RP-Department of Kiswahili and African Languages

Permanent URI for this collection

Browse

Recent Submissions

Now showing 1 - 20 of 97
  • Item
    Athari Ya Viarudhi Vya Ekegusii Kwa Kiimbo Cha Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Upili
    (East African Journal of Swahili Studies, 2023-11-10) Nyougo, Christine; Githinji, Peter
    Makala hii inadhamiria kuonyesha athari ya viarudhi vya Ekegusii kwa matumizi ya kiimbo cha Kiswahili sanifu. Wasailiwa wetu ni wanafunzi wa shule tatu za upili zinazopatikana katika eneo la Kisii. Tulijikita katika nadharia ya Mennen (2015) ya ujifunzaji wa kiimbo katika lugha ya pili. Nadharia hii huchunguza matatizo ambayo wajifunzaji wa lugha ya kwanza hupata wakati wa kujifunza kiimbo cha lugha ya pili. Tumejikita kwa mantiki kuwa mtagusano baina ya lugha moja na nyingine huweza kuibua kufanana au kutofautiana kimatumizi katika uenezaji wa viimbo tofauti. Tumetumia mihimili minne katika uchanganuzi wa data tuliyopata nyanjani. Mhimili wa kimfumo unashughulikia vipengele vya kiarudhi katika lugha husika na usambazaji wake, mhimili wa utekelezaji unashughulikia utaratibu wa namna ambavyo vipengele mbalimbali vya kifonolojia vinavyotekeleza majukumu yavyo katika lugha husika. Mhimili wa ujirudiaji unaangazia kiwango cha matumizi ya vipengele hivi vya fonolojia ambapo lugha hutofautiana katika kiwango cha matumizi ya vipengele vyake na mhimili wa kisemantiki unaoshughuklika maana inayopatikana kutokana na matumizi ya viarudhi husiaka. Usampulishaji wa kimaksudi ulitumiwa katika kuteua wanafunzi wa vidato tofauti katika shule tatu teule na walimu wanaofunza Kiswahili katika shule hizo. Data yetu ilitokana na hojaji, mahojiano usomaji wa sentensi pamoja na kifungu ambacho kilikuwa na aina nne za viimbo ambapo wasailiwa walizisoma kwa sauti. Data ya ziada ilitokana na usomaji wa sentensi nane za Ekegusii zenye kiimbo cha taarifa, swali, amri na mshangao ambazo zilisomwa na walimu wanaozungumza Ekegusii kama lugha ya kwanza katika shule hizo tatu. Uchanganuzi wa data ulifanywa kupitia ufasili wa data ya hojaji, mahojiano na uchunzaji wa kushiriki. Matokeo tuliyopata yalibainisha kuwa uhawilisho wa viarudhi hivi kwa kiwango kikubwa huathiri matumizi sahihi ya kiimbo cha Kiswahili ambapo wasailiwa wa lugha ya kwanza hurudufu baadhi ya vipengele vya lugha hiyo katika kiimbo cha lugha ya pili. Matokeo haya pia yalidhihirisha kuwa maumbo ya silabi katika Ekegusii, shadda, toni na wakaa huathiri matumizi ya kiimbo cha Kiswahili sanifu.
  • Item
    Jinsi Leksimu za Mitishamba Zinavyoakisi Uhifadhi wa Mazingira ya Waswahili Nchini Kenya
    (East African Journal of Swahili Studies, 2023) Karoli, Nelly Bonareri; Mwita, Leonard Chacha
    Lugha na utamaduni wa watu ni vitu visivyoweza kutenganishwa. Mifumo ya lugha huathiri namna binadamu anavyofikiri kuhusu ulimwengu wake na husababisha matendo ambayo ni kiini cha changamoto za kiikolojia wanazokabiliana nazo. Katika makala hii, tulichambua namna leksimu za mitishamba zinachukuliwa kama ishara za uhifadhi wa mazingira katika mifumo ya ikolojia katika jamii ya Waswahili. Data ilikusanywa kwa mbinu ya mahojiano kutoka kwa Waswahili wa Mvita. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya semiotiki ikolojia iliyotusaidia kuelewa kuwa kile kilichotambuliwa kama athari kwa ikolojia mara nyingi huwa na sababu za kisemiotiki na tofauti katika kufasiri ishara au misamiati. Tulibainisha kuwa kuna leksimu za mitishamba kama ‘mpambamwitu’ ambayo Waswahili walitumia kuonyesha ile hali ya kurembesha misitu yao kwa kuleta taswira ya kiasili na mwonekano mzuri wa kipekee, ‘linda ziwa’ iliakisi uhifadhi wa vyanzo vya maji. Mahali ambapo ulimea, maji yalikuwa safi na tayari kutumika katika shughuli za pale nyumbani. Mti huu ulifananishwa na jokofu kwani hata nyakati za joto ulipoenda mtoni ungepata maji hayo ni baridi na safi. Waswahili ambao walikuwa ni watumiaji wa leksimu hizi walionyesha kuwa ilipofikia suala la uhifadhi wa mazingira, wanajamii walijitahidi kutunza mazingira yao. Jinsi tunavyochagua misamiati yetu katika mawasiliano kuhusu mazingira kunaweza kubadilisha jinsi wanajamii wanavyoyaona mazingira hayo. Ikolojia inategemea mawazo yaliyopo, kanuni, na sheria za jamii. Makala hii imapendekeza kuwa kwa kubadilisha jinsi tulivyoyatazama mazingira yetu ya asili tunaweza kutambua thamani yake halisi. Kwa kuiweka thamani hiyo katika sera zetu mipango na mifumo ya uchumi, tunaweza kuelekeza uwekezaji katika shughuli ambazo zinarejesha uasili wa mazingira yetu na tukapata faida. Kwa kutambua kuwa mazingira yetu ni mshirika wetu mkubwa basi tutayafanya kuwa endelevu.
