RP-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing RP-Department of Kiswahili and African Languages by Title
Now showing 1 - 20 of 97
Results Per Page
Sort Options
Item Athari ya Mazingira Asilia ya Mtunzi katika Matumizi ya Kujibadilisha Kimazingaombwe: Uchunguzi wa Riwaya Teule za S. Robert na E. Kezilahabi(AJOL, 2022-08) Maggati, Charles N.; Osore, Miriam; Wafula, RichardMakala haya yalikusudia kuchunguza athari ya mazingira asilia ya mtunzi katika matumizi ya kujibadilisha kimazingaombwe. Ili kulifikia lengo hilo, makala yameangazia jinsi mazingira asilia ya watunzi wawili yaani, Shaaban Robert na Euphrase Kezilahabi yalivyoathiri suala la matumizi ya mbinu ya kujibadilisha kimazingaombwe. Kazi za Shaaban Robert zilizoteuliwa ni riwaya za Adili na Nduguze (1952) na Kufikirika (1946) na kazi za Euphrase Kezilahabi zilijumuisha riwaya za Nagona (1990) na Mzingile (1991). Kujibadilisha kimazingaombwe ni mbinu ya kisanaa inayoonekana kuwa mashuhuri katika kazi za kifasihi za mihula mbalimbali. Mathalani, mbinu hii inapatikana siyo tu katika kazi za kifasihi zilizojitokeza katika kipindi cha usasabaadaye, bali pia mbinu hii inaonekana hata kwenye kazi za kale zaidi, hususani kipindi cha kabla ya usasabaadaye. Kutokana na usuli huo, riwaya za Shaaban Robert zilizoteuliwa zimewakilisha kipindi kabla ya usasabaadaye ilhali riwaya za Kezilahabi ni za kipindi cha usasa na usasabaadaye. Tumechagua riwaya zilizoandikwa katika vipindi hivyo tofauti ili kuthibitisha kuwa mbinu ya kujibadilisha kimazingaombwe ni ya kale, ilikuwako hata kabla ya kipindi cha usasabaadaye. Matokeo yanaonesha kwamba tafsiri ya dhana au wazo katika kazi ya kifasihi imefungamana mno na muktadha wa kijamii uliozaa kazi hiyo. Kutokana na athari ya muktadha wa kijamii, dhana, wazo, suala au tukio fulani linaweza kuonekana la kimazingaombwe katika kazi ya kipindi fulani ilhali dhana, wazo, suala au tukio hilohilo linaweza kuonekana kuwa la kawaida (lisilo la kimazingaombwe). Mabadiliko hayo yanaweza kusababishwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia au na maingiliano ya jamii kiutamaduni na kiimani. Kwa kuongozwa na mtazamo huu, kujibadilisha kimazingaombwe kumebainishwa katika riwaya teule na kisha imeelezwa jinsi ujitokezaji wa mbinu hii ulivyofungamana na uhalisia wa maisha ya wanajamii kadiri ya mazingira asilia yaliyowazaa, kuwalea na kuwakuza watunzi wa riwaya teule.Item Athari Ya Viarudhi Vya Ekegusii Kwa Kiimbo Cha Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Upili(East African Journal of Swahili Studies, 2023-11-10) Nyougo, Christine; Githinji, PeterMakala hii inadhamiria kuonyesha athari ya viarudhi vya Ekegusii kwa matumizi ya kiimbo cha Kiswahili sanifu. Wasailiwa wetu ni wanafunzi wa shule tatu za upili zinazopatikana katika eneo la Kisii. Tulijikita katika nadharia ya Mennen (2015) ya ujifunzaji wa kiimbo katika lugha ya pili. Nadharia hii huchunguza matatizo ambayo wajifunzaji wa lugha ya kwanza hupata wakati wa kujifunza kiimbo cha lugha ya pili. Tumejikita kwa mantiki kuwa mtagusano baina ya lugha moja na nyingine huweza kuibua kufanana au kutofautiana kimatumizi katika uenezaji wa viimbo tofauti. Tumetumia mihimili minne katika uchanganuzi wa data tuliyopata nyanjani. Mhimili wa kimfumo unashughulikia vipengele vya kiarudhi katika lugha husika na usambazaji wake, mhimili wa utekelezaji unashughulikia utaratibu wa namna ambavyo vipengele mbalimbali vya kifonolojia vinavyotekeleza majukumu yavyo katika lugha husika. Mhimili wa ujirudiaji unaangazia kiwango cha matumizi ya vipengele hivi vya fonolojia ambapo lugha hutofautiana katika kiwango cha matumizi ya vipengele vyake na mhimili wa kisemantiki unaoshughuklika maana inayopatikana kutokana na matumizi ya viarudhi husiaka. Usampulishaji