Matumizi ya Filamu Katika Kufunzia Sarufi ya Kiswahili Nchini Kenya
Loading...
Date
2025-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies,
Abstract
Makala haya yananuia kuchunguza uwezekano wa kutumikiza filamu ili
kuimarisha utendaji wa sarufi katika lugha ya Kiswahili. Ni wajibu wa
mwalimu kuteua matumizi ya nyenzo inayomwezesha kuibua mazingira
halisi ya kufunzia sarufi darasani. Hata hivyo licha ya wanafunzi katika
jimbo la Nyeri kutumia lugha ya Kiswahili katika shughuli zao za kila siku
matokeo ya mtihani katika somo la Kiswahili hasa katika mtihani wa KCSE
yalikuwa dhaifu mnamo katika mwaka wa 2019. Hii ndiyo sababu
iliyomchochea mtafiti wa kazi hii kuchunguza matumizi ya filamu na athiri
zake kwa utendaji wa wanafunzi katika lugha ya Kiswahili katika shule za
upili. Wanafunzi katika shule za upili hawajakuwa wakifanya vyema katika
karatasi ya Sarufi. Kulingana na wataalamu filamu imekuwa ikitumikizwa
katika kufunzia lugha ya Kingereza huko Umarekani na Uingereza na pia
somo la Hisabati katika Afrika Kusini ambapo iliripotiwa kwamba
wanafunzi waliotumikiza filamu walifanya vyema katika kujifunza
Kingereza na Hisabati. Nchini Kenya filamu imekuwa ikitumikizwa na
walimu katika kufunzia somo la Fasihi na hivyo kubagua kipengele cha
sarufi. Pengo hili liliibua haja ya kutafitia matumizi ya filamu katika
kufunzia sarufi ya Kiswahili angalao kuboresha matokeo ya karatasi ya pili
yaani inayojulikana kama sarufi au Matumizi ya Lugha. Makala haya
yaliongozwa na Nadharia ya utabia ya Hermer (1996), kupitia kwa mihimili
yake tofauti. Utafiti huu ulitekelezwa maktabani na nyanjani. Utafiti wa
maktabani ulichangia kutambua usuli wa matumizi ya filamu ulimwenguni.
Utafiti wa nyanjani ulifanyika katika eneo la Mukurweini linaloakilisha
jumuiya ya wanafunzi wanaotumia silibasi sawia na wanafunzi wengine
kote nchini Kenya. Sampuli zilizotumikizwa ziliteuliwa kimakusudi na kwa
njia za kuelezea. Katika ukusanyaji data utafiti huu ulizingatia mbinu za
hojaji, Uchunzaji na mtihani kwa wanafunzi. Data iliyokusanywa
ilichanganuliwa na kuwasilishwa kupitia michoro na maelezo tofauti.
Kufuatia jinsi wanafunzi wamekuwa wakipata gredi dhaifu katika sarufi kwa
muda wa miaka mitano mfululizo. Kwa majubu wa matokeo ya utafiti....
Description
research article
Keywords
Citation
Mburu, R., Babusa, H. O. & Ngugi, B. (2025). Matumizi ya Filamu Katika Kufunzia Sarufi ya Kiswahili Nchini Kenya. East African Journal of Swahili Studies, 8(1), 90-104. https://doi.org/10.37284/jammk.8.1.2628