  • Item
    Polisemi ambazo Zimeundwa Kutokana na Sitiari na Metonimu katika Kiswahili
    (EANSO, 2024-02) Masika, Mark Elphas; Mwita, Leonard Chacha
    Makala haya imechunguza polisemi ambazo zimeundwa kutokana na sitiari na metonimu katika Kiswahili. Kimsingi, polisemi ni leksimu moja yenye maana nyingi ambazo zinahusiana kwa njia moja au nyingine. Pia polisemi huundwa kwa njia zingine kwa mfano, ukopaji, mabadiliko katika matumizi ya neno, na ufasiri mpya wa homonimu. Nadharia ya semantiki tambuzi ilitumiwa katika uchambuzi wa data ya utafiti huu. Nadharia hii ni sehemu ya nadharia ya Isimu Tambuzi ambayo ina misingi yake katika saikolojia tambuzi . Data ya makala haya ilikusanywa maktabani. Maneno ambayo ni polisemi na yameundwa kwa sitiari na metonimu kwenye Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2018) yalikusanywa. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika katika uteuzi wa sampuli. Kutokana na data ya utafiti huu, imebainika kuwa kuna baadhi ya polisemi zilizojitokeza ndani ya homonimu. Kwa mfano, tata1 na chuo1. Pia, utafiti huu umebaini kuwa polisemi nyingi huundwa kisitiari ikilinganishwa na metonimu. Makala haya inapendekeza kwamba tafiti zingine zaidi zinaweza kufanywa kuhusu namna mbinu zingine za lugha kama vile chuku, methali, nahau na tashibihi zinaweza kuchangia katika Isimu.
  • Item
    Makosa ya Kiisimu Yanayofanywa na Wanafunzi Wanaozungumza Lahaja ya Kigichugu Wanapojifunza Kiswahili Kama Lugha ya Pili
    (East African Journal of Swahili Studies, 2024) Njagi, Nancy Wanja; Kihara, David
    Binadamu wanahitaji lugha ili kuwasiliana na mojawapo ya lugha maarufu ulimwenguni ni Kiswahili. Kiswahili kimetafitiwa na wataalamu wengi ili kutafuta suluhisho la baadhi ya changamoto zinazokumba lugha hii na kuiboresha. Mojawapo ya changamoto na suala ambalo halijatafitiwa na utafiti huu ulikusudia kubaini ni makosa ya kiisimu ya wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya pili : Uchunguzi kuhusiana na lahaja ya Kigichugu.Utafiti huu ulitumikiza kanuni na mihimili ya nadharia ya Sintaksia Finyizi ili kuweka wazi makosa ya kisintaksia na kisemantiki yanayofanywa na wanagenzi wa Kigichugu wanapojifunza Kiswahili kama L2. Uchunguzi huu uliendelezwa nyanjani na maktabani.Nyanjani ulitekelezwa katika shule za sekondari za kutwa katika kaunti ndogo ya Gichugu kwa sababu ndiko kuna wazungumzaji asilia wa Kigichugu. Katika utafiti huu tulipaswa kuteua shule,na wanafunzi wa kufanyia utafiti. Katika uchaguzi wa shule za kutwa za kufanyia utafiti tulitumia mbinu ya sampuli kimaksudi. Katika uteuzi wa wanafunzi tulitumia usampulishaji wa kinasibu pale ambapo tulipatia wanafunzi nambari kinasibu na kuteua waliopata nambari moja hadi sita. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia hojaji , insha na masimulizi . Data ya utafiti iliwasilishwa kupitia majedwali na maelezo. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha makosa mengi ya kisintaksia na kisemantiki yaliyotokana na lahaja ya Kigichugu. Makosa haya ni kama vile: makosa ya wanafunzi wagichugu katika matumizi ya nomino, vitenzi, vipatanishi, vivumishi, vibainishi, vielezi, vihusishi na vishamirishi. Makosa haya yalipelekea si tu kuibuka kwa muundo wa sentensi usiokubalika(sintaksia) bali hata kuwepo kwa maana, tofauti na iliyokusudiwa na wanafunzi hawa au isiyoeleweka, hivyo basi kuwepo kwa makosa ya kisemantiki (semantiki leksika na semantiki mantiki). Makosa haya yalichanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Sintaksia Finyizi na kudhihirisha ukiukaji wa kanuni za nadharia hii.
