BC-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Recent Submissions
Item Usawiri Wa Waathiriwa wa Ghasia Za Kisiasa na Kijamii Katika Riwaya Teule za Kiswahili(Kenyatta University, 2023-11) Okora, Mogondo EricksonUtafiti huu ulichunguza usawiri wa waathiriwa wa ghasia za kisiasa na kijamii katika riwaya za Chozi la Heri (Matei, 2014) na Kufa Kuzikana (Walibora, 2003). Riwaya hizi ziliteuliwa kutumia mbinu ya usampulishaji nasibu kwani zinadhihirisha matukio na wahusika wa ghasia za kisiasa na kijamii na zilitosheleza mahitaji ya uhakiki huu. Lengo la kwanza la uhakiki huu lilikuwa kubainisha waathiriwa wa ghasia za kisiasa na kijamii katika riwaya teule. Lengo la pili lilikuwa kuchunguza namna waathiriwa wa ghasia za kisiasa na kijamii walivyosawiriwa katika riwaya teule. Lengo la tatu lilikuwa kutathmini maudhui yaliyokuzwa na kuendelezwa na wahusika wa ghasia za kisiasa na kijamii katika riwaya teule. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhalisia. Mihimili ya nadharia ya nadharia ya uhalisia ilifaa utafiti huu katika kukusanya, kuchanganua na kuwasilisha matokeo kulingana na malengo ya utafiti. Utafiti huu ulifanyika maktabani ambapo data ilikusanywa kupitia usomaji wa riwaya teule kisha kuchanganuliwa na kuwasilishwa kwa mtindo wa maelezo. Utafiti huu umegawika katika sura tano; sura ya kwanza inahusu utangulizi wa utafiti ambapo tuliangalia usuli wa mada, malengo ya utafiti, suala la utafiti, na maswali ya utafiti. Aidha sura hii ilionyesha upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusu mada, sababu za kuchagua mada, mbinu na nadharia ya utafiti. Sura ya pili inahusu ubainishaji wa wahusika wa ghasia za kisiasa na kijamii katika riwaya za Chozi la Heri na Kufa Kuzikana. Sura ya tatu ilichunguza namna wahusika wa ghasia za kisiasa na kijamii walivyosawiriwa katika riwaya teule. Sura ya nne inahusu kutathmini maudhui yaliyokuzwa na kuendelezwa na wahusika wa ghasia za kisiasa na kijamii katika riwaya teule. Sura ya tano inahusu muhtasari wa tasnifu nzima, matokeo, mapendekezo, mchango wa utafiti na changamoto za utafiti.Item Ukuzaji- na Maendeleo ya Kiswahili(RealText Printers and Pubishers, 2024) Mwita, Leonard Chacha; Ngugi, Pamela MuhadiaItem Mchango wa Viongozi wa Kenya Katika Kuimarisha Lugha ya Kiswahili(Taasisi Ya Taaluma za Kiswahili, 2018) Ngugi, Pamela M.Y.Item Mitaala ya Kiswahili Katlka Elimu na Utaifa: Nafasi ya Fasihi ya Watoto Katika Uendelezaji na Ulmarishaji wa Mshlkamano wa Kltaifa(Twaweza Communications, 2023) Ngugi, Pamela M.Y.Lengo mojawapo la elimu katika nchi ya Kenya ni kukuza utaifa, uzalendo na kuendeleza umoja wa taifa. Hivyo basi, elimu inayotolewa inahitaji kuziheshimu tamaduni mbalimbali zilizopo nchini na wakati uo huo, kuhakikisha kuwa haiendelezi ubaguzi katika jamii kwa misingi ya rangi, ukabila na dini. Ili kutekeleza lengo hili na malengo mengine, wasomi wengi wanaamini kuwa ufundishaji wa fasihi kwa jumla na hasa fasihi ya watoto unaweza kuchangia katika kuyafikia malengo . haya kwa kukuza hisia za kitaifa miongoni mwa wanafunzi. Ujenzi wa taifa ni juhudi za makusudi na za kujitolea. Tangu uhuru, wananchi wamekuwa wakitafuta njia za kuleta utangamano baina ya makabila na nchi mbalimbali za Afrika. Hatua mojawapo katika ujenzi wa taifa ni Uimarishaji wa utamaduni wa tamaduni mbalimbali. Utamaduni wowote ule utaeleweka vyema kwa kuchunguza mila na desturi zilipo katika jamii husika, pamoja na kufahamu namna kila jamii ilivyowasilisha amali zake mbalimbali kama vile, ukarimu, kujitolea, haki na maslahi ya pamoja, mambo ambayo yalichangia katika kuunda utaifa. Ufahamu wa amali hizi waweza kupatikana kupitia fasihi za jamii hizi. Fasihi ni matokeo ya shughuli za jamii; huibuka, hukua na kusambaa kutokana na mazingira yaliyopo katika jamii. Lengo la makala hii ni kubainisha nafasi ya fasihi ya watoto kama chombo cha kujenga mshikamano wa kitaifa sawia na mshikamano wa eneo la Afrika Mashariki na Bara la Afrika kwa ujumla.Item Magazeti kama Kichocheo cha Kuendeleza Fasihi ya Watoto na Vijana: Mfano kutoka Daily Nation Na TaifaLeo(Twaweza Communications, 2019) Ngugi, Pamela M.Y.Matumizi ya magezeti kama chombo cha