Usawiri wa Mhusika Mkinzani Katika Tamthilia Teule za Ebrahim Hussein: Kinjeketile (1969), Jogoo Kijijini (1976) na Arusi (1980)
Loading...
Date
2024-10
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili
Abstract
Makala hii imechunguza usawiri wa mhusika mkinzani katika tamthilia teule za Ebrahim Hussein; Kinjeketile (1969), Jogoo Kijijini (1976) na Arusi (1980). Swala la usawiri wa wahusika katika kazi za fasihi limeshughulikiwa na watafiti mbalimbali kwa mitazamo tofautitofauti. Usawiri wa wahusika wa kiume umetafitiwa na Kanwa (2022), nao unaohusu usawiri wa wahusika watoto umefanywa na Moige (2015). Aidha, Kitali (2011) naye ameshughulikia usawiri wa wahusika wa kike. Kutokana na uchunguzi wa watafiti, inabainika kuwa tafiti za awali kuhusu usawiri wa wahusika zimejikita kwenye wahusika wa kike, wa kiume, watoto, walemavu na wahusika kwa ujumla wasio wakinzani. Hivyo, panaibuka haja ya kumchunguza mhusika mkinzani na namna anavyosawiriwa katika tamthilia teule. Makala hii imeongozwa na nadharia ya Naratolojia ambayo iliwekewa msingi na Plato (1955) kisha ikandelezwa na Raglan (1936), Genette (1980) na Rimmon-Kennan (1983). Naratolojia inahusika na vipengele vya usimulizi vikiwemo; wakati, nafsi, nafasi, na wahusika. Kipengele cha wahusika ndicho nguzo iliyotumika katika utafiti huu kwani kinaelezea mbinu za usawiri wa wahusika na namna wanavyokuza maudhui. Data iliyotumika ilitolewa maktabani ambapo tamthilia teule, makala na vitabu vinavyohusiana na mada vilisomwa na kuchambuliwa kwa kina. Uwasilishaji wa matokeo umefanyika kw a njia ya maelezo yaliyoambatanishwa na dondoo mwafaka kutoka tamthilia teule. Matokeo yameonesha kuwa, katika tamthilia ya Kinjeketile na Jogoo Kijijini, mhusika mkinzani amechorwa kama mhusika asiyekuwepo kwenye jukwaa na ukinzani wake unabainika kupitia wanachokisema wahusika wengine na msimulizi kuhusu matendo yake. Mbinu alizosawiriwa nazo ni ya kuwatumia wahusika wengine, ya kinatiki, ya ulinganuzi na usambamba na ya kimaelezo. Kwa upande mwingine, mhusika mkinzani katika tamthilia ya Arusi amechorwa kama mhusika aliyepo kwenye jukwaa na ukinzani wake unabainika kupitia matendo na mazungumzo yake ya moja kwa moja na wahusika wengine jukwaani pamoja na wanachokisema wahusika wengine kumhusu. Mbinu alizosawiriwa nazo ni ya kinatiki na ya kuwatumia wahusika wengine
Description
Article
Keywords
Citation
Oluchili, W. & Makhanu, R. W. (2024). Usawiri wa Mhusika Mkinzani Katika Tamthilia Teule za Ebrahim Hussein: Kinjeketile (1969), Jogoo Kijijini (1976) na Arusi (1980). East African Journal of Swahili Studies, 7(1), 477-491. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2268.