  • Item
    Ukiukaji wa Kanuni Bia za Greenberg katika Miundo ya Tungo Zenye Vihusishi Katika Lugha ya Kiswahili
    (EANSO, 2023-11) Ongwae, Jemimah Kwamboka; Githinji, Peter
    Makala haya yalidhamiria kubaini ukiukaji wa baadhi ya kanuni bia za Greenberg katika miundo ya tungo zenye vihusishi vya Kiswahili. Katika utafiti wake, Greenberg (1963), alipendekeza kanuni bia 45 na kutafiti lugha 30 ili kuchunguza mpangilio wa vipashio vya kiisimu katika makundi mbalimbali ya lugha. Lugha ya Kiswahili ilikuwepo mojawapo ya sampuli alizoteua. Hata hivyo, katika kuzingatia uwekaji vihusishi, inaonekana kukiuka baadhi ya kanuni hizo. Kwa hivyo, mkabala wa Greenberg (1963) ulitumika. Kanuni bia za Greenberg hasa zile zinazozungumzia vihusishi pekee zilitumika kuchanganua miundo na mazingira ya kiisimu yanayosababisha ukiukaji wa baadhi ya kanuni za Greenberg katika uwekaji wa vihusishi vya Kiswahili. Data iliyotumika ilikuwa ni tungo zenye vihusishi. Mbinu ya usampulishaji wa kimakusudi ilitumika kuteua vihusishi hivi na vilikusanywa kwa kusoma vitabu vya sarufi na makala kutoka kwenye majarida na makala ya mtandaoni. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa kuzingatia mkabala wa kanuni bia za Greenberg kupitia ufafanuzi wa data kwa njia ya maelezo na unukuzi wa kanuni bia za Greenberg. Ilijidhihirisha kuwa baadhi ya kanuni bia za Greenberg zina ukiushi katika lugha ya Kiswahili. Ukiushi hasa ulitokea kwa sababu sifa A haikumiliki sifa B kwa kuzingatia sheria ya uchanganuzi iliyopeanwa. Haya yalibainika hasa kwa kuwa lugha ya Kiswahili inamiliki aina mbili za vihusishi; vihusishi vya kabla ya nomino na vihusishi vya baada ya nomino katika umbo lake la nje. Hata hivyo, baadhi ya kanuni bia zingine zilionyesha utiifu. Aidha baadhi ya kanuni hizi zina utata ambao unaleta changamoto katika juhudi za kutoa kauli jumlishi. Makala haya yatachangia katika kongoo ya utaratibu wa vipashio katika sentensi, taipolojia ya lugha na sintaksia ya Kiswahili.
  • Item
    Tathmini ya Uamilifu wa Kiswahili Nchini Uganda: Mintarafu, Ueneaji wa Matumizi Yake Kwenye Asasi ya Uchapishaji
    (ENSO, 2022) Rais, Abdu Salim; Onyango, Jacktone; Mbaabu, George Ireri
    Kwa muda mrefu, Kiswahili kilifundishwa nchini Uganda kama taaluma ya Kigeni, licha ya kuwa lugha rasmi ya pili, baada ya Kiingereza (GoU, 1995). Hata hivyo, Kiswahili kina dhima kubwa katika asasi za muziki, ulinzi na elimu ambako Uamilifu wake unadhihirishwa na ueneaji wa matumizi yake (Mbaabu, 1991na Mlacha, 1995). Ingawa Kiswahili kilienea nchini Uganda, kabla ya kufikia mwishoni mwa wakati wa kukamilisha utafiti huu, viwango vya Uamilifu wake vilikuwa havijatathminiwa kitaaluma kupitia asasi ya uchapishaji. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa, kutathmini Uamilifu wa Kiswahili kutokana na ueneaji wa matumizi yake kupitia asasi ya Uchapishaji. Uamilifu wa Kiswahili ulichunguzwa kwa kutumia Nadharia ya Uamilifu iliyoasisiwa na Wanasosholojia Auguste Comte (1787-1857), Herbert Spencer (1830-1903), Vilfredo (1848-1917) na Emile Durkheim (1857-1917) na kuendelezwa na Mesthrie na wenzake (2004). Nadharia ya Uamilifu iliangazia jukumu lililotekelezwa na fani katika jamii mahsusi(Mesthrie et al., 2004).Kiini cha Uamilifu ni uwezekano wa kuweko kwa fani yenye vijisehemu mahsusi ambapo kila kijisehemu huchangia maendeleo kwa kutekeleza jukumu mahsusi katika fani hiyo (Mesthrie et al., 2004). Nadharia hiyo ilisaidia kutathmini dhima ya ueneaji wa matumizi ya Kiswahili kupitia Asasi ya Uchapishaji nchini Uganda. Istilahi Ueneaji hutokana na kitenzi enea chenye maana ya kuwa kila mahali. Kuenea katika muktadha huo, kulimaanisha kusambaa kwa matumizi ya Kiswahili nchini Uganda kwa kupitia asasi ya uchapishaji. Ueneaji ni hali ambapo fani fulani husambaa ijapokuwa muundo huweza kubadilika kulingana na mazingira. Wataalamu wa Ueneaji walishikilia kwamba, fani huweza kupenya kuta za kikabila na kuzagaa zaidi kutoka jamii zilizoendelea, kuelekea zisizoendelea (Buliba et al., 2014). Ithibati ni kwamba, fani za lugha za Watawala Wakoloni zinapatikana
  • Item
    Mwathiriano Kati ya Watunzi wa Riwaya ya Kiswahili: Mwangwi wa Maudhui ya Mafuta (2008) katika Cheche za Moto (2008)
    (EAJSS, 2023-10-18) Kalingwa, Felix Musyoka; Kaui, Titus Musyoka
