Ukiukaji wa Kanuni Bia za Greenberg katika Miundo ya Tungo Zenye Vihusishi Katika Lugha ya Kiswahili
Loading...
Date
2023-11
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
EANSO
Abstract
Makala haya yalidhamiria kubaini ukiukaji wa baadhi ya kanuni bia za
Greenberg katika miundo ya tungo zenye vihusishi vya Kiswahili. Katika
utafiti wake, Greenberg (1963), alipendekeza kanuni bia 45 na kutafiti lugha
30 ili kuchunguza mpangilio wa vipashio vya kiisimu katika makundi
mbalimbali ya lugha. Lugha ya Kiswahili ilikuwepo mojawapo ya sampuli
alizoteua. Hata hivyo, katika kuzingatia uwekaji vihusishi, inaonekana
kukiuka baadhi ya kanuni hizo. Kwa hivyo, mkabala wa Greenberg (1963)
ulitumika. Kanuni bia za Greenberg hasa zile zinazozungumzia vihusishi
pekee zilitumika kuchanganua miundo na mazingira ya kiisimu
yanayosababisha ukiukaji wa baadhi ya kanuni za Greenberg katika uwekaji
wa vihusishi vya Kiswahili. Data iliyotumika ilikuwa ni tungo zenye
vihusishi. Mbinu ya usampulishaji wa kimakusudi ilitumika kuteua
vihusishi hivi na vilikusanywa kwa kusoma vitabu vya sarufi na makala
kutoka kwenye majarida na makala ya mtandaoni. Data ilichanganuliwa na
kuwasilishwa kwa kuzingatia mkabala wa kanuni bia za Greenberg kupitia
ufafanuzi wa data kwa njia ya maelezo na unukuzi wa kanuni bia za
Greenberg. Ilijidhihirisha kuwa baadhi ya kanuni bia za Greenberg zina
ukiushi katika lugha ya Kiswahili. Ukiushi hasa ulitokea kwa sababu sifa A
haikumiliki sifa B kwa kuzingatia sheria ya uchanganuzi iliyopeanwa. Haya
yalibainika hasa kwa kuwa lugha ya Kiswahili inamiliki aina mbili za
vihusishi; vihusishi vya kabla ya nomino na vihusishi vya baada ya nomino
katika umbo lake la nje. Hata hivyo, baadhi ya kanuni bia zingine
zilionyesha utiifu. Aidha baadhi ya kanuni hizi zina utata ambao unaleta
changamoto katika juhudi za kutoa kauli jumlishi. Makala haya yatachangia
katika kongoo ya utaratibu wa vipashio katika sentensi, taipolojia ya lugha
na sintaksia ya Kiswahili.
Description
Article
Keywords
Citation
Ongwae, J. K. & Githinji, P. (2023). Ukiukaji wa Kanuni Bia za Greenberg katika Miundo ya Tungo Zenye Vihusishi Katika Lugha ya Kiswahili. East African Journal of Swahili Studies, 6(2), 30-43. https://doi.org/10.37284/jammk.6.2.1596.