Athari ya mazingira ya kihistoria na kijamii katika uwasilishaji wa maudhui ya dhifa (E. Kezilahabi)
Loading...
Date
2016
Authors
Nasimiyu, Christine M.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulichunguza athari ya mazingira ya kihistoria na kijamii katika uwasilishaji
wa maudhui ya diwani ya Dhifa ya E. Kezilahabi (2008). Malengo yalikuwa, kubainisha
maudhui yaliyowasilishwa na mtunzi wa Dhifa, kubainisha narnna maudhui haya
yalivyowasilishwa na kueleza narnna maudhui haya yalivyoibua mazingira ya kijamii na
kihistoria. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Uhistoria Mpya ambayo huangalia
umuhimu wa muktadha katika utunzi na uhakiki wa kazi za kifasihi. Pia, huonyesha ya
kwamba kadiri jamii zinavyoendelea, utamaduni hubadilika kiwakati na jambo hili
huathiri utunzi, uwasilishaji na uhakiki wa kazi za kifasihi. Utafiti huu ulizingatia
muundo wa kimaelezo kuhusu suala la utafiti, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu
mada na mbinu za utafiti. Utafiti huu ulifanywa maktabani. Sampuli iliteuliwa
kimakusudi ambapo mashairi ishirini na moja yaliteuliwa ili saba yashughulikie
kipengele cha siasa, uchumi na masuala ya kijamii. Data ilikusanywa kutokana na
usomaji wa kina wa mashairi teule. Uchanganuzi wa data ulizingatia uainishaji wa aina
ya maudhui, uwasilishaji wake pamoja na matukio ya kihistoria. Aidha, ulizingatia
chimbuko la maudhui, namna yalivyowasilishwa, dhamira na falsafa ya mtunzi. Hayo
yote yalifanywa kwa kuzingatia pengo lililonuiwa kujazwa na utafiti huu kwa kuongozwa
na nadharia ya utafiti. Utafiti ulibaini na kutambua kwamba, siasa ya Tanzania, baada ya
Azimio la Arusha ilichukuwa rnkondo mpya. Aidha, mazingira mbalimbali ya kijamii,
kisiasa na kiuchumi yalichangia pakubwa katika kuwasilisha maudhui ya diwani ya
Dhifa. Inatarajiwa kuwa utafiti huu utawafaa wanafunzi wa shule za upili, vyuo, watafiti
wa ushairi na wakuza mitalaa. Tasnifu hii iligawanywa katika sura sita. Sura ya kwanza
ilishughulikia mada ya utafiti, maswali ya utafiti, malengo ya utafiti, upeo na mipaka,
yaliyoandikwa kuhusu mad a, sababu za kuchagua mada na misingi ya nadharia. Sura ya
pili ilichunguza historia na falsafa ya mtunzi. Sura ya tatu iliangazia maudhui ya kisiasa.
Sura ya nne ilichambua maudhui ya kiuchumi. Sura ya tano iliangalia maudhui ya
kijamii. Sura ya sita ilijumuisha muhtasari, hitimisho,matokeo ya utafiti na mapendekezo.
Description
Tasnifu hii imew asilishw a kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya Uzamili ya Chuo Kikuu Cha Kenyatta, 2016