Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leola Kenya.

Loading...
Thumbnail Image
Date
2021-11
Authors
Mutuku, Fidelis Kioko
Onyango, Jacktone o.
Mwita, Leonard Chacha
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Editon Consortium
Abstract
Makala hii inaonyesha tofauti iliyopo kati ya majukumu na maumbo ya uhusika katika vichwa vya habari vya siasa kwenye gazeti la Taifa Leo. Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charles Fillmore mnamo mwaka wa 1968 imeongoza uchunguzi huu. Utafiti huu umefanywa baada ya kubaini kuwa wasomi mbalimbali wa gazeti hutafsili maana anuwai kwenye kichwa kimoja cha habari za siasa. Jambo hili husababisha utata wa kimaana na uenezaji wa jumbe zisizoithibatika katika jamii, hivyo basi, kuzalisha migogoro ya kisiasa nchini. Upekuzi wa yaliyomo kwenye matoleo ya gazeti la Taifa Leo ambayo yametawaliwa na vichwa vya habari za siasa na kuchapishwa kati ya mwaka 2017-2019 ni msingi wa data ya utafiti huu. Vichwa kumi na vinane vya habari za siasa vilisampulishwa kimakusudi na kutumika katika uchambuzi wa uchunguzi huu. Data katika makala hii imewasilishwa kupitia mfumo wa majedwali na maelezo. Matokeo ya tathmini ya uchunguzi huu yameshikilia kwamba Kiswahili hakina maumbo dhahiri ya uhusika ispokuwa katika nomino ambazo nafasi yake yaweza kuchukuliwa na viwakilishi vya nafsi ya pili na tatu umoja na wingi. Katika vichwa vya habari ambavyo nomino zake si za ngeli ya A-WA, viwakilishi faafu vya nomino hizo huchukua nafasi hiyo na kuwa maumbo ya uhusika. Kila aina ya uhusika ina jukumu lake la uhusika. Majukumu ya uhusika ni dhahania na hubadilika kulingana na aina ya uhusika. Uchunguzi huu utakuwa wenye umuhimu kwa wasomi wa magazeti na taifa kijumla. Wasomi wa magazeti wataongozwa na kigezo cha dhima ya maneno katika tungo kudondoa maana sawa katika vichwa lengwa vya habari za kisiasa na kupitisha tafsili hiyo moja kwa wanajamii. Kwa kufanya hivi, migogoro ya kisiasa katika jamii iletwayo na tafsili mbalimbali za kimaana itafutiliwa mbali.
Description
Article
Keywords
Uhusika, jukumu, umbo, kauli na hali, Taifa leo
Citation
Mutuku, F. K., Onyango, J. & Mwita, L. C. (2021). Tofauti kati ya majukumu na maumbo ya uhusika katika vichwa vya habari za siasa kwenye gazeti la taifa leola Kenya. Editon Cons. J. Kiswahili,3(1), 335-347.