Utohozi fonolojia wa maneno - mkopo ya dholuo kutoka kwa Kiswahili
Loading...
Date
2008-11
Authors
Omondi, Olal Anne
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Kazi hii inatekeleza madhumuni ya kuchambua maneno-mkopo ya Dholuo yanayotokana
na lugha ya Kiswahili. Kuwepo kwa maneno mageni yanayoshabihiana na Kiswahili
kulizua haja ya kueleza vipi Dholuo inavyoyaruhusu maneno hayo kutumika sawia na
leksia zake asilia. Tatizo hili ndilo linaloshughulikiwa katika uchanganuzi wetu kama
namna ya kuangaza jinsi Dholuo inavyoelekeza fonolojia yake kudhihirisha ukubalifu na
usarufi wa utohozi ndanimwe.
IIi kufanikisha uchambuzi wa mantiki ya mada yetu, tumeteua nadharia inayoafiki
malengo ya utafiti wetu. Nadharia tulizotambua kutufaa ni Fonolojia Tenganishi na
Fonolojia Mizanishi. Hali kadhalika tumewajibika kutumia mbinu husishi
zitakazowajumuisha watafitiwa na mtafiti na kufanikisha utambuzi wa maneno-mkopo
kutoka kwa Kiswahili yanayotumika katika uzungumzaji Dholuo. Mbinu hizo ni
uchunguzi-ushiriki na mahojiano.
Kijumla, mpangilio wa kazi hii umewasilishwa kwenye sura nne. Sura ya kwanza
inatanguliza usuli wa mada pamoja na nyenzo za kimsingi zinazodhibiti kaida za
uchanganuzi. Sura ya pili inaingilia vigezo vya Fonolojia ya Dholuo kwa maksudi ya
kuangaza kanuni zinazoongoza lugha hii, ili kumulika jinsi zinavyoweza kuathiri maneno
kutoka kwa lugha nyingine. Kitovu cha mada yetu kinashughulikiwa katika sura ya tatu
ambapo uchambuzi unazingatia utohozi kifonolojia. Hapa ndipo panapo maelezo ya
maumbo mbalimbali yanayotokana na utohozi pamoja na usawiri wa vielelezo vya sura
dhahiri za maneno-mkopo. Sura ya nne ni tamati inayotoa muhtasari wa kazi yote.
Description
Tasnifu hii imetolewa kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika idara ya
kiswahili na lugha za kiafrika kwenye Chuo Kikuu Cha Kenyatta