Wakaa katika Hotuba Teule za Wanasiasa wa Kenya
Loading...
Date
2025-08
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies
Abstract
Makala hii inachunguza ubainishaji wa wakaa katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Baadhi ya wanasiasa hutoa hotuba zinazovuta makini ya wasikilizaji na wafuasi wao kwa mitindo tofauti. Mojawapo wa mbinu hii ya kimtindo ni usimulizi. Wakaa ni mojawapo wa kipengele cha kimtindo katika usimulizi. Tafiti kadha zimefanywa kubainisha wakaa na matumizi yake katika tanzu za fasihi andishi na fasihi simulizi (taz. Kwaka; 2015; Khamis; 2015; Muiya; 2018; Kinga; 2020; Asige, 2021). Licha ya hayo, tafiti hizi za awali hazikushughulikia wakaa kwa kuhusisha moja kwa moja si hotuba tu bali hotuba za kisiasa. Ni katika msingi huu ndipo makala hii imechunguza jinsi wakaa inavyojitokeza katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Makala hii imeelekezwa na nadharia ya Naratolojia iliyoasisiwa na mwanafalsafa Plato katika chapisho lake The Republic na baadaye ikaendelezwa na mwanafunzi wake Aristotle (1920) aliyewasilisha mawazo yake katika chapisho la The Poetics na wananaratolojia wa hivi majuzi Gennette (1980), Prince (1982) na Rimmon-Kenan (2002). Uchunguzi huu ulizingatia mawazo yake Rimmon-Kenan. Naratolojia ni stadi ya aina ya utendaji kazi wa usimulizi. Huangalia undani wa vifaa vinavyoongoza maelezo ya simulizi na ufahamu wa utendaji kazi wake. Data iliyotumika katika makala hii imetokana na kusoma machapisho maktabani kama vile tasnifu, majarida na vitabu. Halikadhalika, utazamaji, usikilizaji na uchambuzi wa hotuba teule za wanasiasa Mhes. Kenyatta, Odinga na Ruto katika mtandao wa YouTube ulihusishwa. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwepo kwa vipengele vya wakaa vya mpangilio, muda na idadi au umara katika hotuba za wanasiasa. Isitoshe, imebainika kuwa kipengele hiki cha usimulizi kimetumiwa kuendeleza maudhui, fani za lugha na kuchimuza wahusika.
Description
Article
Keywords
Citation
Stanley, M. K. & Kaui, T. (2025). Wakaa katika Hotuba Teule za Wanasiasa wa Kenya. East African Journal of Swahili Studies, 8(2), 173-187. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3485