinavyoathiri kiimbo cha Kiswahili. Kutathmini jinsi usuli wa lugha na tajriba ya wanafunzi inavyochangia matumizi bora ya kiimbo katika uzungumzaji wa Kiswahili. Ili kuafiki madhumuni haya, maswali yafuatayo yalitumiwa: Je, wazungumzaji wa Ekegusii hufasili vipi kiimbo cha Kiswahili sanifu? Viarudhi vingine vya Ekegusii huathiri kiimbo cha Kiswahili vipi? Usuli na tajriba ya wanafunzi huchangia vipi katika matumizi bora ya kiimbo cha Kiswahili? Nadharia ya ujifunzaji wa kiimbo cha lugha ya pili iliyoasisiwa na Mennen (2015) ilitumiwa katika kuchunguza matumizi ya kiimbo. Utafiti huu ulifanywa maktabani na nyanjani. Maktabani ulihusu kusoma matini, vitabu, tasnifu, majarida na makala mtandaoni kuhusu kiimbo. Nyanjani ulijumuisha matumizi ya hojaji funge na wazi katika kupata tathmini ya wanafunzi ya sampuli ya data waliyopewa na mtafiti. Vilevile, mbinu ya mahojiano ambayo yalirekodiwa ilitumika kwa walimu wanaofunza Kiswahili. Pia, uchunzaji wa kushiriki ulitumiwa. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo, majedwali, michoro na chati. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa lugha ya Ekegusii huathiri matumizi ya kiimbo sahihi cha Kiswahili. Wazungumzaji wa Ekegusii walionyesha athari katika usomaji na ufasili wa kiimbo cha Kiswahili. Ilibainika kuwa viarudhi vingine vya Ekegusii huathiri matumizi ya kiimbo cha Kiswahili. Utafiti ulithibitisha kuwa jinsia huchangia katika matumizi sahihi ya kiimbo ambapo ilidhihirika kuwa jinsia ya kike hutumia kiimbo sahihi katika mazingira rasmi ikilinganishwa na jinsia ya kiume. Tajriba pia huchangia kiimbo sahihi pale ambapo wanafunzi ambao wamekuwa shuleni kwa muda mrefu huzungumza kwa kiimbo bora. Vifaa vya kisasa pia huchangia kuboresha matumizi ya kiimbo sahihi cha Kiswahili. Tunapendekeza walimu wakuze matumizi ya vifaa vya kisasa katika ufundishaji wa kiimbo cha Kiswahili, kuwepo sheria shuleni kuhusu matumizi ya Kiswahili katika mazingira rasmi na ufundishaji wa kiimbo utiliwe maanani kuanzia viwango vya chini vya elimu.Item Athari za Katama Mkangi kwa John Habwe: Mfano Kutoka kwa Riwaya Teule za Mafuta (1984) na Cheche za Moto (2008)(Kenyatta University, 2023-11) Musyoka, Kalingwa Felix; Titus M. KauiUtafiti huu unashughulikia athari za Katama Mkangi kwa John Habwe kwa kujikita katika riwaya teule za Kiswahili za Mafuta (1984) na Cheche za Moto (2008). Utanzu wa riwaya ya Kiswahili umeendelea kupanuka kimaudhui na kifani kutokana na juhudi za watunzi mbalimbali kama vile Katama Mkangi na John Habwe. Japo tafiti za awali zimetafitia suala la mwingiliano matini, tafiti nyingi zimejikita katika kazi za mtunzi mmoja.Utafiti wa kina ulihitajika kuchunguza namna utunzi wa Mafuta (1984) ulivyoathiri John Habwe alipoitunga riwaya yake ya Cheche za Moto (2008). Katama Mkangi aliandika riwaya ya Mafuta katika wakati wa chama kimoja cha kisiasa ambapo uhuru wa kujieleza ulikuwa umebanwa sana. Habwe ameandika kazi yake ya Cheche za Moto katika mazingira yaleyale, miaka ishirini na minne baadaye. Wakati wa utunzi wa Cheche za Moto, uhuru wa kujieleza ulikuwa umepanuliwa. Kwa hivyo, amekwepa mtindo wa kimajazi alioutumia Mkangi na kuyaangazia masuala anayoyaibua Mkangi kwa njia wazi. Utafiti huu uliongozwa na malengo matatu: kwanza, ni kufafanua namna mwangwi wa maudhui ya riwaya ya Mafuta unavyojitokeza katika riwaya ya Cheche za Moto, kubainisha athari za usawiri wa wahusika wa Katama Mkangi kwa John Habwe, na mwisho, kuonyesha athari za kimtindo za Katama Mkangi kwa John Habwe. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya mwingiliano matini iliyoasisiwa na Julia Kristeva (1969). Mihimili mikuu ya nadharia hii iliyoongoza utafiti huu ni pamoja na: hakuna matini ya fasihi yenye sifa za pekee, matini hubainisha sifa mbalimbali za matini tangulizi, na mwisho, matini ya baadaye huweza kufafanua dhana fulani kutoka matini tangulizi kwa njia inayoeleweka. Nadharia hii ya mwingiliano matini ilisaidia pakubwa kuonyesha namna kazi ya awali, Mafuta (1984) ilivyomwathiri John Habwe katika utunzi wa Cheche za Moto (2008), kimaudhui na kifani. Riwaya ziliteuliwa kimakusudi ili kupata sampuli faafu yenye data ya kujaza pengo la utafiti. Data ilikusanywa kupitia kwa usomaji wa maktabani na vilevile kusakura mitandaoni kuhusu vipengele vya mwingiliano matini katika riwaya ya Kiswahili. Data hii imewasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Utafiti huu unatarajiwa kutoa mchango katika uhakiki wa utanzu wa riwaya ya Kiswahili, hususan kuhusu kipengele cha kuathiriana baina ya watunzi wa riwaya za Kiswahili.Item Athari za Matukio ya Kihistoria Katika Riwaya za Nyongo Mkalia Ini na Mafamba(Kenyatta University, 2022-04) Ndung’u, Beatrice Wanjiku; Richard Wafula; Jessee MurithiThis research study investigated the effect of historical events on the selected two novels Nyongo Mkalia Ini (Chimerah, 1995) and Mafamba (Olali, 2008). The effects of historical events that include political, administrative, economic and social issues in general and how they affect the presentation of themes, characters and style and language is an issue that has not been addressed as a specific research research topic in the novel. The aim of this research has been to investigate whether historical events affect how novelists portrays themes in their literary works, investigate how historical events affect characterization and investigate how historical events affect the linguistic styles in swahili novel. The research has employed new historicism theory which was founded by Greenblatt (1980). New historicism theory puts into consideration contextual importance in composing and analyzing literary work. The theory also stipulates that, as the society develops; cultural changes occur that consequently affects composition, depiction and analysis of literary works. The topic on effect of historical events to the development of Swahili novel is important for various reasons. This research has been done in the library through reading the selected novels, journals and prior literary works relevant to the research. Research findings have be presented through analysis and explanations. The research has been presented in five chapters. The research has shown the effects of historical events on Nyongo Mkalia Ini and Mafamba. The research has shown that historical events have affected writers in depicting their themes, characters and linguistic styles in Nyongo Mkalia Ini and Mafamba respectively.Item Athari za Sheng’ kwa Kiswahili Sanifu: Uchunguzi wa Kamusi ya Sheng’.(Kenyatta University, 2023) Muyumba, Jotham; David KiharaUtafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ –English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchunguzi huu kwa sababu ndio kamusi ya kwanza ya Sheng’ kuwahi kuchapishwa. Licha ya kamusi hii kuchapishwa katika lugha ya Kiingereza ina leksimu za Sheng’ ambazo yafaa kuchunguzwa namna zinavyoathiri Kiswahili sanifu kwa wakati wa sasa. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kubainisha maneno yaliyomo katika Sheng’- English Dictionary na katika Kiswahili sanifu. Kadhalika, utafiti huu ulinuia kueleza muundo wa kifonolojia wa maneno ya Sheng’ na jinsi yanavyotofautiana na Kiswahili sanifu. Mwisho, utafiti huu ulidhamiria kueleza sababu za utofauti wa muundo wa kifonolojia wa maneno ya Sheng’ na kueleza athari zake kwa Kiswahili sanifu. Nadharia ya utafiti ilikuwa Nadharia ya Fonolojia Boreshi ambayo inapatikana katika mtazamo mpana wa Nadharia Boreshi iliyoasisiwa na Alan Prince na Paul Smolensky (1991). Hii ni nadharia inayochunguza hatua za ukuaji wa msamiati kutoka hali ghafi hadi ukubalifu wake kupitia kwa vizuizi tofauti. Mahali pa utafiti palikuwa