    Makala hii inashughulikia athari za Katama Mkangi kwa John Habwe kwa kujikita katika riwaya teule za Kiswahili za Mafuta (1984) na Cheche za Moto (2008). Utanzu wa riwaya ya Kiswahili umeendelea kupanuka kimaudhui na kifani kutokana na juhudi za watunzi mbalimbali kama vile Katama Mkangi na John Habwe. Japo tafiti za awali zimetafitia suala la mwingiliano matini, tafiti nyingi zimejikita katika kazi za mtunzi mmoja. Utafiti wa kina ulihitajika kuchunguza namna utunzi wa Mafuta (1984) ulivyoathiri John Habwe alipoitunga riwaya yake ya Cheche za Moto (2008). Katama Mkangi aliandika riwaya ya Mafuta katika wakati wa chama kimoja cha kisiasa ambapo uhuru wa kujieleza ulikuwa umebanwa sana. Habwe ameandika kazi yake katika mazingira yaleyale lakini katika kipindi ambapo uhuru wa kujieleza umepanuliwa. Kwa hivyo, amekwepa mtindo wa kimajazi alioutumia Mkangi na kuyaangazia masuala anayoyaibua kwa njia wazi. Makala hii ililenga kuonyesha kuwa maudhui katika riwaya ya Cheche za Moto ni mwangwi unaotokana na riwaya ya Mafuta (1984). Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya mwingiliano matini iliyoasisiwana Julia Kristeva (1969). Mihimili mikuu ya nadharia hii iliyoongoza utafiti huu ni pamoja na: hakuna matini ya fasihi yenye sifa za pekee, matini hubainisha sifa mbalimbali za matini tangulizi, na mwisho, matini ya baadaye huweza kufafanua dhana fulani kutoka matini tangulizi kwa njia inayoeleweka. Nadharia hii ya mwingiliano matini ilisaidia pakubwa kuonyesha namna kazi ya awali, Mafuta (1984) ilivyomwathiri John Habwe katika utunzi wa Cheche za Moto (2008) kimaudhui. Riwaya teule ziliteuliwa kimakusudiili kupata sampuli faafu yenye data ya kujaza pengo la utafiti. Data ilikusanywa kupitia kwa usomaji wa maktabani na vilevile kusakura mitandaoni kuhusu vipengele vya mwingiliano matini katika riwaya ya Kiswahili. Data hii imewasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Utafiti wa makala hii unatarajiwa kutoa mchango katika uhakiki wa utanzu wa riwaya ya Kiswahili, hususan kuhusu kipengele cha kuathiriana baina ya watunzi wa riwaya za Kiswahili
  • Item
    Translated Kiswahili Texts A Case Study of Kithaka wa Mberia’s Texts
    (2018) Jessee, Joseph Murithi; King’ei, Geoffrey Kitula
    Translation is a complex exercise that involves not only transfer of meaning of linguistic aspects of translated texts but more importantly their literary aspects. This means that for a translator come up with the translated text that meets the knowledge, expectations and values of the target audience they must consider their historical and geographical contexts. This paper examined the plays written by Kithaka wa Mberia in Kiswahili and translated in English with a view by the writer to reach a wider audience. We have assessed the themes presented, linguistic and stylistic devices employed and the characters presented to see whether the knowledge, expectations and values of the target audience are met. Given that these texts are originally written in Kiswahili, it was important to see how the translator conveys the message to the wider audience targeted by the choice of use of English language. In our analysis we employed the Skopos theory of translation which focuses on translation as a purposive activity intended for a particular audience. The conclusion is that the translated texts have not to a great extent conveyed the intended message to the audience targeted as the translators focused mainly on the linguistic equivalents and to a large extent failed to meet the knowledge, expectations and values of the wider audience targeted.
  • Item
    Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leola Kenya.
    (Editon Consortium, 2021-11) Mutuku, Fidelis Kioko; Onyango, Jacktone o.; Mwita, Leonard Chacha
    Makala hii inaonyesha tofauti iliyopo kati ya majukumu na maumbo ya uhusika katika vichwa vya habari vya siasa kwenye gazeti la Taifa Leo. Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charles Fillmore mnamo mwaka wa 1968 imeongoza uchunguzi huu. Utafiti huu umefanywa baada ya kubaini kuwa wasomi mbalimbali wa gazeti hutafsili maana anuwai kwenye kichwa kimoja cha habari za siasa. Jambo hili husababisha utata wa kimaana na uenezaji wa jumbe zisizoithibatika katika jamii, hivyo basi, kuzalisha migogoro ya kisiasa nchini. Upekuzi wa yaliyomo kwenye matoleo ya gazeti la Taifa Leo ambayo yametawaliwa na vichwa vya habari za siasa na kuchapishwa kati ya mwaka 2017-2019 ni msingi wa data ya utafiti huu. Vichwa kumi na vinane vya habari za siasa vilisampulishwa kimakusudi na kutumika katika uchambuzi wa uchunguzi huu. Data katika makala hii imewasilishwa kupitia mfumo wa majedwali na maelezo. Matokeo ya tathmini ya uchunguzi huu yameshikilia kwamba Kiswahili hakina maumbo dhahiri ya uhusika ispokuwa katika nomino ambazo nafasi yake yaweza kuchukuliwa na viwakilishi vya nafsi ya pili na tatu umoja na wingi. Katika vichwa vya habari ambavyo nomino zake si za ngeli ya A-WA, viwakilishi faafu vya nomino hizo huchukua nafasi hiyo na kuwa maumbo ya uhusika. Kila aina ya uhusika ina jukumu lake la uhusika. Majukumu ya uhusika ni dhahania na hubadilika kulingana na aina ya uhusika. Uchunguzi huu utakuwa wenye umuhimu kwa wasomi wa magazeti na taifa kijumla. Wasomi wa magazeti wataongozwa na kigezo cha dhima ya maneno katika tungo kudondoa maana sawa katika vichwa lengwa vya habari za kisiasa na kupitisha tafsili hiyo moja kwa wanajamii. Kwa kufanya hivi, migogoro ya kisiasa katika jamii iletwayo na tafsili mbalimbali za kimaana itafutiliwa mbali.
