Mabadiliko ya maudhuikiwakati katika nyimbo za harusi za jamii ya waembu
Loading...
Date
2009
Authors
Mbogo, Njeru S.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Malengo ya utafiti huu yalikuwa kuonyesha j insi maudhui katika nyimbo
za harusi miongoni mwa watu wajamii ya Waembu yalivyobadilika
kiwakati tangu kabla na baada ya maingilio ya Wakoloni. Aidha, utafiti
huu umechunguza na kueleza matukio ya kijamii yaliyochangia
mabadiliko haya. Bali na hayo, utafiti huu umelenga kueleza mabadiliko
haya ya maudhui kinadharia.
Kwa kuzingatia nadharia ya uhalisia iliyoasisiwa kwa pamoja na Gustav
Flaubert (1850), Rene Wellek na wengine kati ya kame ya 19 na 20,
ilibainika kwamba maudhui katika nyimbo kama utanzu wa fasihi
simulizi hubadilika kusadifu matukio ya kihistoria ya kipindi fulani
katika jamii.
Kipindi cha kabla ya maingilio ya wakoloni katikajamii ya Waembu
kilikuwa na nyimbo anuwai za harusi zilizobeba maudhui mahususi.
Baada ya maingilio ya wakoloni, maudhui katika nyimbo hizi yalibadilika
kwa kiasi kikubwa ingawa kuna machache yaliyoendelea.
Kwa sababu ya mabadiliko hayo, kumezuka mitazamo miwili ya
kuangalia maudhui katika nyimbo za harusi za j amii ya Waembu ambayo
ni maudhui ya nyimbo za kabla ya maingilio ya wakoloni na ya zile za
baada ya maingilio hayo. Utafiti huu umeonyesha jinsi maudhui katika
nyimbo za harusi zajamii ya Waembu yalivyobadilika kutoka kipindi
kimoja hadi kingine.
Description
Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Kenyatta, 2008