Usawiri wa wahusika makahaba katika riwaya za Said Ahmed Mohammed

Loading...
Thumbnail Image
Date
1990
Authors
Muindi, Augustine
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti wetu unahusu suala la ukahaba katika riwaya nne za Said Ahmed Mohamed. Tunahakiki usawiri wa wahusika makahaba kwa madhumuni ya kubainisha sababu za kuwepo kwa ukahaba katika jamii. Aidha, tunatilii namna ambavyo mwandishi anawabadilisha wahusika wake kutoka kwa maisha ya ukahaba na kama mabadiliko hayo yanatoasuluhisho halisi kwa jamii ya makahaba. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa ndipo tunapojadili tasnifu kwa jumla, mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti wetu, upeo wa utafiti wetu. Vile vile, tunajadili baadhi ya kazi nyingine zilizowahi kuandikwa na ambazo kwa namna fulani, zinahusiana na utafiti wetu. Aidha, tutasema machache kuhusu nadharia tunayotumia katika utafiti wetu. Kisha tutatazama sababu za kuchagua mada hii na njia tutakazofuata katika kutafiti juu ya mada yetu. Katika sura ya pili na ambayo ndiyo nguzo ya tafiti, tunaelezea dhana na nadharia za ukahaba. Dhana na nadharia hizi zinatusaidia katika kubainisha vigezo mbalimbali vinavyotambulisha kahaba katika jamii. Tunafikia upeo wa utafiti wetu katika sura ya tatu na nne. Katika sura ya tatu, tunanuia kubainisha sababu mbalimbali ambazo zimewavuta baadhi ya wahusika katika maisha ya ukahaba. Sura ya nne, tunajadili namna ambavyo mwandishi anawaondoa wahusika wake kutoka kwa maisha hayo. Sura ya tano ni ya hitimisho. Tunatoa muhtasari wa kazi tuliyoifanya. Kisha, tunatathmini kama tumefikia malengo ya utafiti wetu. Mwisho-kabisa, tunatoa marejeleo ya utafiti wetu.
Description
Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya 'Masters of Arts' katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Keywords
Citation