  • Item
    Sera ya Lugha na Mabadiliko ya Kimaudhui ya Ushairi wa Kiswahili kati ya Miaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzania
    (2023) Njuguna, Helina Wanjiku; King’ei, Geoffrey Kitula; Wafula, Richard Makhanu
    Makala hii inachunguza jinsi sera ya lugha ya kipindi cha ukoloni ilivyochochea mabadiliko ya kimaudhui ya ushairi wa Kiswahili kati ya mwaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzania. Kulingana na makala hii hali ni matukio mahsusi yanayoathiri ubunifu wa maudhui ya ushairi. Ili kukuza mjadala wetu, makala hii imezingatia sera ya lugha ya kipindi cha utawala wa Wajerumani na Waingereza. Uchunguzi unazingatia mashairi teule kutoka diwani za watunzi wafuatao: Mathias Mnyampala, “Diwani ya Mnyampala (1965)”, Amri Abedi, “Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri (1954)”, Akilimali Snow-White, “Diwani ya Akilimali (1963)”, Shaaban Robert , “ Koja la Lugha (1969), Pambo la Lugha (1966), Kielezo cha Fasili (1968), na Masomo Yenye Adili (1967)”, na Saadani Kandoro, “Mashairi ya Saadani, (1966)”. Mashairi yaliyoteuliwa yanasomwa na kuhakikiwa ili kubainisha maudhui yaliyomo. Uchanganuzi wa data unaongozwa na mihimili ya Nadharia ya Utegemezi na Nadharia ya Ubidhaaishaji wa Lugha. Katika mashairi teule, inabainishwa namna washairi walivyotetea na kuinua hadhi ya lugha ya Kiswahili kwa kueleza sifa na umuhimu wake katika ushairi wao. Pia, inadhihirishwa jinsi ushairi uliotungwa kwa Kiswahili sanifu ulivyotumiwa kama chombo cha umma cha kujieleza kwa kupigania haki, usawa, na uhuru pamoja na kuwahimiza wananchi wakae kwa amani, udugu na heshima.
  • Item
    Uhusika katika Vichwa vya Habari za Siasa
    (EAST AFRICAN NATURE & SCIENCE ORGANIZATION, 2021) Mutuku, Fidelis Kioko; Onyango, Jacktone; Mwita, Leonard Chacha
    Uhusika ni dhana ya kisarufi ambayo hutumiwa kuonyesha dhima ya maneno katika tungo. Dhana hii ni muhimu katika uchambuzi wa tungo kwani hunuia kuwasilisha ujumbe wa kisemantiki uliogubikwa katika muundo wa ndani. Makala hii inadhihirisha dhana mbalimbali za uhusika na jinsi zinavyojitokeza katika vichwa vya habari za siasa zilizoko kwenye magazeti teule ya Taifa Leo. Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charles Fillmore mnamo mwaka wa 1968 imeongoza uchunguzi huu. Utafiti huu umefanywa baada ya kubaini kuwa wasomaji mbalimbali wa gazeti hufasiri maana anuwai kwenye kichwa kimoja cha habari za siasa. Jambo hili husababisha utata wa kimaana na uenezaji wa jumbe zisizo thabiti katika jamii, hivyo basi, kuzalisha migogoro ya kisiasa nchini. Upekuzi wa yaliyomo kwenye matoleo ya gazeti la Taifa Leo ambayo yametawaliwa na vichwa vya habari za siasa na kuchapishwa kati ya mwaka 2017-2019 ni msingi wa data ya utafiti huu. Vichwa vya habari za kisiasa kumi na nane vilisampulishwa kimakusudi na kutumika katika uchambuzi wa uchunguzi huu. Data katika makala hii imewasilishwa kupitia mfumo wa majedwali na maelezo. Matokeo ya utafiti huu yameshikilia kwamba, mahusiano kati ya kitenzi na nomino au kiwakilishi chake katika sentensi hubainisha aina ya uhusika. Uchunguzi huu una umuhimu kwa wasomi wa magazeti na taifa kijumla. Wasomaji wa magazeti wameongozwa na kigezo cha dhima ya maneno katika tungo ili kudondoa maana sahihi katika vichwa lengwa vya habari za kisiasa na kupitisha fasiri hiyo moja kwa wanajamii.
  • Item
    Fasihi ya Watoto katika Ufundishaji wa Kiswahili katika Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki
    (KAKAMA, 2019) Ngugi, Pamela
    Utafiti uliofanywa na shirika la Uwezo - Kenya kuanzia mwaka wa 2014 hadi 2016 kuhusu "Are our Children Reading?" umethibitisha kuwa watoto wengi hasa katika shule za msingi hawajui kusoma na kuandika kwa mujibu wa viwango vya madarasa waliyomo. Kwa sababu hiyo, shirika hili limependekeza mabadiliko katika ufundishaji na kupendekeza kuturnika kwa mkabala jumuishi wa elimu iwapo sekta ya elimu inatarajia kupata maendeleo thabiti. Mkabala jumuishi huhimiza wanafunzi kushiriki katika ujifunzaji wao na hivyo basi, kusaidia katika ukuzaji wa maarifa ya kufikiria kwa kiwango kikubwa. Katika kufanya hivi, ujifunzaji huwa wa maana kwa mwanafunzi na huchangia katika kujenga stadi nne za lugha ambazo ni: kusikiliza, kuongea, kusoma na kuandika, kusikiliza na kuongea kwa kiwango cha juu. Lengo la makala hii ni kujadili na kubainisha namna ambavyo fasihi ya watoto inaweza kutumika kama kichocheo cha kujua kusoma na kuandika, hasa pale ambapo wanafunzi wanapewa nafasi ya kujenga maana kutokana na usomaji wao. Fasihi ya watoto inaweza kuchangia katika kuinua maarifa, stadi na milelekeo chanya miongoni mwa wanafunzi kuhusiana na masuala ya kusoma na kuandika hali ambayo itachangia katika kufikia lengo la 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu katika sekta ya elimu kuhusiana na kuhakikisha Mitaala ya Kiswahili katika Vyuo Vikuu rya Afrika Mashariki I 212 kuwa watoto wanapata elimu bora na yenye usawa kwa wote na kutoa furs a kwa wote kujiendeleza (UN, 2015) katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Fasihi ya Watoto katika Elimu
  • Item
    Fasihi ya Watoto kama Njia ya Kukuza Mshikamano wa Kiraifa
    (Moi University Press, Moi University, Eldoret, 2019) Ngugi, Pamela M. Y.
