Athari ya Utenzi Katika Uandishi wa Riwaya Teule ya Kiswahili.

Loading...
Thumbnail Image
Date
2017-06
Authors
Nabangi, Judith Khasoa
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu umejikita katika kuonyesha athari ya utenzi katika uandishi wa riwaya teule ya Kiswahili. Matumizi ya utenzi katika uandishi wa riwaya ni mojawapo ya mbinu za kimtindo za uandishi. Kwa hivyo, utafiti huu umefanywa kwa kuongozwa na malengo matatu ambayo ni: Kudhihirisha jinsi utenzi umechangia uandishi wa riwaya kimaudhui. Pili, kuonyesha mtindo ulivyochangiwa na utenzi katika kuandika riwaya teule. Tatu, kubainisha jinsi wahusika wa riwaya teule wamechangiwa na utenzi. Utafiti ulifanywa ili kuonyesha usemezano wa utenzi na riwaya teule ya Kiswahili. Utafiti huu ulifuata muundo wa kimaelezo na ulifanyiwa maktabani. Utafiti uliongozwa na nadharia ya usemezo ya Mikhail Bakhtin, ambayo inashikilia kwamba tanzu za fasihi husemezana. Sampuli lengwa katika utafiti huu ilikuwa riwaya tatu ambazo ziliteuliwa kimaksudi; Kasri ya Mwinyi Fuad, Msimu wa Vipepeo na Walenisi. Data ilikusanywa kwa kusoma riwaya hizo tatu kwa kina na kunukuu mambo muhimu yanayohusiana na utafiti huu. Mambo haya ni maudhui, mtindo wa uandishi wa riwaya na wahusika wa riwaya teule. Data hiyo ilichanganuliwa kwa kuzingatia maswali ya utafiti. Utenzi unawiana vipi na uandishi wa riwaya kimaudhui? Pili, utenzi unawiana vipi na riwaya teule kimtindo? Tatu, je, kuna uwiano upi baina ya wahusika wa utenzi na wale wa riwaya teule? Aidha, data ilichanganuliwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti, pia, iliongozwa na mihimili ya nadharia ya usemezo. Matokeo ya utafiti huu yamewasilishwa kwa njia ya maelezo na utoaji wa mifano mwafaka. Utafiti huu uligundua kwamba athari za utenzi katika uandishi wa riwaya ni mojawapo ya mbinu za kimtindo za uandishi. Kwa hivyo, kipengele cha utanzu mmoja kinaweza kutumiwa kama mbinu ya kimtindo katika uandishi wa utanzu mwingine.
Description
Tasnifu Iliyowasilishwa Katika Idara ya Kiswahili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili ya Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords
Citation