Usawiri wa wahusika ka tika dafina ya Umalenga (H.M Mbega) na jiero la ndani (S.A Mohamed)
Loading...
Date
2008
Authors
M' garuthi, Timothy Kinoti
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia swala la usawm wa wahusika katika mashairi ya
Kiswahili. Mtafiti ameyahakiki mashairi teule ya washairi .wawili kwa lengo la
kutathmini jinsi washairi hawa walivyowateua wahusika wao, aina za wahusika na
jinsi wahusika hawa walivyotumiwa kutolea hisia za w,ashairi. Diwani
zilizochaguliwa ni mbili; moja ya Hassan Mwalimu Mbega Dafina ya Umalenga
(1984) na nyingine ya Said Ahmed Mohamed Jicho la Ndani (2002).
Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ile ya Ulimbwende ambayo hujaribu kueleza
umuhimu wa wahusika katika ushairi, hasa katika kutolea hisia za mshairi badala
ya kujifunga na arudhi. Nadharia hii pia hueleza umuhimu wa kuzin tia
mazingira ya aina mbalimbali katika utunzi wa mashairi.
Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti ambapo mtafiti
ameifafanua mada ya utafiti, sababu za kuchagua mada na upeo wa utafiti. Sura hii
pia inao ufafanuzi juu ya udurusu wa maandishi yanayohusu mada hii pamoja na
nadharia iliyoongoza utafiti. Hatimaye pana maelezo juu ya mbinu za utafiti
zilizotumika.
Katika sura ya pili pamejadiliwa vigezo vinavyozingatiwa na washairi katika
uteuzi wa wahusika wao. Mtafiti ameshughulikia aina mbalimbali za mazingira
ambayo huchangia katika uteuzi wa wahusika.
Sura ya tatu imejadili aina za wahusika wanaopatikana katika mashairi teule na
jinsi washairi walivyowaunga kwa ubunifu wa hali ya juu kwa lengo la
kuuwasilisha ujumbe wao kikamilifu.
Vlll
Mtafiti ameangaha jinsi wahusika hawa wanavyohusiana na kuathiriana na hivyo
kusaidia katika ujenzi wa maudhui.
Katika sura ya nne mtafiti amejadili jinsi washairi walivyowatumia wahusika
kudhihirishahisia mbalimbali.
Sura ya tano ni hitimisho linalotoa muhtasari na matokeo ya utafiti, pamoja na
mapendekezoya mtafiti.
Mwishonimwa tasnifu kuna marejeleo ya utafiti huu.
Description
Iliyotolewa kwa madhumuni ya kutosheleza baadhi ya
Mahitaji ya shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha
Kenyatta