maktabani na mtandaoni. Mbinu ya uchunguzi ikawa kupitia kusikiliza wazungumzaji wa Sheng’ na kusoma makala mbalimbali kuhusu mada hii. Data ilikusanywa kupitia kwa kuchunguza maneno na vidahizo vya maneno kutoka kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003). Iliaminika kuwa kamusi hii ingetoa sampuli ya maneno mahsusi ya Sheng’ ambayo muundo wake huathiri matumizi katika Kiswahili sanifu kwenye jamii ya kisasa. Uchanganuzi wa maelezo ulitegemea mtazamo wa Fonolojia Boreshi katika nadharia ya fonolojia inayoangazia sarufi zalishi. Katika mtazamo huu, uambishaji wa maneno uliangaziwa na jinsi uundaji huo hutawaliwa na vizuizi mbalimbali na sheria za fonolojia. Kadhalika nadharia ya Fonolojia Boreshi ilitumika kueleza michakato ya namna wazungumzaji wa Sheng’ hubuni leksimu mbalimbali katika mawasiliano. Uwasilishaji wa data ulikuwa kupitia kwa maelezo ya kina, michoro na jedwali. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa: maneno yanayopatikana katika Sheng’ – English Dictionary na Kiswahili sanifu yalibainishwa. Pia, muundo wa kifonolojia wa maneno ya Sheng’ na namna yanavyotofautiana na Kiswahili sanifu ulielezwa. Kadhalika, sababu zinazochangia utofauti wa muundo wa kifonolojia wa maneno ya Sheng’ na Kiswahili sanifu zilielezwa. Uchunguzi huu ulidhamiria kuchangia usomi wa Kiswahili kwa kuweka wazi athari za Sheng’ katika ukuaji wa lugha ya Kiswahili kimsamiati. Kadhalika, utafiti huu utawasaidia wanafunzi kuweka mipaka bayana kati ya msimbo wa Sheng’ na lugha ya Kiswahili sanifu.Item Changamoto Katika Ujifunzaji Fonolojia Arudhi ya Kiswahili Katika Shule za Upili, Gatuzi la Homabay, Kenya(Kenyatta University, 2023-05) ‘Wagabi, Wanga James; Jacktone O. OnyangoAbstractItem Changamoto za Kimofosintaksia Miongoni Mwa Wanafunzi wa Kiswahili wa Shule za Upili Wilayani Muhanga, Nchini Rwanda(2014-07-31) Ntawiyanga, SylvainPendekezo hili la utafiti linatarajia kuchunguza "Changamoto za kimofosintaksia miongoni mwa wanafunzi wa Kiswahili wa shule za upili wilayani Muhanga, nchini Rwanda". Katika utafiti huu, makosa ya kimofosintaksia yanayofanywa na wanafunzi hawa yatachunguzwa kwani kipengele hiki huchukuliwa kama kiini cha lugha yoyote ile. Vipengele vingine vya sarufi huingiliana nacho na kukitegemea kwa kiwango kikubwa. Kwa hivyo, utafiti huu unalenga kubainisha makosa ya kimofosintaksia yanayofanywa na wanafunzi wa Kiswahili wa shule za upili wilayani Muhanga, kuainisha makosa hayo; kuyaeleza na kutathmini mikakati inayozingatiwa kupunguza makosa hayo. Utafiti huu utaongozwa na nadharia za Uchanganuzi Makosa (UM) na ile ya Lugha Kadirifu (LK). UM unatilia mkazo mbinu za kuichunguza lugha ya mwanafunzi kwa kubainisha makosa anayoyafanya, aina za makosa hayo, kuyaeleza na kuyatathmini. Nayo LK inachunguza lugha ya mwanafunzi kwa kuzingatia mikakati ya isaikoljia katika mchakato unaoendelea wa ujifunzaji wa L2. Katika LK, vyanzo vya makosa yanayofanywa na mwanafunzi huchunguzwa kutegemea mikakati hiyo ya kisaikolojia ambayo mwanafunzi anatumia katika jitihada zake za kujifunza L2. Kwa hivyo, kupitia uzingatifu wa nadharia hizi, matokeo ya utafiti huu yatasaidia kutoa mapendekezo mwafaka kwa washikadau wa ufundishaji wa Kiswahili wa shule za upili nchini Rwanda ili kupunguza makosa ya kisarufi yanayofanywa na wanafunzi hawa. Utafiti huu utakuwa wa kimaelezo na data zitakusanywa nyanjani kwa kuzihusisha shule tatu wilayani Muhanga ambazo ni Groupe Scolaire de Kirwa, Groupe Scolaire de Nyarusange na shule ya Groupe Scolaire de Shyogwe. Mbinu ya kimakusudi itazingatiwa katika usampulishaji na watafitiwa watapatikana kwa kutumia mbinu nasibu ambapo wanafunzi kumi watachaguliwa katika madarasa ya tano na sita kutoka kila shule iliyoteuliwa. Hojaji na mahojiano ndiyo yatakayozingatiwa na mtafiti kukusanya data kutoka kwa wanafunzi hao na walimu