wa kimaksudi ulitumiwa katika kuteua wanafunzi wa vidato tofauti katika shule tatu teule na walimu wanaofunza Kiswahili katika shule hizo. Data yetu ilitokana na hojaji, mahojiano usomaji wa sentensi pamoja na kifungu ambacho kilikuwa na aina nne za viimbo ambapo wasailiwa walizisoma kwa sauti. Data ya ziada ilitokana na usomaji wa sentensi nane za Ekegusii zenye kiimbo cha taarifa, swali, amri na mshangao ambazo zilisomwa na walimu wanaozungumza Ekegusii kama lugha ya kwanza katika shule hizo tatu. Uchanganuzi wa data ulifanywa kupitia ufasili wa data ya hojaji, mahojiano na uchunzaji wa kushiriki. Matokeo tuliyopata yalibainisha kuwa uhawilisho wa viarudhi hivi kwa kiwango kikubwa huathiri matumizi sahihi ya kiimbo cha Kiswahili ambapo wasailiwa wa lugha ya kwanza hurudufu baadhi ya vipengele vya lugha hiyo katika kiimbo cha lugha ya pili. Matokeo haya pia yalidhihirisha kuwa maumbo ya silabi katika Ekegusii, shadda, toni na wakaa huathiri matumizi ya kiimbo cha Kiswahili sanifu.Item Athari ya Washairi Wakongwe Juu ya Washairi wa Kisasa: Mfano wa Muyaka Bin Haji na Ahmad Nassir(Kioo cha Lugha, 2007) King'ei, G. K.Kwakutumiavichwavyamashairi, umbo namtindo, msamiatinamaudhui, makalahiiinavitambulishabaadhiyavipengelevyausanifuvinavyopatikanakatikaushairiwaMuyakawaMuhajinajinsiambavyovipengelehivyovimeathiri, kilakimojakwakiasichake, ushairiwa Ahmad Nassir katikadiwaniyaMalengawaMvita. MakalainatumiatungozaMuyakazilizochambuliwana Mohamed Hassan Abdulaziznakuchapishwamwakawa 1979. Humumnaonyeshakiwango cha atharizaushairiwaMuyakanakuthibitishajinsimvutomkubwanausanifuwatungozaMuyakaulivyowapendezawashairiwakarneyaishirinikama Ahmad Nassir.Item Athari za Kiswahili na lugha nyingine kwa umilisi wa lugha za mama miongoni mwa vijana: Mfano wa Gikuyu.(2012-04-30) Kamau, Stephen NjihiaItem Baadhi Ya Sifa Za Sauti Zoloto Zinazotumiwa Na Baadhi Ya Wahubiri Wa Kipentekosti Kuwasilisha Injili Na Umuhimu Wake(EANSO, 2023) Nyambura, Teresiah; Githinji, PeterMakala haya yalilenga kubainisha baadhi ya vigezo vinavyobainisha sauti zoloto zinazotumiwa na baadhi ya wahubiri wa Kipentekosti kama mtindo wa kuwasilisha injili. Tulilenga waumini wa madhehebu tofauti ya Kipentekosti katika eneo la Gilgil katika kaunti ya Nakuru. Tulitumia mihimili miwili ya nadharia ya “Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji” (Bell, 1984, 2014). Mhimili wa kwanza unadai kuwa Mtazamo wa wasikilizaji hutumika katika viwango vyote vya lugha iwe ni lugha moja au wingi lugha kwani haiangazii tu kubadilisha mtindo wa utamkaji wa sauti, bali pia uchaguzi wa jinsi ya kutamka sauti na upole wa mazungumzo. Mhimili wa pili hudai kuwa mtindo wa matumizi ya lugha katika uzungumzaji huwa chanzo cha mabadiliko katika mahusiano ya mazungumzo. Usampulishaji wa kimaksudi ulitumika kwa sababu ya urahisi wa kupata walengwa wa makala haya. Kiasa kikubwa cha data kilitokana na kanda za sauti za mahubiri mbalimbali kutoka kwa wahubiri tofauti. Hatimaye, kanda tatu ambazo wahubiri walizolota na tatu ambazo wahubiri hawakuzolota zilitumika. Kanda za mahubiri zilichujwa kwa kutumia programu ya PRAAT ili kupata sifa za kiakustika zinazobainisha sauti zoloto. Mbinu za hojaji, mahojiano na wahubiri binafsi, uchunzaji na mahojiano na makundi legwa zilitumika katika uchanganuzi na ufasili wa data. Matokeo ya utafiti yalibainisha vigezo vikuu vitano ambavyo ni kipimo cha hezi, urefu wa mawimbi ya sauti, kiwango cha desibeli, mpumuo wa sauti, kiwango cha tambo na tofauti kati ya fomanti ya kwanza na ya pili kama baadhi ya sifa zinazobainisha sauti zoloto za wahubiri wa Kipentekosti.Item The case for Kiswahili as a regional broadcasting language in East Africa(The Journal of Pan African Studies, 2009-03) Makokha, J.S.The peoples of East Africa have a