    Lengo la nchi yoyote iliyojikomboa kutokana na ukoloni na kupata uhuru ni kugeuza asasi za kiukoloni ilizorithi ili ziweze kuhudumia mahitaji na tamaduni za jamii mpya (Ochieng, 1985 katika Mbatia, 2012). Kenya ilipopata uhuru mwaka wa 1963, na kikwazo kikuu katika ujenzi wa taifa jipya kilikuwa ni ukabila. Wakenya waliendelea kudumisha uaminifu kwa makabila yao kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni. Hivyo basi kulikuwa na haja ya kubuni njia za kukabiliana na hali hii. Ujenzi wa utarnbulisho wa kitaifa ni muhimu katika kupunguza migogoro ya kikabila na kimbari. Utambulisho huu hauji kisadfa bali hujengwa kimakusudi kama sehemu ya ajenda ya viongozi wenye mtazamo mpana na urazini wa kitaifa. Kama anavyosisitiza Njogu (2012) "Utambulisho wa kitaifa unasaidia katika kuimarisha asasi za utawala bora, kuwajibisha viongozi na kuweka uwazi katika utoaji huduma kwa umma." Tangu enzi za kabla ya uhuru hadi sasa, Kiswahili kama lingua franka kimeweza kutoa mchango muhimu katika kujenga mshikamano wa kitaifa, (Mbatia, 2012). Kwa mfano, mara tu baada ya uhuru Kiswahili kilichangia katika kujenga tabaka la wafanyikazi ambalo lilijumlisha watu kutoka makabila mbalimbali. Watu waliotoka mashambani na kuja kufanya kazi katika miji mbalimbali walilazimika kutumia Kiswahili ili kuweza kuwasiliana. Hivyo basi lugha ya Kiswahili ikawa mojawapo wa nyenzo za kujenga utaifa wa Kenya. Baada ya uhuru, serikali ya Kenya iliteua TUl11eya Ominde chini ya Uenyekiti wa Prof S.H. Ominde. Jukumu la tume hiyo lilikuwa ni kushauri serikali kuhusu utungaji na utekelezaji wa sera ya elimu baada ya kufanya uchunguzi uliohitajika. Tume hii iliibuka na malengo kadhaa ya elimu nchini Kenya.Lengo mojawapo la elimu lilikuwa na lingali ni kukuza utaifa, uzalendo na kuendeleza umoja wa taifa. Hivyo basi, elimu inayotolewa inahitaji kuziheshimu tamaduni mbalimbali zilizopo nchini na wakati uo huo, kuhakikisha kuwa haiendelezi ubaguzi katikajamii kwa misingi ya rangi, ukabila na dini. IIi kutekeleza lengo hili na malengo mengine, wasomi wengi wanaamini kuwa ufundishaji wa fasihi kwa jumla na hasa fasihi ya watoto unaweza kuchangia katika kuyafikia malengo haya kwa kukuza hisia za kitaifa miongoni mwa wanafunzi. ,- Ujenzi wa taifa ni juhudi za makusudi na za kujitolea. Tangu uhuru, wananchi wamekuwa wakitafuta njia za kuleta utangamano baina ya makabila na nchi mbalimbali za Afrika. Hatua moja kuhusu ujenzi wa taifa ni uimarishaji wa utamaduni wa tamaduni mbalimbali. Utamaduni wowote ule utaeleweka vyema kwa kuchunguza mila na desturi zilipo katika jamii husika, pamoja na kufahamu namna kila jamii ilivyowasilisha amali zake mbalimbali kama vile, ukarimu, kujitolea, haki na maslahi ya pamoja, mambo ambayo yalichangia katika kuunda utaifa. Ufahamu wa amali hizi waweza kupatikana kupitia fasihi za jarnii hizi. Fasihi ni matokeo ya shughuli za jamii; huibuka, hukua na kusambaa kutokana na mazingira yaliyopo katika jamii. Lengo la sura hii ni kubainisha dhima ya fasihi ya watoto kama kichochezi cha kujenga
  • Item
    Mikakati ya Uchambuzi wa Fasihi ya Watoto: Mtazamo wa Upokezi wa Msomaji
    (AJOL, 2016) Ngugi, Pamela M.Y.
