Uwiano wa picha na matini katika mabango ya matangazo ya ukimwi: mtazamo wa Kisemiotiki
Loading...
Date
2006
Authors
Kimani, Hellen Wanjlku
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Lengo la kazi hii ni kuchanganua uwiano wa maana za picha na matini katika
mabango ya matangazo ya UKIMWI kwa kuzingatia tathmini za wapokezi.
Watafitiwa ambao walishirikishwa katika utafiti huu waliteuliwa kutoka maeneo ya
Githurai na Kiandutu katika wilaya ya Thika, Vitengo vya watu wenye umri, kazi,
elimu, tajriba, falsafa na mielekeo tofauti vilihusika. Kwa kurejelea misimbo ya
nadharia ya Semiotiki kwa mujibu wa Barthes uchanganuzi wa ishara zote za
kisanaa na kiisimu katika mabango thelathini na matano yanayohusu ugonjwa
hatari wa UKIMWI yamechanganuliwa.
Kazi hii imegawanyika katika sehemu tano. Sura ya kwanza imetanguliza kazi yote
kwa kuangazia mada ya utafiti, maswali, malengo, upeo na mipaka ya utafiti.
Mengine yaliyoshughulikiwa katika sura hii ni misingi ya nadharia, tahakiki za
maandishi yanayohusiana na mada hii, ukusanyaji na uwasilishaji wa data. Sura ya
pili imeshughulikia viunzi vya matangazo kwa nia ya kupata maana msingi katika
mabango ya UKIMWI, kwa kutalii yale yanayojidhihirisha wazi pasi kuhusisha
tajriba, mielekeo na falsafa za mtu binafsi na za kijamii. Sura ya tatu, imeangazia
ujumbe katika mabango ya matangazo ya UKIMWI pamoja na kuhakiki dhamira za
miguso tofauti. Uhakiki huo uliegemea upande wa yaliyomo kwenye tangazo kama
vile: mada, maudhui, wahusika, pamoja na msuko wa picha na matini kwa kurejelea
maoni ya watafitiwa.
Kwenye sura ya nne, vigezo vya uwiano wa maana na ujumbe katika picha na matini
vimeshughulikiwa. Tumechunguza namna picha na matini zinavyohimiliana,
kutegemeana na kuathiriana katika kumwelekeza mpokezi kufasiri maana na
ujumbe. Tumeangazia pia mchango wa usanii wa picha na matumizi ya lugha
kwenye matini katika kufanikisha uwiano wa maana na ujumbe unaofikia hadhira.
Sura ya tano imetoa muhtasari wa kazi yote. Aidha, sura hii imeshughulikia
matokeo, mahitimisho pamoja na mapendekezo ya utafiti wa baadaye kwa azima ya
upanuzi wa mawasiliano ya ishara za kisanaa katika hatua za kuboresha uwasilishaji
wa maana na ujumbe, ili yaende sambamba na yale ya ishara za kiisimu.
Description
lliyotolewa kwa madhumuni ya kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Kenyatta, 2006