long history of a rich and diverse regional heritage. Perhaps one of the most renowned aspects of this heritage is Kiswahili, the language widely spoken and understood across Eastern Africa. As the numbers of people who are proficient in the language continue to grow year after year, there have been numerous enriching perspectives on the anthropological, historical , literary and sociolinguistic aspects of Kiswahili. In this article, we offer a fresh perspective on how Kiswahili can be tapped as a resource for mobilizing popular support for the East African regional integration process across the five member states of the current East African Community: Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, and Burundi. Kiswahili should be elevated to the position of a regional broadcasting language for a proposed regional broadcasting network operating under the aegis of the East African Community in Arusha, Tanzania. This is the main argument of the article. The argument is grounded on three main points, namely, media studies indicate that ICT and FM radio stations have become very popular mass media across Africa in the past two decades; radios are ubiquitous media of communication, entertainment and education across East Africa, especially in the rural areas where the vast majority of the people still live; and a regional broadcasting service, using the popular FM mode, can be mooted by the EAC Secretariat in Arusha to promote the programs of the EAC and harness the popular support for its intentions. Kiswahili should be given priority as the chief broadcasting language, as it is a rich symbol of the shared regional heritage. The paper concludes with a proposed framework that offers a basis for further thought and action towards the realization of the foregoing.Item Children’s Literature Research in Kenyan Universities: Where Are We Now?(Center for Enhancing Knowledge, UK, 2012) Ngugi, P.Y.The history of literature written and published specifically for Kenyan children began in the 1960’s with independence from the colonial rule. Pre- colonial literature for children was oral in nature, passed down by adults in the form of folktales, myths, songs, riddles and proverbs. During the colonial period, children’s reading was confined to textbooks and Western literature which promoted western culture and values. Political independence led to the development of an intellectual climate that firmly insisted that children’s literature should work out word from the home base of the African child so that they will not become culturally stateless persons. This paper sets out to asses and describes critical studies that have been carried out in children’s literature at Kenyatta University. It should be noted that criticism and reviewing of any literary genre, including children’s literature, contributes immensely to the improved development of the literature, (Haviland, 1974: 391)Item Constraints on the Acquisition Planning of Indigenous African Languages: The Case of Kiswahili in Kenya(2011-10-27) Musau, Paul M.The paper examines the linguistic situation in Kenya and the teaching of Kiswahili in its schools. While there is widespread support for the school programme, the paper concludes that there are major problems to be overcome, particularly in the areas of attitudes, teacher training and course materials. General expressions of support for Kiswahili are of little value without effective interventions in these areas.Item The Contribution of Persian Language to Kiswahili Phonology and Lexicon(2001, 2005) Osore, Miriam; Ngugi, Pamelahe favourable climatic and sociological conditions along the East African Coast made it possible for the inhabitants of non-African countries to open up relations with the indigenous