    Fasihi ni kama ndovu, nasi kama wafasili tunaweza kugusa sehemu mbalimbali za mwili wake kujua alivyo ndovu huyu. Kila mara tunapofanya hivyo, tunagundua jambo jipya. Unapomgusa ndovu huyu leo wakati mikono yako imejaa maji au ina unyevunyevu au hata baada yo miaka mingi, unapata kumjua kwa njia tofauti. Fasihi ni kama ndovu huyu, kila mara unapoisoma unagundua jambo jipya ... (Maoni yaliyotolewa no Prof Ngugi katika mahojiano baina yoke no Dkt. Tom Odhiambo na Julias Sigei, Juni, 2, 2015). Kauli hii aliyotoa Prof Ngugi inadhihirisha ukweli kuwa msomaji wa kazi yoyote yo fasihi ana nafasi kuu katika harakati ya kuipa maana kazi ya kifasihi. Kilo mara msomaji anaposoma kazi ya kifasihi huvyaza maana mpya. Maana hizi anazopata kutoka kazi hiyo hutokana na mazingira ya msomaji, ufahamu wake na uzoefu wa kiusomaji pamoja na muktadha wa msomaji. Makala haya yanalenga kubainisha mikakati ya uchambuzi wa fasihi ya watoto kwa kuegemea mkabala wa Upokezi wa Msomaji hasa kwa kuegemea msimamo wa Rosenblatt (1995) wa "Mapatano katika usomaji." Mtazamo huu unachukulia kwamba msomaji wa kazi fulani ana mchango mkubwa katika harakati za kuipa maana kazi ya kifasihi.
  • Item
    Mchango Wajamii Yawaesha Katika Kuendeleza Lugha na Fasihi ya Kiswahili
    (CHEMCHEMI INTERNATIONAL JOURNAL OF HUMANITIES AND SOCIAL SCIENCES, 2016-07) Ngugi, Pamela Yalwala
    The Asian people arrived in Africa more than one hundred years ago from Pakistan and India. Many of them are the children of the generations that entered Kenya at the beginning of the twentieth century. They came in as merchants from Gujarati, railway workers from Punjabi and clerks from Goa. When they arrived in Kenya, they found very few Africans who understood English. So they had to use Kiswahili, a language which by then had become largely a means of communication with Africans, who were mostly domestic servants and workers in their stores. Due to this interaction, this community has contributed significantly to the language repertoire of Kenya at various levels including sociolinguistic languagsand literature. The aim of this article is to highlight the contribution of the Asian community in the field of sociolinguists, language and literature to the Kenyan community and East Africa at large.
  • Item
    Mbinu na Mikakati ya Kutumia Fasihi ya Watoto kama Bibliotherapia'
    (Journals.UDSM, 2015) Ngugi, Pamela M.Y.
    Katika ulimwengu wa sasa, sanaa ya uchoraji, dansi, muziki na hata fasihi imechukuliwa kama aina moja ya tiba kwa wagonjwa wanaougua magonjwa mbalimbali. Wataalamu wa tiba-therapia wameanza kutumia fasihi kama njia ya kuwasaidia wanajamii kukabiliana na hali mbalimbali za kijamii baada ya kugundua nafasi muhimu ya vitabu katika kutibu wagonjwa na wanajamii wengine wanaopitia hali ngumu za kijamii. Fasihi ya watoto kama ilivyo fasihi ya watu wazima ina majukumu mbalimbali katika jamii yoyote ya binadamu. Kupitia fasihi, wanajamii hujuzwa, huelimishwa na kuburudishwa. Fasihi ya watoto huwa na lengo maalum katika maisha ya watoto kwani inaweza kutumika kama kitulizo cha moyo kutokana na hali mbalimbali zinazowakumba watoto wa kisasa. Hadithi za watoto zinaweza kutumika kama njia mbadala za namna ya kukabiliana na hali ngumu za kimaisha. Usomaji wa vitabu vya fasihi ya watoto unaweza kutumika kama kichocheo cha mijadala ama darasani au hata nyumbani kuhusiana na hali mbalimbali zinazowakumba watoto katika viwango mbalimbali vya ukuaji. Lengo la makala hii ni kubainisha mbinu na mikakati ya kutumia fasihi ya watoto kama bibliotherapia. Katika kutekeleza hili, makala itaeleza dhana ya bibliotherapia pamoja na kubainisha njia mwafaka zinazoweza kutumiwa na wadau hasa walimu katika kutumia vitabu kama bibliotherapia miongoni mwa wanafunzi wao. Pamoja na hayo, mifano ya narnna bibliotherapia inavyotumika katika hali mbalimbali za watoto imetolewa.
  • Item
    Matumizi ya Teknohama na Lugha ya Kiswahili kama Nyenzo ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo: Tathmini ya Majukwaa ya Youtube naFacebook
    (CHAKITA, 2021-11) Kihara, David; Ngugi, Pamela M.
