Usambamba katlka ushairi-huru
Loading...
Date
2007
Authors
Mwania, James M.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia usambamba katika ushairi hum wa
. Kiswahili. Lengo la utafiti huu ni kudhihirisha namna mshairi wa kisasa
anavyotumia uhuru wake wa utunzi katika kujadili maswala mbalimbali
yanayoikumba jamii. Utafiti huu umetumia usambamba katika
kuzihakiki diwani za Kichomi, Mchezo wa Karata na Chembe cha
Mayo.
Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni nadharia ya semiotiki. Nadharia hii
huzingatia zaidi ishara na uashiriaji katika kazi za fasihi. Hivyo
\
humsaidia mhakiki kuchunguza ujumbe unaowasilishwa na msann
katika kazi zake.
Kazi hii imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza
imeshughulikia mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti pamoja na
sababu za kuchagua mada. Hali kadhalika, udurusu wa maandishi
yanayohusu mada ya utafiti pamoja na msingi wa nadharia iliyoongoza
utafiti huu ni baadhi ya mambo ambayo yameshughulikiwa. Pia
imeshughulikia mbinu za utafiti, sampuli, ukusanyaji pamoja na
uchanganuzi na uwasilishaji wa data.
Sura ya pili imeshughulikia historia fupi ya ushairi pamoj a na dhana ya
ushairi, ushairi hum na historia fupi ya ushairi hum. Kadhalika,
mazingira ya msanii, enzi ya ukoloni katika Afrika Mashariki na
kuchipuka kwa usambamba nchini Tanzania na Kenya ni baadhi ya
yaliyojadiliwa. Pia imeshughulikia maisha ya wasanii tuliochunguza
kazi zao Kezilahabi, Mberia na Mazrui.
Description
Idara ya kiswahili na lugha za Kiafrika chuo kikuu cha kenyatta
tasnifu hii imetolewa ill kutosheleza baadhi ya mahitaji ya
siiahada ya uzamili katlka chuo kikuucha kenyatta , June2007