peoples of the East African Coast. Such relations existed from the remotest times and that they have continued during the passage of centuries up to the present day. Individuals and groups of people from Persia immigrated to the East African Coast almost 900 years ago. They settled temporarily as well as permanently. Owing to the trade along the coast, the necessity arose for oral understanding between the people of the coastal districts and the various immigrants. Because of these, Kiswahili lan- guage which was being spoken at the coast, both as a first language and a language of general communication has assimilated many lexical items from various languages that were spoken by different groups of sailors and visitors. This process of absorp- tion came naturally as Swaluli civilization acquired foreign concepts and influences without in any way affecting the Bantu base of the Kiswahili language. It is in this understanding that this paper addresses the contribution of the Shirazi to the development ofKiswahili language. It demonstrates that borrowing is an active and creative process that has led to the enrichment of Kiswahili language and has not as many people would have us believe, turned it into a hybrid language. Borrowing is determined by linguistic and sociolinguistic factors. The paper examines briefly the history of Waswahili and the Persian migration to the East African Coast with a view of showing how the two languages came into contact. It then goes on to show how this affected the way oflife of the Waswahili as well as Kiswahili language especially its phonology and lexicon.Item The Contribution of the Germans to the Spread and Development of Kiswahili Language and Literature(Across Boarders:, 2005) Osore, Miriam; Ngugi, PamelaFollowing the partition of Africa, Tanganyika (mainland) was declared a German colony in 1885. The German.s had a brief rule, which was terminated with their defeat in the First World War. By the time the Germans co-Ionized Tanganyika, they found that Kiswahili had already spread in the interior by Arab and Swahili caravan traders. There were also-coastal people, Kiswahili speakers, who had settled in such inland centres such as Tabora and Ujiji. Kiswahili was already serving as a form of 'linqua-franca' in the mainland Tanganyika long before the advent _of the German colonization. During the German rule, they made use of this rich 'lingua-franca' in education and administration.Item Defamiliarizing Marriage in a Patriarchal Socio-Cultural Context: An analysis of the Novels of Euphrase Kezilahabi and Said Ahmed Mohamed published in Kiswahili.(University of Dar es Salaam, 2016) Osore, MiriamA major objective of this paper is to uncover ideological assumptions on marriage that are embedded in the defamiliarization techniques that are utilized by Euphrase Kezilahabi and Said Ahmed Mohamed in their works. The controlling question is: Under what circumstances are defamiliarization techniques used and what effect do they achieve? The paper therefore discusses the aspects that defamiliarize. marriage in apatriarchal socio-cultural context in the works of the two authors. It therefore explores the relationship between the defamiliarization techniques and the socio-cultural structures. The paper further discusses the meanings. aesthetics and effects of defamiliarization devices on the readers. I argue that one of the fundamental motivations of use of defamiliarization techniques is to ideologically put forward a definite moral value. The analysis of the defamiliarization techniques makes inferences from the works under study while constructing indicators of worldview, values and attitudes, which construct and deconstruct the popular ideological and cultural beliefs