    Ulimwengll wa sasa IImeshllhlldia atbari chanya 11abasi leatilea matllmi:(j ya tekllolojia. Kwa haki/ea, learibll kila eneo la maisba ya binadamll leatilea IIlimwengll tua sasa linashllhlldia matllmi:(j ya aina mbalimbali za teknolojia katilea sekta mbalimbali, iwe elimll, biasbara na kilimo kwa lengo la kufikia malengoya Maentkleo Endeio». Hcya ni malengoya matamanio ya IIlimwengllyantryokllslldiwa kllleta maentkleo ya killChllmi, Iffllmuishwaji wa kfjamii na lIentklevll wo ma:(jngira. Mo/awapo ya malengoya maentkleo entklevlI m kHtokomeza '!foo, kuwa na IIhakilea wa chakHla, lishe bora na kHkH~ kilimo entklevll. lli kufikia lengo hili, ni mllhimll kilimo kibonshwe, kikH~ na kiwe entklevll ili ifikiapo 2030 tatizo la njoo liwe limekrvisha. Viryo hiryo, ni mllhimll kHwashirikisha wakHlima kupitia njia za mawasiliano :(jnazopatileana kwa urabisi na :(jnazoelewelea. Lugha ya KiSIVahili ina jllkllmll la kHtekeleza mawasiliano miongoni mtua wakl.lima kwa kllwa ni lugha intryowqfikia watll wengi Afrilea Mashariki. Katilea en:(j bii, nyenzo za kHwqfikia w(Jklllima ha:(jna budi kuhllsisha 1EKNOHAMA Ni leatilea mllktadha hllll ambapo maleala hii inalellga klltathmini mitandao ya kfjamii, basssan YOllTube na Facebook, kwa kHbainisha aina ya lIshallri lInaotolewa kwo waklllima na lIpoke:(j wake pomo/a na changamoto zozote wanazokumbana nazo. Hatimoye, mapentkkezo kllhusu mileakati ya kHleabiliana na changamoto hiZOyameto/ewa.
  • Item
    Fasihi katika Labaja Ibukizi. Mifano kutoka Chapisho La"Shujaaz"
    (TAASISI VA TAALUMA ZA KISWAHILI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM, 2016) Ngugi, Pamela
    Katika miaka ya hivi karibuni, kumezuka mjadala kuhusu uwezekano wa kuchapisha vitabu na makala kwa kutumia msimbo wa Sheng. Kwa upande mmoja, kuna wale wanaodai kuwa Sheng ni msimbo unaowatambulisha vijana na hivyo basi msimbo huu unaweza kutumiwa ili kuwafikia vijana hawa kwa kuchapisha vitabu au hata makala mbalimbali yanayoweza kuwafaidi (Mugubi, 2006). Kutokana na mwelekeo huu, pameibuka kijitabu kwa jina “Shujaaz”, ambacho hulenga vijana katika umri wa miaka mbalimbali. Makala hii inalenga kubaini uamilifu wa kijitabu cha Shujaaz ambacho hutumia lugha ya Sheng katika kuwasilisha jumbe mbalimbali kwa vijana. Mjadala huu utajikita katika muktadha wa taaluma ya fasihi, hasa ikichukuliwa kuwa fasihi huelemisha na huburudisha. Tunalenga kuonyesha ni kwa namna gani, kupitia msimbo wa Sheng, masuala mbalimbali yanayohusu maisha ya vijana hujadiliwa. Makala itajadili maudhui mbalimbali yanayojadiliwa katika Shujaaz na kisha kuyaoanisha na taaluma nzima ya fasihi.
  • Item
    Developmental Change and Peace among Children in Kenya
    (2015) Ngugi, Pamela M. Y.
    The concept of engaging children all over the world in participation or consultation is a relatively recent advent within the children’s right arena, and at least at first glance is an idea alive with promises and potential. This promise has special significance, given the range of conditions in Kenya that render most of the children particularly vulnerable. Thus children have been given a platform through the Children’s Assembly, through which they can engage with the many unique problems that curve out their daily existence. It is in this regard that the paper argues that given an opportunity children can be agents of peace, change and development in their own right. The paper presents information from the children’s themselves concerning their present experiences and future aspiration by examining the functions of the Children’s Assembly, Kenya and how the assembly engages children in contributing in meaningful ways to discussions of issues affecting them. By so doing, they are considered as agents of change, peace and development in relation to their engagement in the educational process, access to and negotiation of work, development of survival strategies in extreme conditions of poverty and deprivation that affects most of the children in Kenya.
  • Item
    Tathmini ya Uwasilishaji na Upokezi wa Somo la Imla katika Shule za Upili Nchini Kenya” in MULIKA:
    (ournal of the Institute of Kiswahili Research, 2020) Kurema, L.; Osore, M; Chacha, L
    Makala haya yanalenga kutoa tathmini ya uwasilishaji na upokezi wa somo la imla katika shule za upili nchini Kenya. Somo la imla limeratibiwa kwenye mtaala na Iinapaswa kufundishwa kuanzia shule za msingi hadi za upili (KIE, 2005). Somo hili ni mojawapo ya masomo katika stadi ya kuandika. Ufundishaji wa somo la imla unapaswa kuimarisha vipengele vya stadi ya kuandika lakini kwa mujibu wa utafiti wa awali uliofanywa suala hili Iinasailika. Wanafunzi katika shule za upili bado wanafanya makosa mengi ya tahajia, uakifishaji, msamiati, matamshi na sarufi ambayo yanapaswa kupunguzwa au kuondolewa kabisa na masomo katika stadi ya kuandika hasa somo la imla. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa ufundishaji wa somo la imla unaathiri stadi ya kuandika na matumizi ya lugha kwa jumla. Hata hivyo, somo la imla linaonekana kuwa na nafasi kubwa katika kuimarisha stadi ya kuandika na kuzungumza ikiwa litafundishwa ipasavyo. Kwa hivyo, makala haya yanatalii somo la imla kwa undani kwa lengo la kubainisha umuhimu, uwasilishaji na upokezi wake na kutathmini ikiwa kuna udhaifu unaofanya rnalengo ya somo hili yasiafikiwe katika kazi za wanafunzi wa shule za upili nchini Kenya. Makala haya pia yanatoa mapendekezo ya namna ya kuimarisha uwasilishaji na upokezi wa somo la imla nchini Kenya.