kufunzia darasani ni jambo ambalo limepokelewa na wasomi wengi. Magazeti yanaweza kuiumika kama njia moja ya kujaliza na kutimiliza masomo mbalimbali ikiwemo fasihi ya watoto. Lengo la makala hii ni kubainisha mchango wa magazeii katika kuendeleza fasihi ya watoto na vijana. Mchango huu uiabainika kua kuchambua vitanzu mbalimbali vinavyojumuishwa kaiika magazeti haya na namna vinavyochangia kaiika. kuendeleza fasihi ya watoto.Item Hatua za Maendeleo Katika Tafiti Zilizofanywa Katika Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu Cha Kenyatta(Moi University Press, Moi University, Eldoret, 2019) Ngugi, Pamela MuhadiaMojawapo ya mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Ominde ya mwaka 1964 ilikuwa kuanzishwa kwa idara ya 1simu na lugha za Kiafrika katika Kitivo cha Sanaa katika Chuo Kikuu cha Nairobi mwaka 1969 ambapo somo la Kiswahili lingepewa kipaumbele. Baadaye, katika mwaka 1985, Chuo cha Kenyatta kiliJanywa Chuo Kikuu cha tatu ..Katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Idara ya Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika ilianzishwa mwaka wa 1987, ambapo mafundisho katika taaluma ya fasihi nafasihi hutolew. Vilevile tafiti katika maeneo mbalimbali ya lugha ya Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika na fasihi yake hutolewa. Jdara hii huendesha programu za uzamili na uzamifu. Matokeo yake, yamedhihirika kupitia kwa tafiti mbalimbali katika lugha ya Kiswahili. Lengo la sura hii ni kueleza na kutathmini mwelekeo ambao tafiti hizi zimechukuwa tangu kutambuliwa kwa lugha hii kama somo katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.Item Fasihi Yakiswahiliya Watoto: Maendeleo, Nadharia, Mbinu na Mifano: va Uchambuzi(Taasisi Ya Taaluma za Kiswahili, 2019) Ngugi, Pamela M.Y.; Lyimo, Edlth B; Bakize, Leoard H.Item Children Literature in Kiswahili: A Stylistic Approach(Logs Verlag Berlin, 2011) Ngugi, Pamela; Nabea, WendoSwahili children's literature in Kenya has seen tremendous developments in the recent past. The ambience in which this literature is produced and disseminated is usually characterised by a focus on content, particularly the theme. In essence, the literature has maintained a commitment to making young people aware of the topical debates taking place in the society, in particular; substance abuse, bullying, disability, children's rights, equal opportunities and injustices that are inherent in society. Style in children's literature receives little attention. However, style, thus the way in which things are represented, based on complex codes and conventions of language as well as presuppositions about language, is an important component of children's books (Stephen, 1992). A study of it allows us access to some of the key processes which shape text production. This essay explores style as used in selected Swahili storybooks for children, and shows how the literary elements make the language used in these books memorable. Within the language system of Swahili, it is possible for young readers to encounter in their reading an extensive range and variety of language issues. Some textual varieties such as lexicon and syntax will seem familiar and immediately accessible, since they can be appreciated as everyday language. However, other features will appear as less familiar, either because the lexicon contains forms or uses that are specific to a different speech community, or because writers may choose to employ linguistic forms whose occurrences are largely or wholly restricted to narrative fiction. As a result of differences in language use, books which may have a common theme or topic will differ just because the theme is expressed through differing linguistic resources. This means that writers have many options of styles to choose from. The study is guided by models of Manfred (2005), Rothlin (2001) and Lukens (2003), as they apply a structural approach which is one of the modern methods of literary study. We examine the novels in regard to discourse structure, point of view, register, and foregrounding. It also focuses on imaginary speech, presentation of speech, imagery, figurative