Mitaala ya Kiswahili Katlka Elimu na Utaifa: Nafasi ya Fasihi ya Watoto Katika Uendelezaji na Ulmarishaji wa Mshlkamano wa Kltaifa
Loading...
Date
2023
Authors
Ngugi, Pamela M.Y.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Twaweza Communications
Abstract
Lengo mojawapo la elimu katika nchi ya Kenya ni kukuza utaifa,
uzalendo na kuendeleza umoja wa taifa. Hivyo basi, elimu inayotolewa
inahitaji kuziheshimu tamaduni mbalimbali zilizopo nchini na wakati
uo huo, kuhakikisha kuwa haiendelezi ubaguzi katika jamii kwa misingi
ya rangi, ukabila na dini. Ili kutekeleza lengo hili na malengo mengine,
wasomi wengi wanaamini kuwa ufundishaji wa fasihi kwa jumla na
hasa fasihi ya watoto unaweza kuchangia katika kuyafikia malengo
. haya kwa kukuza hisia za kitaifa miongoni mwa wanafunzi. Ujenzi wa
taifa ni juhudi za makusudi na za kujitolea. Tangu uhuru, wananchi
wamekuwa wakitafuta njia za kuleta utangamano baina ya makabila na
nchi mbalimbali za Afrika. Hatua mojawapo katika ujenzi wa taifa ni
Uimarishaji wa utamaduni wa tamaduni mbalimbali. Utamaduni wowote
ule utaeleweka vyema kwa kuchunguza mila na desturi zilipo katika jamii
husika, pamoja na kufahamu namna kila jamii ilivyowasilisha amali zake
mbalimbali kama vile, ukarimu, kujitolea, haki na maslahi ya pamoja,
mambo ambayo yalichangia katika kuunda utaifa. Ufahamu wa amali
hizi waweza kupatikana kupitia fasihi za jamii hizi. Fasihi ni matokeo ya
shughuli za jamii; huibuka, hukua na kusambaa kutokana na mazingira
yaliyopo katika jamii. Lengo la makala hii ni kubainisha nafasi ya fasihi
ya watoto kama chombo cha kujenga mshikamano wa kitaifa sawia na
mshikamano wa eneo la Afrika Mashariki na Bara la Afrika kwa ujumla.
Description
Book Chapter