Umuhimu wa Vipengele vya Kiisimu katika Kuendeleza Kazi ya Mashairi Huru

Loading...
Thumbnail Image
Date
2025-04
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies
Abstract
Makala hii imelenga kuchunguza umuhimu wa vipengele vya kiisimu katika kuendeleza kazi ya mashairi huru ya Kiswahili katika diwanı teule za Kithaka wa Mberia na Kezilahabi. Diwani teule zilizochanganuliwa ni: Doa, Mvumo wa Helikopta, Msimu wa Tisa, Kichomi na Karibu Ndani. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Fonolojia Mizani ambayo iliasisiwa na Liberman (1975) na kuendelezwa na Liberman na Prince (1977), Nadharia ya Fonolojia mizani inadai kuwa mkazo katika lugha uko katika mfumo wa mfuatano wiani wa kimsonge ambao hupanga silabi maneno na virai katika sentensi. Vipengele vya kiisimu vilivyochanganuliwa ni: aina za sentensi, kipengele cha nafsi na uakifishaji. Utafiti huu ulitumia sampuli ya kimakusudi katika kuteua diwani teule. zilizohakikiwa. Data Iliyotumika katika utafiti huu ilikusanywa kutoka maktabani. Ni Maktabani ndiko tuliweza kusoma mashairi kutoka katika diwani teule, nadharia ya utafiti na vitabu vingine vinavyohusiana na mada ya utafiti huu. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia mbinu ya uhakiki matini kwa kuongozwa na pengo la utafiti. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo yaliyoambatanishwa na mifano ya beti mwafaka za mashairi kutoka katika diwani teule. Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kuwa vipengele vya isimu vinachangia pakubwa katika kuendeleza kazi ya mashairi huru ya Kiswahili. Utafiti lengwa umechangia katika taaluma ya ushairi kwa kuelewa umuhimu wa vipengele vya kiisimu katika kuendeleza kazi ya mashairi huru ya Kiswahili. utafiti huu unapendekeza wasomaji wa mashairi, huru wazingatie matumizi ya vipengele vya kiisimu katika kuendeleza kazi ya mashairi huru ya Kiswahili.
Description
Article
Keywords
Citation
Wafula, P. N. & Masinde, E. (2025). Umuhimu wa Vipengele vya Kiisimu katika Kuendeleza Kazi ya Mashairi Huru. East African Journal of Swahili Studies, 8(1), 285-300. https://doi.org/10.37284/jammk.8.1.2918