Maudhui ya Ukungwi katika Nyimbo Teule za Taarab
Loading...
Date
2025-07
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies
Abstract
Nyimbo za taarab zimetafitiwa na wataalam mbalimbali kwa mitazamo
tofautitofauti. Kutokana na uchunguzi wa kina wa mtafiti, inabainika kuwa
tafiti za awali kuhusu nyimbo za taarab, zimeegemezwa kwenye uchunguzi
wa mafumbo katika taarab, masuala ya itikadi,
nafasi ya mwanamke katika
nyimbo za taarab usimulizi pamoja na uchanganuzi wa taswira katika
nyimbo za taarab. Swala la jumbe za nyimbo za taarab kufungamana na
mambo ya kijamii yakiwemo utamaduni limetajwa tu kijuujuu katika tafiti
zao. Kutokana na upeku
zi wa kina wa mtafiti, hakuna utafiti ambao
umefanywa kuhusu dhima ya kungwi inavyotekelezwa na baadhi ya nyimbo
za taarab. Utafiti huu ulihusu ubainishaji wa maudhui ya ukungwi katika
nyimbo teule za taarab. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Simiotik
i.
Nadharia hii iliasisiwa na Ferdinand Dessaussure (1983) na Charles Pierce
(1998) na inahusu uhusiano uliopo kati ya kitaja na kitajwa na matumizi ya
ishara, picha na msimbo. Nguzo hii ilisaidia katika kufafanua mbinu za
uwasilishaji wa ujumbe katika n
yimbo teule za taarab. Data ya kimsingi
iliyoichanganuliwa ilikuwa ya maktabani ambapo mtafiti alipakua nyimbo
teule kutoka kwenye mtandao wa You Tube na kuzichanganua kwa kina.
Matokeo yalionyesha kuwa kungwi ana jukumu la kuwafundisha wanawari
kuhusu mas
uala ya unyumba yakiwemo usafi wa mwili na nyumba, namna
ya kumhudumia mume, namna ya kusema na marafiki na jamaa za mume,
matumizi ya vifaa vya kiasili kama vile mbuzi, kinu, mchi ufagio miongoni
mwa mengine. Aidha, maudhui haya ya ukungwi yanafundishwa n
a
waimbaji wa nyimbo teule za taarab
Description
Article
Keywords
Citation
Wendo, F. H. & Titus, K.(2025). Maudhui ya Ukungwi katika Nyimbo Teule za Taarab.East African Journal of Swahili Studies, 8(2), 119-132. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3347