language, hyperbole, allusion, use of proverbs and use of dreams.Item An Evaluation of Researches Done on African Languages at Kenyatta University(Kenyatta University, 2018) Ngugi, Pamela M.Y.; Wamalwa, StephenOne of the declarations that were passed and agreed upon during the first conference on African languages and literature that was held in Asmara, Eriteria in 2000, was the need to promote research on African languages. This was considered very vital for their development. In this article, we focus on the Language and Literature Departments at Kenyatta University by examining the researches that have been done on language and literature with the aim of showing how they have contributed to the documentation of African languages.Item Ukiushi kama Mbinu ya Kudhihirisha Itikadi ya Kuumeni katika Fasihi ya Kiswahili Mifano kutoka Riwaya za Said Ahmed Mohamed na Euphrase Kezilahabi”, in Kiswahili na Utaifa Nchini Kenya(Twaweza Communications, 2012) Osore, Miriam; Ryanga, CharlotteDhana ya ukiushi (defamiliarization) ina ma~na ya kudhihirisha kitu au hali kwa njia isiyokuwa ya kawaida, au isiyo dhahiri. Dhana hii hutumiwa kuele~a kijumla hali arnbapo kitu fulani hudhihirishwa kwa njia isiyo kuwa ya kawaida. Stacy (1977:178)anaeleza kwamba mbinu ya ukiushi inaweza kutumiwa kwa malengo mbalimbali; kama kuchekesha, kushangaza, kuhuzunisha, kukasirisha au kumfanyia mtu mzaha. 'Hata hivyo, mbinu hii imetumiwa kueleza uvumbuzi mpya arnbao umebadilisha maisha, na fikra za binadamu. Mbinu hii inapotumiwa katika fasihi huwa imetumiwa kimaksudi ili kudhihirisha jambo fulani. Mbinu ya ukiushi ina historia ndefu katika utunzi wa fasihi. Wananadharia na wanafasihi wamekiri, kwa mfano, kwamba mbinu ya ukiushi haiwezi kuepukika katika utunzi wa ushairi. Tangu awali, matumizi ya mbinu hii ya ukiushi yameelekea kusisitiza wazo kwamba, mbinu hii huturniwa kwa malengo mawili: kiujumi na kudhihirisha maana katika fasihi. George Steiner (1976:217~218),kwa mfano, anasema, "Lugha ndicho kifaa muhimu ambacho binadamu anaweza kutumia kukataa kuuona tilimwengu jinsi ulivyo". Anachosisitiza katika madai haya ni kwamba lugha hutumiwa kukiuka maana ya kawaida na kuvumbua njia mpya za kuuona ulimwengu. Dhana ya ukiushi katika fasihi iliasisiwa na mwanamaumbo mrusi Viktor Shklovsky ambaye aliunda dhana ya Kirusi 'Ostranenie' ambayo ilitafsiriwa ..katika Kiingereza kama "kueleza kwa njia ya ajabu" (making strange). Aliamini kwarnba jukumu la fasihi lilikuwa kueleza au kubainisha ulimwengu kwa njia isiyokuwa ya kawaida. Alikiri kwamba jukumu lafasihi KlSWAHILl NA UTAIFA NCHINI KENYA 121 I lilikuwa kuchochea hisia za msomaji. Kwake 'Ostranenie' ilijumlisha mbinu zote ambazo mwandishi wa fasihi anaweza kuturnia ili kubainisha kitu cha kawaida kwa njia ya kukifanya kieleweke kwa njia mpya. Kwa hivyo, alichukulia kwamba mbinu za ukiushi zililenga sio tu kudhihirisha maana, bali pia kutoa picha ya kipekee ya kile ambacho kilikuwa kikielezwa (Shklovsky 1965). Mbinu hizi zinapotumiwa katika fasihi, hutufanya kuona mambo kwa njia iliyo tofauti kabisa na jinsi tunavyoyajua. Mbinu za ukiushi ni muhimu kwa sababu msomaji wa fasihi huzitarnbua moja kwa moja anaposoma. Anapokutana na mbinu hizi, yeye hulazimishwa kuzifikiria na kisha kutambua ile maana mpya inayokusudiwa na mwandishi. Mbinu hizi ni nyingi na huweza kuwa za kitamathali kama vile jazanda, taswira, tashihisi, tashbihi na methali. Makala hii inafafanua jinsi Euphrase Kezilahabi na Said Ahmed Mohamed wanavyoshughulikia na kubainisha itikadi ya kuumeni (patriarchal ideology) kupitia mbinu za ukiushi. Watafiti wengi wameshughulikia mbinu mbalimbali za fasihi lakini si wengi ambao wamejaribu kuonyesha jinsi uhakiki wa mbinu za ukiushi unavyoweza kutumiwa kuelewa maana katika kazi za fasihi. Msimamo wetu ni kwamba mbinu za ukiushi ni muhimu katika utunzi wa fasihi na uchunguzi wa mbinu hizi unaweza kubainisha maudhui ya mwandishi kwa njia nzuri zaidi,Item Ufundishaji wa Taaluma ya Tafsiri katika Vyuo Vikuu Nchini Kenya in New Horizons in Pedagogy(Masinde Muliro University of Science and Technology, 2013) Osore, MiriamItem Ufundishaji wa Kiswahili katika Nchi za Kigeni: Mfano