Uamilifu wa Tonisho Katika Sentensi za Kikamba

Loading...
Thumbnail Image
Date
2009
Authors
Muinde, Sarah Nthenya
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulitekelezwa kwa madhumuni ya kuchambua na kujadili ruwaza za tonisho katika sentensi za Kikamba, ili kubainisha muundo na uamilifu katika nyanja za sintaksia na pragmatiki. Uchanganuzi ulitegemea mihimili ya Sarufi Amilifu Mfumo, hasa amali za lugha, tanzu za kisarufi na mitazamo ya kishazi. Nadharia ya Sarufi Amilifu Mfumo ilishirikisha misingi ya kimuundo ya Sarufi Zalishi. Swala la utafiti lilikuwa kudhihirisha uamilifu wa tonisho katika sentensi za Kikamba kupitia dhima za kisintaksia na kipragmatiki. Mbinu za utafiti zilijumuisha nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yaliwakilishwa kwa njia ya maelezo katika sura nne. Sura ya kwanza ilichambua usuli wa mada na kubainisha suala la utafiti, malengo na tahakiki za utafiti, misingi ya kuchagua mada, tahakiki ya maandishi, misingi ya kinadharia na mbinu za utafiti. Sura ya pili ilifafanua muundo wa sentensi za Kikamba. Dhima kuu ya sura hii ilikuwa kutambulisha maneno na kuchanganua miundo virai vyake, kwa madhumuni ya kuwakilisha sentensi za Kikamba. Uchanganuzi wa kishazi ulifanywa kupitia mitazamo mitatu ya kishazi. Ruwaza za tonisho katika hivi vishazi zilibainishwa kwa mujibu wa maana na uamilifu wake katika sura ya tatu. Tonisho ni kigezo muhimu katika sarufi ya Kikamba na ina mchango katika uwanja wa sintaksia kwa jumla pamoja na utumikizi katika ufundishaji wa lugha.
Description
Department of Kiswahili and African Languages, 143p. 2009
Keywords
Citation