Sera ya Lugha na Mabadiliko ya Kimaudhui ya Ushairi wa Kiswahili kati ya Miaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzania

Loading...
Thumbnail Image
Date
2023
Authors
Njuguna, Helina Wanjiku
King’ei, Geoffrey Kitula
Wafula, Richard Makhanu
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Makala hii inachunguza jinsi sera ya lugha ya kipindi cha ukoloni ilivyochochea mabadiliko ya kimaudhui ya ushairi wa Kiswahili kati ya mwaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzania. Kulingana na makala hii hali ni matukio mahsusi yanayoathiri ubunifu wa maudhui ya ushairi. Ili kukuza mjadala wetu, makala hii imezingatia sera ya lugha ya kipindi cha utawala wa Wajerumani na Waingereza. Uchunguzi unazingatia mashairi teule kutoka diwani za watunzi wafuatao: Mathias Mnyampala, “Diwani ya Mnyampala (1965)”, Amri Abedi, “Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri (1954)”, Akilimali Snow-White, “Diwani ya Akilimali (1963)”, Shaaban Robert , “ Koja la Lugha (1969), Pambo la Lugha (1966), Kielezo cha Fasili (1968), na Masomo Yenye Adili (1967)”, na Saadani Kandoro, “Mashairi ya Saadani, (1966)”. Mashairi yaliyoteuliwa yanasomwa na kuhakikiwa ili kubainisha maudhui yaliyomo. Uchanganuzi wa data unaongozwa na mihimili ya Nadharia ya Utegemezi na Nadharia ya Ubidhaaishaji wa Lugha. Katika mashairi teule, inabainishwa namna washairi walivyotetea na kuinua hadhi ya lugha ya Kiswahili kwa kueleza sifa na umuhimu wake katika ushairi wao. Pia, inadhihirishwa jinsi ushairi uliotungwa kwa Kiswahili sanifu ulivyotumiwa kama chombo cha umma cha kujieleza kwa kupigania haki, usawa, na uhuru pamoja na kuwahimiza wananchi wakae kwa amani, udugu na heshima.
Description
Article
Keywords
Sera ya Lugha, Ushairi, Mabadiliko, Ubunifu, Maudhui, Utegemezi, Ubidhaaishaji
Citation
Wanjiku, N. H., & Makhanu, W. R. (2023). Sera ya Lugha na Mabadiliko ya Kimaudhui ya Ushairi wa Kiswahili kati ya Miaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzania. Mwanga wa Lugha, 8(1), 25-36.