wa Chuo Kikuu cha Syracuse’, in Miaka Hamsini ya Kiswahili Nchini Kenya,(Twaweza Communications, 2014) Osore, Miriam; Midika, BrendaUfundishaji na ujifunzaji wa lugha za Kiafrika katika nchi za kigeni un historia ndefu. Kwa mujibu wa Moshi katika Bokamba (2000:uk 26-27 ufundishaji wa lugha za Kiafrika haukuanzia madarasani bali ulianzi nyanjani katika kame ya 15 ambapo wamishenari walitaka kujua zaic kuhusu lugha zajamii walizokuwa wakieneza injili.Walianza kwa kuandik makamusi na vitabu vya sarufi ambavyo viliwahamasisha wanaisimu kam vile Wilhelm Bleek ambaye alichapisha kitabu A Comparative Grammar ( African Languages. Miongoni mwa wanaisimu wengine ni kama [ame Frederick Schon na Carl Meinhof ambaye alichapisha kitabu cha fonoloji ya lugha za Kibantu na Johann Ludwig Krapf aliyechapisha kitabu ch kwanza cha sarufi ya Kiswahili. Mafunzo ya lugha zaKiafrika nchini Marekani yalianzishwa miaka y 1950,kama kipengele muhimu cha sheria ya Taifa,The National Defense A( ya 1958,Sheria hii .ilianzisha vituo vya mafunzo kuhusu Afrika. Mafunz haya yalihusisha hasa lugha na fasihi. Kuanzia wakati huo vyuo nchin Marekani vimekuwa vikifunza lugha zaKiafrikaikiwemolugha yaKiswahil Katika kuadhimisha miaka 50ya Kiswahili ni muhimu kutathmini namn taalurria ya ufundishaji wa Kiswahili katika nchini za Kigeni inavyoendele. na mchango wake katika maenezi ya Kiswahili kimataifa. Makala hay. yanalenga kufafanua ufundishaji wa lugha ya Kiswahili nchini Marekani Yanagusia mbinu za ufundishaji kama, matumizi ya teknolojia n, changamoto ambazo walimu Waafrika wanakumbana nazo katik, kufundisha wazungu Kiswahili hasa katika Chuo Kikuu cha Syracuse.Item Ufasiri katika Sekta ya Afya: Kituo cha Afya cha Mathare North, Kenya’ in Kiswahili, Utangamano na Maendeleo Endelevu Afrika Mashariki(KAKAMA, 2019) Osore, MiriamUfasiri ni shughuli isiyoweza kutenganishwa na matumizi ya lugha katika mazingira ya wingi lugha. Shughuli hizi zinahusisha kuhamisha ujumbe kutoka lugha moja hadi nyingine. Watu wengi wanaohitaji huduma ya afya nchini Kenya wan a kiwango cha chini cha uelewa wa lugha ya Kiingereza na hivyo basi wanahitaji ufasiri ili waweze kupata huduma kutoka vituo vya afya na hospitali. Mara nyingi wahudumu wa afya kama madaktari na wauguzi hujaribu kuwafasiria wagonjwa kutoka Kiingereza hadi Kiswahili au lugha za kwanza. Katika hali kama hizi inachukuliwa kwamba wahudumu hawa wana uwezo wa kutekeleza jukumu hili kwa sababu wanaweza kuzungumza lugha hizo. Kinyurne cha matarajio hayo, ufasiri ni taaluma inayomhitaji mtu kupata mafunzo rnaalumu. Uwezo wa kuzungumza lugha mbalimbali siyo kigezo pekee cha kumwezesha mtu kumudu stadi ya kufasiri. Vivyo hivyo, taaluma ya tiba inahitaji utaalamu wa hali ya juu. Kimsingi, kuhamisha ujumbe wa aina yoyote kutoka lugha moja hadi nyingine kwa kuzingatia umilisi wa lugha pekee ni jambo la kupotosha na kuhatarisha maisha ya wagonjwa. Kwa hivyo, ujuzi wa taaluma ya tiba pamoja na umilisi wa lugha ni mambo muhimu ya kuzingatia katika tafsiri ya sekta ya afya. chini Kenya hakuna wafasiri ambao wameajiriwa na serikali katika sekta ya afya. Makala hii inalenga kuchanganua na kutathmini jinsi fasiri inavyoendelezwa katika kituo cha afya cha Mathare North nchini Kenya. Kiwango cha mawasiliano na usahihi wa habari ' hospitalini kinachunguzwa.· Makala inapendekeza kwa .Kamisheni ya Afrika Mashariki (KAKAMA).kuwekwe mikakati ya kuunda sera ya kuhakikisha kwamba ufasiri katika sekta ya afya unafanywa na wataalamu wa afyaItem The Contribution of African Literature in the Preservation of Culture: The case of Kiswahili Literature’ in Isimu na Fasihi ya Lugha za Kiafrika(Moi University Press, 2018) Osore, MiriamThere is a symbiotic relationship between language, culture and literature. This is because each one of these aspects reinforces the other. Oral literature has served to enlighten, educate and portray the African world view, practices and problems. It was largely used to pass on African values and way of life from generation to generation. This significance of literature has not changed even with the coming of written literature and western education. African writings such as