Ufasiri katika Sekta ya Afya: Kituo cha Afya cha Mathare North, Kenya’ in Kiswahili, Utangamano na Maendeleo Endelevu Afrika Mashariki

Loading...
Thumbnail Image
Date
2019
Authors
Osore, Miriam
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
KAKAMA
Abstract
Ufasiri ni shughuli isiyoweza kutenganishwa na matumizi ya lugha katika mazingira ya wingi lugha. Shughuli hizi zinahusisha kuhamisha ujumbe kutoka lugha moja hadi nyingine. Watu wengi wanaohitaji huduma ya afya nchini Kenya wan a kiwango cha chini cha uelewa wa lugha ya Kiingereza na hivyo basi wanahitaji ufasiri ili waweze kupata huduma kutoka vituo vya afya na hospitali. Mara nyingi wahudumu wa afya kama madaktari na wauguzi hujaribu kuwafasiria wagonjwa kutoka Kiingereza hadi Kiswahili au lugha za kwanza. Katika hali kama hizi inachukuliwa kwamba wahudumu hawa wana uwezo wa kutekeleza jukumu hili kwa sababu wanaweza kuzungumza lugha hizo. Kinyurne cha matarajio hayo, ufasiri ni taaluma inayomhitaji mtu kupata mafunzo rnaalumu. Uwezo wa kuzungumza lugha mbalimbali siyo kigezo pekee cha kumwezesha mtu kumudu stadi ya kufasiri. Vivyo hivyo, taaluma ya tiba inahitaji utaalamu wa hali ya juu. Kimsingi, kuhamisha ujumbe wa aina yoyote kutoka lugha moja hadi nyingine kwa kuzingatia umilisi wa lugha pekee ni jambo la kupotosha na kuhatarisha maisha ya wagonjwa. Kwa hivyo, ujuzi wa taaluma ya tiba pamoja na umilisi wa lugha ni mambo muhimu ya kuzingatia katika tafsiri ya sekta ya afya. chini Kenya hakuna wafasiri ambao wameajiriwa na serikali katika sekta ya afya. Makala hii inalenga kuchanganua na kutathmini jinsi fasiri inavyoendelezwa katika kituo cha afya cha Mathare North nchini Kenya. Kiwango cha mawasiliano na usahihi wa habari ' hospitalini kinachunguzwa.· Makala inapendekeza kwa .Kamisheni ya Afrika Mashariki (KAKAMA).kuwekwe mikakati ya kuunda sera ya kuhakikisha kwamba ufasiri katika sekta ya afya unafanywa na wataalamu wa afya
Description
Book Chapter
Keywords
Citation
Miriam Osore (2019): ‘Ufasiri katika Sekta ya Afya: Kituo cha Afya cha Mathare North, Kenya’ in Kiswahili, Utangamano na Maendeleo Endelevu Afrika Mashariki edited by Walibora, K. W., Kipacha A. H., na Simala, K. I. Zanzibar, KAKAMA pp 198 – 215.