wao. Uwasilishaji wa data utafanywa kwa njia ya kimaelezo ambapo majedwali na vielelezo vitatumika ili kufafanua zaidi matokeo ya utafiti huu.Item Changamoto za mikondo mipya ya utunzi wa mashairi ya kiswahili: mfano wa tunu ya ushairi(Kenyatta University, 2015) Onyancha, Judy Wangari; King'ei, Kitula Osore, MiriamThis study investigated the challenges brought about by new stylistic perspectives in Kiswahili poetry. The main objective was to identify new stylistic perspectives in Kiswahili poetry, the settings which contributes to the new patterns of poetic compositions, and the challenges brought about by these new perspectives. In achieving the objectives of the study, the research was guided by the theory of stylistics which was expounded by among others Coombs (1953), Leech (1961). The study has analysed data from an antology entitled diwani ya Tunu ya Ushairi. Inorder to achieve these goals, the study analysed poems from the antology of diwani ya Tunu which apart from focusing on the well known stylistic perspectives, also has got new stylistic modes of style in Kiswahili prosodic poetry. These new styles in Kiswahili poetry have made it necessary to revist our understanding on how Kiswahili poetry is described and categorized. The research was mainly library based where background reading was done on relevant theories on the criticism and reading of Kiswahili poetry. In addition, information on various issues regarding the styles of poetry was gathered. A sample of Kiswahili poems from diwani ya Tunu ya Ushairi was selected using purposive sampling techniques. Using this primary data, the researcher did indepth reading and analysis of the new stylistic attributes under the guidance of the theory of the stylistics. The results were convyed using a descriptive approach using of examples as per the objectives and organized into five chapters. The research found out that development of poetic composition has no end. Therefore, there is need to review the concepts and terminologies used inorder to be in consonant with current trends.Item Chuo Kikuu cha Kenyatta Shule ya Sanaa na Sayansi za Jamii Idara ya Kiswahili Dhima za Hurafa Katika Fasihi ya Watoto(Kenyatta University, 2019-11) Ngiti, Agnes Makandi; King'ei, Kitula Osore, MiriamThis study is about the role of fables in children’s literature. Its main objectives are to evaluate the role, themes and literal devices used in fables to make them significant to children. It was a descriptive research done in the library. Purposeful sampling was used to select three fables. These were: Ngiri Mganga (2010) by Kariuki, Sungura na Mbwa (2011) by Nyakeri and Sisimizi Amuua Tembo (2004) by Mayega. Data was collected and analyzed according to research questions and objectives. The research was guided by two theories; semiotic and narratology, whose scholars are Pierce (1977) and Prince (2003) respectively. The Semiotic theory analyzes the meaning of the fables to children. It depicts the roles they play in educating chidren. Fables are themed to relay specific lessons to children. The narratology theory describes the style used by the writer. Writters ensure fables are written in a manner that enables childern to understand them easily. The role of animal characters in children’s literature is explained. The findings were described and summarized. The importance of fables to children is explained. The research is beneficial to authors, university students and any one else interested in children’s literature.Item Code switching in the contemporary Kiswahili rap song(2012-01-03) Munuku, Anne WangariThis is a sociallinguistic study that investigates code switching in the contemporary Kiswahili rap song. It seeks to identify, interprete and explain the patterns code switching, the constraints governing these patterns and the communicative