Hatua za Maendeleo Katika Tafiti Zilizofanywa Katika Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu Cha Kenyatta

Loading...
Thumbnail Image
Date
2019
Authors
Ngugi, Pamela Muhadia
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Moi University Press, Moi University, Eldoret
Abstract
Mojawapo ya mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Ominde ya mwaka 1964 ilikuwa kuanzishwa kwa idara ya 1simu na lugha za Kiafrika katika Kitivo cha Sanaa katika Chuo Kikuu cha Nairobi mwaka 1969 ambapo somo la Kiswahili lingepewa kipaumbele. Baadaye, katika mwaka 1985, Chuo cha Kenyatta kiliJanywa Chuo Kikuu cha tatu ..Katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Idara ya Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika ilianzishwa mwaka wa 1987, ambapo mafundisho katika taaluma ya fasihi nafasihi hutolew. Vilevile tafiti katika maeneo mbalimbali ya lugha ya Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika na fasihi yake hutolewa. Jdara hii huendesha programu za uzamili na uzamifu. Matokeo yake, yamedhihirika kupitia kwa tafiti mbalimbali katika lugha ya Kiswahili. Lengo la sura hii ni kueleza na kutathmini mwelekeo ambao tafiti hizi zimechukuwa tangu kutambuliwa kwa lugha hii kama somo katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Description
Book Chapter
Keywords
Citation