Athari Ya Viarudhi Vya Ekegusii Kwa Kiimbo Cha Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Upili
Loading...
Date
2023-11-10
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies
Abstract
Makala hii inadhamiria kuonyesha athari ya viarudhi vya Ekegusii kwa matumizi ya kiimbo cha Kiswahili sanifu. Wasailiwa wetu ni wanafunzi wa shule tatu za upili zinazopatikana katika eneo la Kisii. Tulijikita katika nadharia ya Mennen (2015) ya ujifunzaji wa kiimbo katika lugha ya pili. Nadharia hii huchunguza matatizo ambayo wajifunzaji wa lugha ya kwanza hupata wakati wa kujifunza kiimbo cha lugha ya pili. Tumejikita kwa mantiki kuwa mtagusano baina ya lugha moja na nyingine huweza kuibua kufanana au kutofautiana kimatumizi katika uenezaji wa viimbo tofauti. Tumetumia mihimili minne katika uchanganuzi wa data tuliyopata nyanjani. Mhimili wa kimfumo unashughulikia vipengele vya kiarudhi katika lugha husika na usambazaji wake, mhimili wa utekelezaji unashughulikia utaratibu wa namna ambavyo vipengele mbalimbali vya kifonolojia vinavyotekeleza majukumu yavyo katika lugha husika. Mhimili wa ujirudiaji unaangazia kiwango cha matumizi ya vipengele hivi vya fonolojia ambapo lugha hutofautiana katika kiwango cha matumizi ya vipengele vyake na mhimili wa kisemantiki unaoshughuklika maana inayopatikana kutokana na matumizi ya viarudhi husiaka. Usampulishaji wa kimaksudi ulitumiwa katika kuteua wanafunzi wa vidato tofauti katika shule tatu teule na walimu wanaofunza Kiswahili katika shule hizo. Data yetu ilitokana na hojaji, mahojiano usomaji wa sentensi pamoja na kifungu ambacho kilikuwa na aina nne za viimbo ambapo wasailiwa walizisoma kwa sauti. Data ya ziada ilitokana na usomaji wa sentensi nane za Ekegusii zenye kiimbo cha taarifa, swali, amri na mshangao ambazo zilisomwa na walimu wanaozungumza Ekegusii kama lugha ya kwanza katika shule hizo tatu. Uchanganuzi wa data ulifanywa kupitia ufasili wa data ya hojaji, mahojiano na uchunzaji wa kushiriki. Matokeo tuliyopata yalibainisha kuwa uhawilisho wa viarudhi hivi kwa kiwango kikubwa huathiri matumizi sahihi ya kiimbo cha Kiswahili ambapo wasailiwa wa lugha ya kwanza hurudufu baadhi ya vipengele vya lugha hiyo katika kiimbo cha lugha ya pili. Matokeo haya pia yalidhihirisha kuwa maumbo ya silabi katika Ekegusii, shadda, toni na wakaa huathiri matumizi ya kiimbo cha Kiswahili sanifu.
Description
Journal Article
Keywords
Citation
Nyougo, C., & Githinji, P. (2023). Athari Ya Viarudhi Vya Ekegusii Kwa Kiimbo Cha Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Upili. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 6(1), 468-482.