Uhusika katika Vichwa vya Habari za Siasa

Loading...
Thumbnail Image
Date
2021
Authors
Mutuku, Fidelis Kioko
Onyango, Jacktone
Mwita, Leonard Chacha
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
EAST AFRICAN NATURE & SCIENCE ORGANIZATION
Abstract
Uhusika ni dhana ya kisarufi ambayo hutumiwa kuonyesha dhima ya maneno katika tungo. Dhana hii ni muhimu katika uchambuzi wa tungo kwani hunuia kuwasilisha ujumbe wa kisemantiki uliogubikwa katika muundo wa ndani. Makala hii inadhihirisha dhana mbalimbali za uhusika na jinsi zinavyojitokeza katika vichwa vya habari za siasa zilizoko kwenye magazeti teule ya Taifa Leo. Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charles Fillmore mnamo mwaka wa 1968 imeongoza uchunguzi huu. Utafiti huu umefanywa baada ya kubaini kuwa wasomaji mbalimbali wa gazeti hufasiri maana anuwai kwenye kichwa kimoja cha habari za siasa. Jambo hili husababisha utata wa kimaana na uenezaji wa jumbe zisizo thabiti katika jamii, hivyo basi, kuzalisha migogoro ya kisiasa nchini. Upekuzi wa yaliyomo kwenye matoleo ya gazeti la Taifa Leo ambayo yametawaliwa na vichwa vya habari za siasa na kuchapishwa kati ya mwaka 2017-2019 ni msingi wa data ya utafiti huu. Vichwa vya habari za kisiasa kumi na nane vilisampulishwa kimakusudi na kutumika katika uchambuzi wa uchunguzi huu. Data katika makala hii imewasilishwa kupitia mfumo wa majedwali na maelezo. Matokeo ya utafiti huu yameshikilia kwamba, mahusiano kati ya kitenzi na nomino au kiwakilishi chake katika sentensi hubainisha aina ya uhusika. Uchunguzi huu una umuhimu kwa wasomi wa magazeti na taifa kijumla. Wasomaji wa magazeti wameongozwa na kigezo cha dhima ya maneno katika tungo ili kudondoa maana sahihi katika vichwa lengwa vya habari za kisiasa na kupitisha fasiri hiyo moja kwa wanajamii.
Description
Article
Keywords
Uhusika, Uhusika Kiima, Uhusika Mahali, Uhusika Yambwa, Uhusika Tendea, Uhusika Tokeo, Uhusika Ala, Muundo Ndani, Muundo Nje
Citation
Mutuku, F. K., Onyango, J., & Mwita, L. C. (2021). Uhusika katika Vichwa vya Habari za Siasa. East African Journal of Swahili Studies, 4(1), 58-67. https://doi.org/10.37284/eajss.4.1.494