Tathmini ya Uamilifu wa Kiswahili Nchini Uganda: Mintarafu, Ueneaji wa Matumizi Yake Kwenye Asasi ya Uchapishaji
Loading...
Date
2022
Authors
Rais, Abdu Salim
Onyango, Jacktone
Mbaabu, George Ireri
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
ENSO
Abstract
Kwa muda mrefu, Kiswahili kilifundishwa nchini Uganda kama taaluma ya Kigeni, licha ya kuwa lugha rasmi ya pili, baada ya Kiingereza (GoU, 1995). Hata hivyo, Kiswahili kina dhima kubwa katika asasi za muziki, ulinzi na elimu ambako Uamilifu wake unadhihirishwa na ueneaji wa matumizi yake (Mbaabu, 1991na Mlacha, 1995). Ingawa Kiswahili kilienea nchini Uganda, kabla ya kufikia mwishoni mwa wakati wa kukamilisha utafiti huu, viwango vya Uamilifu wake vilikuwa havijatathminiwa kitaaluma kupitia asasi ya uchapishaji. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa, kutathmini Uamilifu wa Kiswahili kutokana na ueneaji wa matumizi yake kupitia asasi ya Uchapishaji. Uamilifu wa Kiswahili ulichunguzwa kwa kutumia Nadharia ya Uamilifu iliyoasisiwa na Wanasosholojia Auguste Comte (1787-1857), Herbert Spencer (1830-1903), Vilfredo (1848-1917) na Emile Durkheim (1857-1917) na kuendelezwa na Mesthrie na wenzake (2004). Nadharia ya Uamilifu iliangazia jukumu lililotekelezwa na fani katika jamii mahsusi(Mesthrie et al., 2004).Kiini cha Uamilifu ni uwezekano wa kuweko kwa fani yenye vijisehemu mahsusi ambapo kila kijisehemu huchangia maendeleo kwa kutekeleza jukumu mahsusi katika fani hiyo (Mesthrie et al., 2004). Nadharia hiyo ilisaidia kutathmini dhima ya ueneaji wa matumizi ya Kiswahili kupitia Asasi ya Uchapishaji nchini Uganda. Istilahi Ueneaji hutokana na kitenzi enea chenye maana ya kuwa kila mahali. Kuenea katika muktadha huo, kulimaanisha kusambaa kwa matumizi ya Kiswahili nchini Uganda kwa kupitia asasi ya uchapishaji. Ueneaji ni hali ambapo fani fulani husambaa ijapokuwa muundo huweza kubadilika kulingana na mazingira. Wataalamu wa Ueneaji walishikilia kwamba, fani huweza kupenya kuta za kikabila na kuzagaa zaidi kutoka jamii zilizoendelea, kuelekea zisizoendelea (Buliba et al., 2014). Ithibati ni kwamba, fani za lugha za Watawala Wakoloni zinapatikana
Description
article
Keywords
Uamilifu, Uchapishaji, Ueneaji
Citation
Rais, A., Onyango, J., & Mbaabu, I. (2022). Tathmini ya Uamilifu wa Kiswahili Nchini Uganda: Mintarafu, Ueneaji wa Matumizi Yake Kwenye Asasi ya Uchapishaji. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 73-83. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.641