and practices. Significantly, the paper directs inquiry into the relationships between power, status and solidarity, which have been ignored in most linguistic models of communication but which arefundamental to the understanding of literary texts. It is my view that normal usage of language has the important role of establishing normative concepts that define social reality, which in turn has a controlling power over individual identity. It is within this understanding that this paper discusses how defamiliarization techniques are instrumental in exposing and "questioning some of the popular ideologies, at the levels of cultural beliefs and practices especially in relation to marital confinement, gender roles in marriage and parenthood with a view of establishing their cultural and ideological underpinnings.Item Developmental Change and Peace among Children in Kenya(2015) Ngugi, Pamela M. Y.The concept of engaging children all over the world in participation or consultation is a relatively recent advent within the children’s right arena, and at least at first glance is an idea alive with promises and potential. This promise has special significance, given the range of conditions in Kenya that render most of the children particularly vulnerable. Thus children have been given a platform through the Children’s Assembly, through which they can engage with the many unique problems that curve out their daily existence. It is in this regard that the paper argues that given an opportunity children can be agents of peace, change and development in their own right. The paper presents information from the children’s themselves concerning their present experiences and future aspiration by examining the functions of the Children’s Assembly, Kenya and how the assembly engages children in contributing in meaningful ways to discussions of issues affecting them. By so doing, they are considered as agents of change, peace and development in relation to their engagement in the educational process, access to and negotiation of work, development of survival strategies in extreme conditions of poverty and deprivation that affects most of the children in Kenya.Item Dhima Ya Usimulizi Katika Uwasilishaji Wa Nyimbo Za Taarab: Uchunguzi Wa Kipengele Cha Wakati(EAST AFRICAN NATURE & SCIENCE ORGANIZATION, 2022) Misoi, Dorcas; Wafula, Richard MakhanuTaarab ni aina ya nyimbo yenye asili katika Pwani ya Afrika Mashariki. Nyimbo hizi kama zilivyo nyimbo zingine, ni zao la shughuli na hisia za binadamu. Hivyo, ujumbe katika nyimbo hizo hujikita katika miktadha mbalimbali ya jamii. Ntarangwi (2001) anasema, mbali na kuwa nyimbo za taarab huimbwa sana katika harusi za Waswahili, nyingi ya nyimbo hizo hugusia masuala mengine ya maisha kama vile uongozi, dini, urembo wa wanawake, mabadiliko ya kisiasa au hata kuhusu uchungu wa kumpoteza mpenzi. Masuala haya huwasilishwa na watribu kwa kutumia mbinu za lugha kwa ubunifu wa kiwango cha juu. Makala haya yamechunguza dhima ya usimulizi katika uwasilishaji wa nyimbo za taarab kwa kuzingatia kipengele mahsusi cha wakati. Kazi hii imeongozwa na nadharia ya naratolojia inayohusishwa na mwanafalsafa wa Kiyunani aitwaye Plato na kuendelezwa na wataalamu kama vile Genette, Stanzel, Manfred Jan na Mieke Bal. Nadharia hii inahusu usimuliaji wa hadithi. Misingi yake ni kuwa usimulizi lazima uwe na msimulizi, kitendo kinachosimuliwa, usemi kuhusu kinachofanyika, wahusika na dhamira ya usimulizi wowote hubainika kupitia kwa mtazamo wa msimulizi. Kipengele cha usimulizi cha wakati kimetumiwa kuonyesha dhima ya usimulizi katika uwasilishaji wa maudhui na mtindo wa uwasilishi katika nyimbo za taarab. Katika kufanya hivyo, makala haya yamebainisha kuwa kipengele cha usimulizi cha wakati kimedhihirika