Achebe (1988), through using the English language, have weaved African culture through their creative writings. . \ Chinua Achebe, who is regarded by scholars as the father of African literature in English; declared that an African writer has a responsibility different from' that of his/her western counterparts. This is because African literature is different from other literatures since it has its own traditions, models and norms. Achebe (1988) further notes that Africari history and.culture imposes upon it preoccupation which at times are quite different from those of other literatures. Achebe's argues that, literature reflects the value system and exceptions of the society from which it springs. African culture is diverse and dynamic. It encompasses the totality of attitudes, behavior, beliefs and world view. According to Ameh (2002: 165), culture is that "complex pattern of behavior and material achievement which are produced, learned and shared by members of a community." Culture is therefore an integral part of human society 'and all human communities are characterized by it. This then means that, every human community has its unique cultural patterns. One of the main components of culture is the language through which it finds expression; thus there is no culture which does Hot have a linguistic basis. The totality of attitudes, behaviours, beliefs and world views find their expression through language. Literature on the other hand is defined as any piece of writing that expresses human experience and feelings through imagination. These writings become African due to the fact that they address aspects of African life, society, philosophy and experiences regardless of whatever language it iswritten in. This paper investigates aspects of African culture as presented by selected authors of Swahili texts. OJaide (1992) asserts that, there is no art for art's sake in Africa and that every literary work has a social significance. Achebe (1988:44); speaking about African literature, argues that his agenda .in writing is to help his society regain belief in itself and put away the complex of the years of degeneration and self-abasement. Achebe further categorically states that no African writer can be excused from the duty of educating through their writings. What Achebe seems to stress is that the foremost duty of an African creative writer is to teach African culture. In order for a writer to fulfill his mission, language is key. The African writer has to get his/her message across a wider readership but without losing the cultural aspect of the African people and their language. ~ 75 ~ lsimu na Fasihi ya Lugha za Kiafrika Whereas African writers writing in European languages have to contend with brewing old wine of African ideas and expressions in new bottles of English language (Achebe 1973), writers ir .Kiswahili, an African language do not face serious challenges in expressing African culture inar African language. African literature endeavors to describe the lives of traditional Africans African people are portrayed like other people of the world with their unique dreams, values customs and practices.Item Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kama nyenzo ya kukuza na kuendeleza Kiswahili’ in Lugha na Maswala Ibuka(Chama cha Kiswahili cha Taifa, 2018) Osore, MiriamMatumizi ya Kiswahili yametanuka kimaeneo kutoka pwani na maeneo ya Bara Hindi na kuendelea kutumika katika nchi nyingine barani Afrika na mabara mengineyo. Kiswahili sasa kinatumika katika nchi ya Kongo, Afrika Kusini, Rwanda, Burundi, Gabon, Marekani, Ujerumani, Bara la Ulaya, Uchina na kwingineko. Kiswahili kinatambulika miongoni mwa lugha kuu za kimataifa kama vile Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kihispaniola, na hata Kireno. Kati ya lugha za Kiafrika kama Hausa na Kilingala, Kiswahili ndiyo lugha ambayo imeenea kwa kasi na kuvuka mipaka ya bara la Afrika hadi kwingineko ulimwenguni. Awali, wamisionari walipofika Afrika Mashariki, walijifunza Kiswahili. Waliporejea kwao, walianzisha mafunzo ya Kiswahili kwa wale ambao walinuia kuzuru Afrika Mashariki kwa shughuli mbalimbali