Athari ya mbinu rejeshi katika hadithi fupi za Kiswahili
Loading...
Date
2015-11
Authors
Musili, Lucia Muli
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulishughulikia athari ya mbinu rejeshi katika hadithi fupi za Kiswahili. Diwani zilizoshughulikiwa ni za miaka ya elfu mbili nazo ni Mwendawazimu na Hadithi Nyingine (2000) na Kunani Merikani na Hadithi Nyingine (2011). Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya eilmumtindo. Nadharia hii ilimfaa mtafiti katika utafiti huu maana diwani hizi ambazo zimeteuliwa zimesheheni matumizi ya mtindo wa mbinu rejeshi. Utafiti huu umegawanywa katika sura nne. Sura ya kwanza ilitupa mwelekeo wa utafiti wetu. Katika sura hii tumejadili swala la utafiti, malengo ya utafiti na sababu za kuchangua mada. Pia katika sura hii tumejadili misingi ya nadharia, upeo wa mipaka na yalioandikwa kuhusu mada. Mwisho mbinu za utafiti, uteuzi wa sampuli, ukusanyaji wa data uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa data zimeangaziwa, Sura ya pili nayo imejadili matumizi ya mbinu rejeshi katika diwani ya Mwendawazimu na hadithi Nyingine. Katika sura hii mtafiti amebainisha matumizi ya mbinu rejeshi katika diwani hii na athari ya mtindo huu. Sura ya tatu imezingatia matumizi ya mbinu rejeshi na athari yake katika diwani ya Kunani Merikani na Hadithi Nyingine. Sura ya nne ambayo ni hitimisho imekuwa muhtasari, matatizo na mapendekezo ya mtafiti. Utafiti huu unanuia kuwafaidi wahakiki wengine, wasomi na waandishi wa kazi za fasihi. Pia utafiti huu utawasaidia wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vikuu katika kuhakiki kazi zao.
Description
Tasnifu hii imetolewa ill kutosheleza baadhi ya maritaji ya shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Kenyatta.