katika nyimbo teule za taarab na kimechangia kukuza maudhui na mtindo wa uwasilishi kwa kuonyesha kuwa wimbo wa taarab ni utanzu telezi unaosheheni usimulizi.Item A Digital Africa Kiswahili Holds the Key(African Journals Online, 2008) Kamau, Stephen NjihiaItem Economic Perspectives in East African Literature: A Study in Selected Novels in Kiswahili(International Journal Corner, 2021) Wafula, R. M.This paper examines economic perspectives in East African Literature with a particular focus on one author who wrote his works during the colonial times and two others who created their works in the postcolonial period. Whereas Shaaban Robert wrote his novellas in the 1950 when East African countries had not attained their independence, EuphraseKezilahabi and George KatamaMkangi wrote in 1970s to 1990s long after the formation of East African States. From reading their literary pieces, it becomes increasingly clear that the society which Shaaban Robert depicted was hierarchical in which economic points of view and attitudes depended on the class in which a person belonged. On the other hand, Kezilahabi and Mkangi portray a highly adversarial society in which economic attitudes are defined by the binary model of social description.Item An Emic Reading of Drums of Death by Chris Lukorito Wanjala, 2009(Kenya Scholars & Studies Association, 2010) Wafula, R. M.Item Fasihi katika Labaja Ibukizi. Mifano kutoka Chapisho La"Shujaaz"(TAASISI VA TAALUMA ZA KISWAHILI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM, 2016) Ngugi, PamelaKatika miaka ya hivi karibuni, kumezuka mjadala kuhusu uwezekano wa kuchapisha vitabu na makala kwa kutumia msimbo wa Sheng. Kwa upande mmoja, kuna wale wanaodai kuwa Sheng ni msimbo unaowatambulisha vijana na hivyo basi msimbo huu unaweza kutumiwa ili kuwafikia vijana hawa kwa kuchapisha vitabu au hata makala mbalimbali yanayoweza kuwafaidi (Mugubi, 2006). Kutokana na mwelekeo huu, pameibuka kijitabu kwa jina “Shujaaz”, ambacho hulenga vijana katika umri wa miaka mbalimbali. Makala hii inalenga kubaini uamilifu wa kijitabu cha Shujaaz ambacho hutumia lugha ya Sheng katika kuwasilisha jumbe mbalimbali kwa vijana. Mjadala huu utajikita katika muktadha wa taaluma ya fasihi, hasa ikichukuliwa kuwa fasihi huelemisha na huburudisha. Tunalenga kuonyesha ni kwa namna gani, kupitia msimbo wa Sheng, masuala mbalimbali yanayohusu maisha ya vijana hujadiliwa. Makala itajadili maudhui mbalimbali yanayojadiliwa katika Shujaaz na kisha kuyaoanisha na taaluma nzima ya fasihi.Item Fasihi ya Watoto kama Njia ya Kukuza Mshikamano wa Kiraifa(Moi University Press, Moi University, Eldoret, 2019) Ngugi, Pamela M. Y.Lengo la nchi yoyote iliyojikomboa kutokana na ukoloni na kupata uhuru ni kugeuza asasi za kiukoloni ilizorithi ili ziweze kuhudumia mahitaji na tamaduni za jamii mpya (Ochieng, 1985 katika Mbatia, 2012). Kenya ilipopata uhuru mwaka wa 1963, na kikwazo kikuu katika ujenzi wa taifa jipya kilikuwa ni ukabila. Wakenya waliendelea kudumisha uaminifu kwa makabila yao kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni. Hivyo basi kulikuwa na haja ya kubuni njia za kukabiliana na hali hii. Ujenzi wa utarnbulisho wa kitaifa ni muhimu katika kupunguza migogoro ya kikabila na kimbari. Utambulisho huu hauji kisadfa bali hujengwa kimakusudi kama sehemu ya ajenda ya viongozi wenye mtazamo mpana na urazini wa kitaifa. Kama anavyosisitiza Njogu (2012) "Utambulisho wa kitaifa unasaidia katika kuimarisha asasi za utawala bora, kuwajibisha viongozi na kuweka uwazi katika utoaji huduma kwa umma." Tangu enzi za kabla ya uhuru hadi sasa, Kiswahili kama lingua franka kimeweza kutoa mchango muhimu katika kujenga mshikamano wa kitaifa, (Mbatia, 2012). Kwa mfano, mara tu baada ya uhuru Kiswahili kilichangia katika