kama biashara, dini na utawala. Wataalamu wengi wa bara la Ulaya, walijitolea kufanya utafiti na kuandika vitabu kuhusu Kiswahili. Kwa mfano, Askofu Steere, Whiteley, Ashton na Krapf. Waliandika vitabu kama vile Handbook of Swahili Language (1870) cha Steere na Swahili Dictionary (1850) .cha Krapf. Uandishi wa vitabu hivi ni miongoni mwa hatua za mwanzo za kukiendeleza Kiswahili. Huko Marekani, Wamarekani wenye asili ya Kiafrika na Wazungu wamekuwa wakijifunza Kiswahili kama mojawapo ya masomo katika vyuo vikuu. Kwa Wamarekani weusi, hatua hii ni kama kielelezo cha urithi wa utamaduni wao. Barani Afrika, Kiswahili kinatumiwa kuleta utangamano kati ya jamii mbalimbali. 123 Kiswahili kimeteuliwa kama lugha mojawapo iliyo rasmi ya Umoja wa Afrika (VA). Lugha nyingine ni Kiingereza, Kifaransa, Kiispaniola, Kireno na Kiarabu. Aidha, Kiswahili ndiyo lugha rasmi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika. Katika kiwango hiki, Kiswahili ni lugha ya kimataifa. Kiswahili kimepanda hadi ngazi ya kimataifa kwa sababu mbalimbali. Kwa mujibu wa Mbaabu (1979) baadhi ya sababu hizo ni kwamba Kiswahili ni lugha ambayo haina mihemko ya kisiasa; inakubali mabadiliko ya istilahi mpya na unyambuaji wa maneno. Aidha, Kiswahili hakina vikwazo vya kimazingira; kina maandishi, historia na fasihi yake (Chiraghdin na Mnyampala, 1977).Item Utahini wa Kiswahili katika Vyuo Vikuu Nchini Kenya’, in Kiswahili katika Elimu ya Juu(University Press, 2019) Osore, Miriam; Mudhune, EverlineMakala haya yanahusu utahini wa Kiswahili katika Vyuo Vikuu mbalimbali nchini Kenya. Utahini hulenga kubainisha ikiwa mwanafunzi anaweza kukumbuka aliyofundishwa darasani kwa njia ya mtihani. Hivyo basi katika kila somo, mhadhiri hutunga maswali mbalimbali ambayo yatajibiwa na mwanafunzi. Maswali husika yanaweza kulenga ufahamu, ufafanuzi, uchanganuzi, utathmini n.k.Item Riwaya za Kiswahili na Suala la Jinsia: Mfano wa Riwaya za Said Ahmed Mohamed na Euphrase Kezilahabi’, in Kiswahili na Maendeleo ya Jamii(Chama cha Kiswahili cha Afrika Mashariki (CHAKAMA), 2015) Osore, MiriamMakala haya yanaangalia suala la jinsia katika riwaya za Said Ahmed Mohamed: Utengano (1980) na Asali Chungu(1977) na za Euphrase Kezilahabi: Rosa Mistika (1971), Kichwa-Maji(1974) na Gamba fa Nyoka (1978). Msimamo wa makala haya ni kwamba, ili kuhakiki suala la jinsia katika riwaya teule kikamilifu, lazima liangaliwe katika misingi ya utamaduni wa Kiafrika. Makala haya yanachukulia kazi ya fasihi kuwa zao la kijamii na lazima ihakikiwe katika misingi namiktadha ya jamii inayohusika. Kwa hivyo, katika kutalii jinsi suala la jinsia lilivyoshughulikiwa na waandis~i hawa, tunatambua umuhimu wa matukio ya kijamii. Msimamo wa makala haya ni kwambamwandishi wa fasihi hueleza hisia na itikadi zake za kibinafsi na falsafa za jamii yake katika fasihi anayoitunga. Katika misingi hiyo, nadharia iliyotumika ni ya uchanganuzi usemi (Critical Discourse Analysis- CDA). Nadharia hii ina waasisi wengi wakiwemo Fowler (1975), (1991), Fairclough (1992), (1995), Van Dijk (1977); (1981) na Wodak (1989). Wote wanasisitiza kwamba matumizi yoyote ya lugha ni kitendoau usemi wa kijamii. Wodak na Meyer (2001) wanaeleza kwamba CDA ni nadharia ya kisasa ambayo haitoi masuluhisho maalum ya masuala yanayomkumba binadamu. Inachukulia kuwa uhakiki wowote na matokeo yake yachukuliwe tu kamajinsi mojawapo ya kuelewa suala fulani. Inalenga kutoa mitazamo mbalimbali ya masuala yanayohusu jamii. Nadharia hii inapendekeza kuwa matumizi ·yote ya lugha ni tukio la kijamii. Katika uhakiki, mhakiki huchanganua miundo yamakala kwa kurejelea sifa zake za kiisimu pamoja na vipengele vya kijamii na vya kitamaduni. Inashikilia kwamba maana kamili ya makala hudhihirika kupitia ushirikiano baina ya vipengele hivi. Inasisitiza kwamba uhusiano baina ya wanajamii huathiri na kudhihirika kupitia kwajinsi wanajamii hawa wanavyozungumza baina yao na kujieleza. Kiujumla makala haya yanashikilia kwamba matumizi yoyote ya lugha yanaelekezwa katika misingi na mipaka ya mfumo wa kijamii na kitamaduni. Ili kupata ujumbe wa Mohamed na Kezilahabi kuhusu suala la jinsia kupitia matumizi yao ya