functions of code switching in the songs. The study is organized in five chapters covering different areas of code switching. Chapter one forms the introduction of the study comprising the statement of the problem, research objectives and assumptions, justification for the study and the scope and limitation of the study. Literature review, theoretical framework and the research methodology are also presented in this chapter. Code switching takes place in a given pattern constrained by various grammatical and structural factors. This is discussed in chapter two. Chapter three consists of the stylistic strategies that these artists employ in their songs for various communicational purposes. The social symbolism and the communicative functions of the codes are outlined in chapter four. The focus is on how artists make code choices based on societal expectations and norms. Chapter five forms the conclusion of the study. It includes the summary of the research findings as well as the conclusions drawn from these findings. The recommendations for further research are also outlined.Item A comparative study of Ekegusii, Lulogooli and Lwitakho: the phonological, lexical and morphosyntastic structures(2012-05-17) Ingonga, Lilian Indira; Muthiani, JosephThis research project is the study of the grammatical errors in standard eight pupils’ written work in English. The specific objectives of this study were as follows: (1) To establish the types of grammatical errors in the pupil’s written work. (2) To assess the comparative frequency of the different types of errors. (3) To infer the cause(s) of the most frequent type of grammatical error. We chose a heterogeneous group of a hundred and twenty subjects from four city schools. In order to obtain the required data, the subjects wrote a composition. We marked it noting the systematic deviations, or errors, for our analysis. Various types of errors were determined. Verb group errors (past tense errors) had the highest frequency count and we also observed that the psycholinguistic strategy of overgeneralization was their main cause. We then attempted a specification of the possible pedagogic implications of these findings. In our view, this research project is significant in a number of ways. Being the first of its kind in Kenya, its findings will be of great use to practicing teachers of English in our schools. This because the findings point out the priority areas of content to focus on as well as its weightage. In the same vein, the findings will be of use to would-be writers of standard eight English textbooks and curriculum developers at K.I.E.Item Dhima ya lugha teule katika kuwasilisha taswira ya mtoto katika jamii ya abagusii tasnifu(Kenyatta University, 2018) Ombaye, Robert Omuga; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu ulichunguza dhima ya lugha teule katika kuwasilisha taswira ya mtoto katika jamii ya Abagusii. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kutambua lugha iliyowasilisha taswira ya mtoto na kubainisha dhima na athari zake katika jamii ya Abagusii. Nadharia ya Ethnografia ya Mawasiliano iliyoasisiwa na Hymes (1964) ilitumika katika utafiti huu. Nadharia hiyo ilifaa kwa sababu iliangazia jinsi mawasiliano yalivyochanganuliwa kwa kuzingatia vipengele vya: mada, umbo la ujumbe, muktadha, wahusika, sababu za mawasiliano, kanuni za ufafanuzi wa ujumbe, njia za mawasiliano na utendaji. Data ya kimsingi ilipatikana kutoka eneo bunge la Nyaribari Chache, Ugatuzi Mdogo wa Kisii ya Kati, Kaunti ya Kisii. Aidha, data nyingine ilikusanywa maktabani kwa kusoma vitabu, kumbukumbu, ripoti, tasnifu, makala na majalida kuhusu mada ya utafiti. Nyanjani mtafiti alitumia sampuli iliyoteuliwa kwa kutumia mbinu ya kimakusudi kuwahoji watu sabini na wawili. Mbinu ya makusudi ilitumiwa kupata watafitiwa walioimudu vyema lugha ya Ekegusii kuhojiwa ili kupata matokeo faafu. Mtafiti aliwahoji watu wawili (2) kutoka kila kikundi; watoto, vijana, watu wazima, naibu wa machifu, machifu na wataalamu wa haki za watoto kutoka wodi sita (6) za eneo bunge la Nyaribari Chache. Vifaa vilivyotumiwa kuwahoji ni hojaji wazi na maswali ya mahojiano ya ana kwa ana na wahojiwa. Data iliyokusanywa ilirekodiwa na kuchanganuliwa kwa kuzingatia maswali, malengo na nadharia ya utafiti. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa kutumia maelezo na yalibainisha kuwa, lugha hasi na chanya ilitumika katika kuwasilisha taswira mbalimbali za watoto katika jamii ya Abagusii. Matokeo ya utafiti huu vilevile yalibainisha kuwa dhima za lugha hiyo ni: kuelimisha, kukuza maadili, kuonya, kurekebisha tabia, kuwasiliana, kutia motisha, kusifu, kufariji, kulinganisha, kushauri na kukemea. Aidha, matokeo ya utafiti huu yalibainisha kuwa lugha hiyo ilizua athari kadhaa kwa mtoto ambazo ni: kuhama kutoka nyumbani kwao, kutelekezwa, kubaguliwa, kukata tamaa, kuchanganyikiwa akili, kuwa na tabia nzuri au mbaya, kupendwa, kukubalika na kufurahi. Utafiti huu ulikuwa wa manufaa katika jamii ya Abagusii kwa vile uliwawezesha kuelewa kuhusu lugha iliyowasilisha taswira ya mtoto. Ufahamu wa lugha hiyo ni muhimu kwa vile ulichangia katika kuamua maisha ya mtoto siku za usoni. Aidha, ufahamu huo ulichangia pakubwa katika utoaji wa mielekeo, maoni na matendo ya watu wazima kwa watoto katika jamii ya Abagusii.Item Dhima ya Usimulizi Katika Uwasilishaji wa Nyimbo za Taarab(Kenyatta University, 2022) Misoi, Dorcas; Richard M. WafulaThis research aimed at investigating narration in taarab songs with the aim of identifying the role of narration aspects in presenting taarab songs. The narrative aspects that were investigated were narrative time, characterization, narrative levels and voices and speech representation. The researcher used narrative theory. This theory is associated with a Greek Philosopher known as Plato, it was later developed by narratologists like Genette, Stanzel. Manfred Jahn and Mieke Bal. It pertains narration of a story. The tenets of this theory is that, a narrative hasa narrator, a story, speech that represents an act and characters. The objectives of this research wereto identify the various narrative aspects in taarab songs and how the narrative aspects in taarab songs make them to be termed as narratives,to show how narrative aspects helps in bringing out various themes in taarab songs and to show how narratives aspects aid in stylistic devices in taarab songs. Data collection was done in the library. Books, journals and thesis related to our topic of study were studied in detail. Primary data was collected from taarab songs that were selected by purposive sampling were listened to, recorded and interpreted. Tools that were used in collecting and recording data were note books and pens. Data collected were analyzed by narrative theory. Report of this research was presented in five chapters. This research contributed to the scholarship of the song as a genre of oral literature specifically the taarab song. It showed that taarab songs has narrative and poetic characteristics. Finally, it has demonstrated that taarab song is a slippery genre which bears the characteristics of a narrative.Item Dhima ya utawala wa nabongo mumia katika maenezi ya lugha ya kiswahili ubukusuni, Mkoani Magharibi (Kenya)(Kenyatta University, 2009) Nakhisa, Andrew W.; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu umeeleza na kuchanganua dhima ya utawala wa Nabongo Mumia katika maenezi ya lugha ya Kiswahili Ubukusuni, Magharibi mwa Kenya. Utafiti huu ulijikita katika kipindi cha utawala wa Nabongo Mumia tangu kutawazwa kwake kama Chifu Mkuu, mnamo mwaka wa 1910 hadi kifo chake katika mwaka wa 1949. Katika