kujenga tabaka la wafanyikazi ambalo lilijumlisha watu kutoka makabila mbalimbali. Watu waliotoka mashambani na kuja kufanya kazi katika miji mbalimbali walilazimika kutumia Kiswahili ili kuweza kuwasiliana. Hivyo basi lugha ya Kiswahili ikawa mojawapo wa nyenzo za kujenga utaifa wa Kenya. Baada ya uhuru, serikali ya Kenya iliteua TUl11eya Ominde chini ya Uenyekiti wa Prof S.H. Ominde. Jukumu la tume hiyo lilikuwa ni kushauri serikali kuhusu utungaji na utekelezaji wa sera ya elimu baada ya kufanya uchunguzi uliohitajika. Tume hii iliibuka na malengo kadhaa ya elimu nchini Kenya.Lengo mojawapo la elimu lilikuwa na lingali ni kukuza utaifa, uzalendo na kuendeleza umoja wa taifa. Hivyo basi, elimu inayotolewa inahitaji kuziheshimu tamaduni mbalimbali zilizopo nchini na wakati uo huo, kuhakikisha kuwa haiendelezi ubaguzi katikajamii kwa misingi ya rangi, ukabila na dini. IIi kutekeleza lengo hili na malengo mengine, wasomi wengi wanaamini kuwa ufundishaji wa fasihi kwa jumla na hasa fasihi ya watoto unaweza kuchangia katika kuyafikia malengo haya kwa kukuza hisia za kitaifa miongoni mwa wanafunzi. ,- Ujenzi wa taifa ni juhudi za makusudi na za kujitolea. Tangu uhuru, wananchi wamekuwa wakitafuta njia za kuleta utangamano baina ya makabila na nchi mbalimbali za Afrika. Hatua moja kuhusu ujenzi wa taifa ni uimarishaji wa utamaduni wa tamaduni mbalimbali. Utamaduni wowote ule utaeleweka vyema kwa kuchunguza mila na desturi zilipo katika jamii husika, pamoja na kufahamu namna kila jamii ilivyowasilisha amali zake mbalimbali kama vile, ukarimu, kujitolea, haki na maslahi ya pamoja, mambo ambayo yalichangia katika kuunda utaifa. Ufahamu wa amali hizi waweza kupatikana kupitia fasihi za jarnii hizi. Fasihi ni matokeo ya shughuli za jamii; huibuka, hukua na kusambaa kutokana na mazingira yaliyopo katika jamii. Lengo la sura hii ni kubainisha dhima ya fasihi ya watoto kama kichochezi cha kujengaItem Fasihi ya Watoto katika Ufundishaji wa Kiswahili katika Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki(KAKAMA, 2019) Ngugi, PamelaUtafiti uliofanywa na shirika la Uwezo - Kenya kuanzia mwaka wa 2014 hadi 2016 kuhusu "Are our Children Reading?" umethibitisha kuwa watoto wengi hasa katika shule za msingi hawajui kusoma na kuandika kwa mujibu wa viwango vya madarasa waliyomo. Kwa sababu hiyo, shirika hili limependekeza mabadiliko katika ufundishaji na kupendekeza kuturnika kwa mkabala jumuishi wa elimu iwapo sekta ya elimu inatarajia kupata maendeleo thabiti. Mkabala jumuishi huhimiza wanafunzi kushiriki katika ujifunzaji wao na hivyo basi, kusaidia katika ukuzaji wa maarifa ya kufikiria kwa kiwango kikubwa. Katika kufanya hivi, ujifunzaji huwa wa maana kwa mwanafunzi na huchangia katika kujenga stadi nne za lugha ambazo ni: kusikiliza, kuongea, kusoma na kuandika, kusikiliza na kuongea kwa kiwango cha juu. Lengo la makala hii ni kujadili na kubainisha namna ambavyo fasihi ya watoto inaweza kutumika kama kichocheo cha kujua kusoma na kuandika, hasa pale ambapo wanafunzi wanapewa nafasi ya kujenga maana kutokana na usomaji wao. Fasihi ya watoto inaweza kuchangia katika kuinua maarifa, stadi na milelekeo chanya miongoni mwa wanafunzi kuhusiana na masuala ya kusoma na kuandika hali ambayo itachangia katika kufikia lengo la 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu katika sekta ya elimu kuhusiana na kuhakikisha Mitaala ya Kiswahili katika Vyuo Vikuu rya Afrika Mashariki I 212 kuwa watoto wanapata elimu bora na yenye usawa kwa wote na kutoa furs a kwa wote kujiendeleza (UN, 2015) katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Fasihi ya Watoto katika ElimuItem Femininity and Masculinity in the Novels of Euphrase Kezilahabi and Said Ahmed Mohamed(University of Dar es Salaam, 2015) Osore, Miriam