lugha, tunazingatia·mfumo mzima wa kijamii na kitamaduni. Kwa hiyo katika uhakiki wetu, tunajaribu kuonesha uhusiano baina ya usawiri wa suala la j insia katika riwaya teule .na muktadha wa kitamaduni na mifumo ya kiitikadi.Item Mchango wa Tafsiri na Ukalimani katika Utekelezaji wa Katiba ya Kenya, 2010’ in Uwezeshwaji wa Kiswahili kama Wenzo wa Maarifa(Moi University Press, 2019) Osore, MiriamNchi zilizotawaliwa na mataifa ya kimagharibi hujikuta katika hali ya wingi lugha. Kwa mujibu wa Mbaabu (1996), kufikia mwishoni mwa Kame ya 19 bara la Afrika lilishuhudia unyakuzi ulioendelezwa na mataifa ya kimagharibi yaliyokuwa na uwezo mkubwa. Bara la Afrika liligawanywa na kuwekewa mipaka katika kongamano la Berlin la Disemba 1884 hadi Januari 1885. Afrika iligawanyiwa mataifa ya Uingereza, Ufaransa, Udachi, Ujerumani, Ubelgiji, Uhispania, Itali na Ureno (Mbaabu 1996). Kabla ya tukio hili la kikoloni kila kabila lilikuwa na mipaka na utaifa wake. Makabila yalizungumza lugha zao ambazo ziliyabainisha na kuyatofautisha na makabila mengine yaliyopakana nayo. Ijapokuwa kila kabila lilijisimamia kiutawala 'jamii hizi ziliendesha biashara na makabila mengine jirani. Katika eneo Ia Afrika. Mashariki, Kiswahili kilitumika kama 'Lingua Franca' kati ya makabila haya hata kabla ya ukoloni wa kimagharibi. Mbaabu (1996) anasema kwamba kirpitia biashara za waturnwa na pembe za ndovu, Kiswahili kilienea kutoka mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki hadi maeneo ya ndani mwa Tanganyika, Kenya na Uganda. Anaendelea kusema kwamba hata kabla ya biashara hii Waswahili walikuwa wanajua kusoma na kuandika na Kiswahili kilikuwa kimeandikwa tayari, katika hati za kiarabu. Kiswahili basi kilikuwa kimeenea eneo kubwa wakoloni walipofika Afrika ya Mashariki. . . Kutokana na maenezi ya Kiswahili, wamishenari waliofika Afrika Mashariki kama Dkt. Krapf, John Rebmann, David Livingstone na wageni kama Sir Henry Morton Stanley waliwajibika kujifunza Kiswahili ili kuweza' kuwasiliana na wenyeji. Vilevile, wakoloni walipofika walitambua Kiswahili na kuanza kukitumia katika elimu na shughuli zao za utawala. Baadaye, wakati wa uhuru, Kiswahili kiliteutiwa kama lugha ya taifa ya kuwaunganisha Wakenya wote. Kupitia Ripoti ya Elimu ya Mackay ya mwaka wa 1984, Kiswahili kilipendekezwa kufundishwa kama somo la lazima kutoka shule ya msingi hadi sekondari. Utekelezaji wa ripoti hiyo ulifanyika mwaka wa 1985 kupitiamfumo mpya wa elimu wa 8-4-4. Kwa miaka yote hadi 2010 Kiswahili kimekuwa S01110 la lazima shuleni huku kikichukua nafasi ya lugha ya taifa. Kama ilivyotajwa hapo juu, kupitia katiba ya Kenya ya 2010, Kiswahili kinatambulika kama mojawapo ya lugha rasmi nchini Kenya kupitia kwa Sura ya Pili Ibara ya Saba. Hali hii inaungwa mkono na vipengele vingine katika katiba hiyo. Katika kipengele cha I na 2 cha sura hiyo, katiba inasisitiza kwamba serikali inajukumu la kuimarisha na kuendeleza lugha rasmi na za kikenya. Aidha katika Sura ya 8 Ibara ya 120, katiba inasema kwamba lugha rasmi za bunge la Uwezeshwaji wa Kiswahili kama Wen::o wa Maarifa Kenya ni Kiswahili na Kiingereza na lugha ya ishara ya Kenya. Nayo Sura ya 4 Ibara ya 44 inasisitiza kwamba kila raia wa Kenya ana haki ya kutumia lugha anayotaka na kushiriki katika shughuli za kitamaduni anazotaka. Vipengele vingine katika Katiba vinavyohusiana na lugha ni Sura ya 33 kipengele cha ) ambacho kinahimiza uhuru wa Mkenya kujieleza huku Sura ya 4, Ibara ya 35 ikilenga haki ya mwananchi kupata taarifa. Haki ya kusikizwa mahakamani inasisitizwa katika sura ya 4, ibara ya 50 vipengele hivi vyote vya Katiba vinaonyesha umuhimu wa kuendeleza matumizi ya Kiswahii na Kiingereza katika shughuli zote za serikali ili kuhakikisha kwamba mwananchi anahudumiwa na kuelezwa kinachoendelea katika nchi yake kupitia lugha anayofahamu vizuri. Kwa vile kwa miaka mingi Kiingereza kimekuwa lugha rasmi, tafsiri na ukalimani ndizo taaluma zitakazohitajika kwa kiwango kikubwa katika utekelezaji wa katiba hiyo. Kabla ya kuangazia jinsi hili litafanyika ni muhimu kutambua kwamba uteuzi wa lugha rasmi nchini ni mchakato unaofuata hatua mahsusi za upangaji wa lughaItem Maisha: Kitendawili