utafiti huu, tutalenga kuainisha, kueleza kuchunguza na kuchanganua mikakati iliyotumiwa na Nabongo Mumia kuchangia maenezi ya lugha ya Kiswahili. Katika kulifafanua swala la utawala, misingi iliyowekwa ili kufanikisha maenezi ya lugha ya Kiswahili iliangaliwa. Maendeleo na mabadiliko yaliyojikita katika asasi muhimu kama dini ,biashara, ndoa na maingiliano ya kijamii kwa kuitumia mizani ya mifanyiko ya kijamii yalichangia maenezi ya lugha ya Kiswahili Ubukusuni. Lugha ya Kiswahili ilipata hadhi kubwa katika kipindi hiki kwa sababu iliendesha shughuli nyingi za Nabongo Mumia ambaye alikuwa mshiriki wa karibu wa mkoloni. Utafiti huu basi umebainisha nafasi muhimu ya utawala wa Nabongo Mumia katika kuwekea lugha ya Kiswahili msingi thabiti wa kuenea Ubukusuni. Tasnifu hii imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi imeshughulikia swala la utafiti, sababu zakuichagua mada, upeo wa utafiti, madhumuni ya utafiti, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za mtafiti. Sura ya pili imechunguza historia ya jamii mbili - Ababukusu na Abawanga - hasa jinsi walivyoingiliana na kuathiriana. Sura ya tatu inaangalia dhima ya utawala wa Nabongo Mumia katika maenezi ya Kiswahili. Sura ya nne imeangazia asasi nyinginezo kama dini, mahakama, ndoa miongoni mwa nyingine. Mwisho, sura ya tano ni hitimisho. Mtafiti arnetoa muhtasari, matokeo kuhusu utafiti, mapendekezo ya utafiti zaidi na matatizo yaliyokumba utafiti huu. Kutokana na utafiti huu imedhihirika kwamba utawala ulichukua nafasi muhimu zaidi katika maenezi ya lugha ya Kiswahili Ubukusuni. Pili, utafiti huu umeonyesha kwamba Babukusu walikuwa wategemezi kwa kuwa katika kuitumia lugha ya Kiswahili, walianza kuunga mkono utamaduni wa kigeni. Mwisho, asasi kama ndoa, dini, biashara, mahakama za Kiafrika, elimu, muziki, michezo na miundo misingi ilifanikiwa Ubukusuni kwa sababu ya kutumia lugha ya Kiswahili. Kwa kiasi kikubwa asasi hizi zilifanikishwa na utawala wa Nabongo Mumia.Item Dhuluma dhidi ya watoto katika riwaya za kiswahili(2011-11-16) Kavuria, Peter N.Utafiti huu umeshughulikia maudhui ya dhuluma dhidi ya watoto kama vanavyobainika katika riwaya teule za Kiswahili. Mtafiti amehakiki kazi teule za waandishi za riwaya zilizoandikwa na waandishi wa k ke na wa kiume. Riwaya zilizohakikiwa ni: Siku Njema, ya K. Walibora, :. Momanyi, Yatima ya K.Wamitila. na k pimo cha Alizani ya :-.Burhani . nadharia iliyotumiwa katika utafiti huu ni ya Ukata tamaa na ushari Nadharia hii hujumuisha mambo ya kibinafsi na ya!e ya kijam ambayo yanaweza kue!eza chanzo cha aina nyingi za dhuluma. Tasnifu hii imegawika katika sura tano. Sura ya kwan za imeshug hulika mada ya utafiti, malengo ya utafiti na sababu za kuchagua mada Vilevile imegusia udurusu wa tafiti za awali, misingi ya nadharia, ukusanyaji w a data pamoja na uchanganuzi na uwasilishaii wa data. Sura ya pili imetalii aina mbalimbali za dhuluma zinazowakabili watoto zinavyodhihilika pamoja na athari zake. Katika sera ya tatu, wanajamii wanaotekeleza dhuluma dhidi ya watoto wameonyeshwa Sura ya tano nayo imeshughulikia tofauti na ukubaliano wa waandishi wa kiume na wa kike kuhusu dhuluma kwa watoto. Sura ya tano ni hitimisho linalotoa muhtasari na matokeo ya utafiti huu pamoja na mapendekezo ya mtafiti. Mwisho Kuna marejeleo ya utafiti huuItem Dhuluma za Kitabaka katika Riwaya za Mkamandume na Shetani Msalabani(Kenyatta University, 2021) Kausi, Barasa George; Kitula King‟ei; Japhet M. MukobwaUtafiti huu umebainisha namna masuala ya dhuluma za kitabaka yanavyojitokeza katika riwaya za Mkamandume (2004) na Shetani Msalabani (1982). Waandishi wa riwaya hizi; Said A. Mohamed na Ngugi wa Thiong’o mtawalia wametuchorea picha halisi ya namna dhuluma za kitabaka zimekithiri katika jamii wanamoishi. Katika riwaya teule, wahusika wanyonge kutoka tabaka la chini wamedhulumiwa na wahusika wa tabaka la juu kwa misingi ya kiuchumi. Hali hii imechangia utengano uliopo baina ya wahusika maskini na matajiri katika riwaya za utafiti. Malengo ya utafiti yalikuwa ni kuonyesha jinsi dhuluma za kitabaka zinavyobainika katika riwaya teule, kubainisha athari zake kwa wahusika na kuchunguza mbinu wanazotumia wanyonge kujikomboa na kujiimarisha kimaisha. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Uhakiki wa ki-Marx ambayo iliasisiwa na Karl Marx na Engles (1959). Nadharia hii inaeleza kuwa historia ya maisha ya binadamu inaweza kuelezeka katika misingi yakinifu ya kiuchumi ambayo huchunguza njia kuu za uzalishaji na usambazaji mali. Tabaka la juu lenye watu wachache huwa na uwezo mwingi kiuchumi kuliko tabaka la chini lenye watu wengi wasiomiliki mali. Pia huonyesha namna jamii huimarika kutokana na migogoro ya kitabaka baina ya watu wa tabaka la chini dhidi ya wale wa tabaka la juu. Utafiti huu uligundua kwamba riwaya za Mkamandume na Shetani Msalabani zimeonyesha kwa undani namna tabaka nyonyaji linavyowanyonya wachochole wa tabaka la chini. Riwaya hizi zimebainisha suala la kiuchumi kama chanzo cha dhuluma zinazowakumba wahusika wanyonge. Aidha, dhuluma hizi zimesababisha athari chungu nzima katika tabaka la walalahoi. Vilevile, utafiti huu umebainisha kuwa wanyonge katika riwaya teule wanaungana na kujikomboa kiuchumi, kisiasa na kielimu. Mbinu walizotumia kupigania ukombozi ni: maandamano, migomo kazini, kuelimika kimasomo, uandishi wa vitabu vya fasihi na kuanzisha biashara ili kujikimu kimaisha. Utafiti huu utawazindua wahusika wanyonge kujikomboa dhidi ya dhuluma za kitabaka katika jamii.Item Dini kama chombo cha kuwadhulumu waumini: mifano kutoka fasihi katika kiswahili(Kenyatta University, 2011-05) Ng'etich, Kiprugut Daniel; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu umeshughulikia dini kama chombo cha kuwadhulumu waumini katika fasihi andishi ya Kiswahili. Vitabu vilivyoteuliwa na kutumiwa katika utafiti ni : Nitaolewa Nikipenda (1982), Masaibu ya Ndugu Jero (1974), Nguvu ya Sala (1999) na Paradiso (2005). Katika sura ya kwanza ya utafiti tumetanguliza utafiti huku tukijadili mambo yafuatayo kwa kina: utangulizi, swala la utafiti, maswali ya utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu ya kuchagua mada, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada, mbinu za utafiti, upeo na mipaka ya utafiti na mbinu za utafiti. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya udenguzi na nadharia ya maadili. Sura ya pili imeweka wazi namna ambavyo dini inadenguliwa kuwa chombo cha dhuluma katika tamthilia ya Nitaolewa Nikipenda na Masaibu ya Ndugu Jero. Katika sura ya tatu tumeeleza jinsi dini inadenguliwa kuwa chombo cha udhalimu katika riwaya ya Paradiso na Nguvu ya Sala. Katika sura ya nne tumefafanua aina za dhuluma za kidini na visababishi vyake. Sura ya tano nayo imejadili athari za dhuluma na jinsi waandishi wa fasihi wametumia mbinu za kisanaa kuunga au kupinga udhalimu wa kidini. Tumehitimisha utafiti wetu na kutoa mapendekezo kwa tafiti zijazo katika sura ya sita. Data za utafiti zimekusanywa, kuchanganuliwa na kuwasilishwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti na nadharia teule. Uwasilishaji wa data umefanywa kwa njia ya kimaelezo. Utafiti huu ulimulika kwa undani udhalimu wa kidini. Tulionyesha kuwa dini ni asasi muhimu sana katika jamii. Asasi hii muhimu inaweza kutumiwa kukuza maadili na umoja wa kijamii. Hata hivyo, baadhi ya waumini wametumia nafasi hii kuwadhulumu wenzao. Tulionyesha kuwa ni rahisi kutumia dini kama chombo cha udhalimu kwa sababu aghalabu binadamu hukwepa kupinga chochote kinachohusiana na Mungu au miungu. Nadharia ya udenguzi ilitusaidia kufafanua unafiki wa viongozi wa kidini na nadharia ya maadili ilitufaa katika kujadili dhima ya dini miongoni mwa wanajamii.