na Johari” in Daisaku Ikeda and Africa(Nairobi University Press,, 2001) Osore, Miriam; Ngugi, PamelaThis chapter examines Daisaku Ikeda's Maisha: Kitendawili na Johari translated into Kiswahili from Life: An Enigma, A Precious Jewel. It focuses on the contribution of the translated text on the subject of life and death. Our main objective is to highlight the.relevance of Ikeda's work to the Kiswahili audience in East and Central Africa. But first we look at the meaning of translation. _"oc According to th~ Internatil!nal Encyclopaedia of Linguistics Vol. 4 (1992), the word translation refers to the transfer of a written message from a source language to a target language. We can therefore say that translation is a process of substituting a text in one language for a text,in another language. At another level, translation could be regarded as communication; thus, it is intended to communicate some information to a given audience. This 97 Maisha Kitendawili na Joha,; implies, therefore, that in order for a translation to be done, there must be a need for doing it. It is in this regard that Maisha: Kitendawili na Johari is timely. Translation is an activity of enormous importance in the modem world. A lot has been translated into the various languages of the world. Research findings, in different fields have been disseminated through translation in different languages of the world. In the nineteenth century, Christian missionaries translated very many books including the Bible into Kiswahili and other languages in Kenya and East Africa. During the colonial period, a lot of literary works from Europe and Asia were translated into Kiswahili. After independence, the Africans, themselves were at the forefront in translating some of the great-literary works of the world into Kiswahili. For example, two of Shakespeare's plays, The Merchant of Venice as Mabepari wa Venisi and Julius Caesar as Julias Kaizari, were translated by Julius Nyerere.Maisha: Kitendawili na Johari by Daisaku Ikeda is an important addition to the 'other, translations that we have in the Kiswahili language. In Maisha: Kitendawili na Johari, Daisaku Ikeda has addressed very salient issues which are relevant to the human race all over the world.Item Jua Linapotua na Hadithi Nyingine(Longhorn, 2011) Osore, MiriamVita vya Kukata Masikio Moses Isegawa alizaliwa Uganda mnamo mwaka. wa 1965, Sehemu kubwa ya maisha yake ya ujana aliishi Uholanzi (Netherlands) ambapo alikuza kipawa chake kama mwandishi na akatia fora katika uandishi wa fasihi. Lakini alitambua kwamba kiini cha msukumo wake kilikuwa jamii yake na kwa sababu hii, alirejea nyumbani kutangamana nao. Baadhi ya kazi zake zilizochapishwa ni riwaya za Abyssinia Chronicles na Snakepit. Almasi Anita Desai alizaliwa Mussoorie, sehemu ya milima iliyo Kaskazini mwa Delhi, mwaka wa 1937. Alianza kuandika katika Kiingereza akiwa na umri wa miaka saba. Hadithi yake ya mwanzo ilichapishwa akiwa na umri wa miaka tisa. Desai alisornea katika chuo kikuu cha Delhi ambapo a1ipata shahada yake ya BA katika fasihi ya Kiingereza. Riwaya yake ya kwanza, The Peacock ilichapishwa mwaka wa 1963, ikifuatiwa na Voices of the City (1965). A1ipata tuzo ya Guardian kutokana na kitabu chake cha The Village by the Sea. ambacho ni uandishi wa kubuni wa kazi za watoto. Katika mwaka wa 1978 alipata tuzo ya National Academy of Letters kutokana n~ uandishi wa Fire on the Mountain. Kwa sasa ni mwanachama msomi wa The Royal Society of Literature. kule London. Mtaa wa Sandra Michaeal Anthony, mwandishi mashuhuri nl;l mwanahistoria, kutoka visiwa vya Caribbean, alizaliwa Mayaro, Trinidad na Tobago mnamo mwaka wa 1930. Mashairi yake ya kwanza yalichapishwa katika gazeti la Trinidad Guardian mnamo mwaka wa 1953. Mwandishi huyu alichapisha kitabu chake cha kwanza, The Games were Coming ambacho kilisifiwa sana na wahakiki na baadaye akachapisha riwaya, The Year in San Fernando. Anthony ameandika zaidi ya vitabu ishirini katika taaluma yake ya miongo minne. Hadithi hiiya Mtaa WGSandra inapatikana katika mkusanyo wa hadithi fupi unaoitwa: Cricket in the Road and Other Stories.
- «
- 1 (current)
- 2
- 3
- »