Mchango wa Tafsiri na Ukalimani katika Utekelezaji wa Katiba ya Kenya, 2010’ in Uwezeshwaji wa Kiswahili kama Wenzo wa Maarifa
Loading...
Date
2019
Authors
Osore, Miriam
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Moi University Press
Abstract
Nchi zilizotawaliwa na mataifa ya kimagharibi hujikuta katika hali ya wingi lugha. Kwa mujibu wa Mbaabu (1996), kufikia mwishoni mwa Kame ya 19 bara la Afrika lilishuhudia unyakuzi ulioendelezwa na mataifa ya kimagharibi yaliyokuwa na uwezo mkubwa. Bara la Afrika liligawanywa na kuwekewa mipaka katika kongamano la Berlin la Disemba 1884 hadi Januari 1885. Afrika iligawanyiwa mataifa ya Uingereza, Ufaransa, Udachi, Ujerumani, Ubelgiji, Uhispania, Itali na Ureno (Mbaabu 1996). Kabla ya tukio hili la kikoloni kila kabila lilikuwa na mipaka na utaifa wake. Makabila yalizungumza lugha zao ambazo ziliyabainisha na kuyatofautisha na makabila mengine yaliyopakana nayo. Ijapokuwa kila kabila lilijisimamia kiutawala 'jamii hizi ziliendesha biashara na makabila mengine jirani. Katika eneo Ia Afrika. Mashariki, Kiswahili kilitumika kama 'Lingua Franca' kati ya makabila haya hata kabla ya ukoloni wa kimagharibi.
Mbaabu (1996) anasema kwamba kirpitia biashara za waturnwa na pembe za ndovu, Kiswahili kilienea kutoka mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki hadi maeneo ya ndani mwa Tanganyika, Kenya na Uganda. Anaendelea kusema kwamba hata kabla ya biashara hii Waswahili walikuwa wanajua kusoma na kuandika na Kiswahili kilikuwa kimeandikwa tayari, katika hati za kiarabu. Kiswahili basi kilikuwa kimeenea eneo kubwa wakoloni walipofika Afrika ya Mashariki. . .
Kutokana na maenezi ya Kiswahili, wamishenari waliofika Afrika Mashariki kama Dkt. Krapf, John Rebmann, David Livingstone na wageni kama Sir Henry Morton Stanley waliwajibika kujifunza Kiswahili ili kuweza' kuwasiliana na wenyeji. Vilevile, wakoloni walipofika walitambua Kiswahili na kuanza kukitumia katika elimu na shughuli zao za utawala. Baadaye, wakati wa uhuru, Kiswahili kiliteutiwa kama lugha ya taifa ya kuwaunganisha Wakenya wote. Kupitia Ripoti ya Elimu ya Mackay ya mwaka wa 1984, Kiswahili kilipendekezwa kufundishwa kama somo la lazima kutoka shule ya msingi hadi sekondari. Utekelezaji wa ripoti hiyo ulifanyika mwaka wa 1985 kupitiamfumo mpya wa elimu wa 8-4-4. Kwa miaka yote hadi 2010 Kiswahili kimekuwa S01110 la lazima shuleni huku kikichukua nafasi ya lugha ya taifa.
Kama ilivyotajwa hapo juu, kupitia katiba ya Kenya ya 2010, Kiswahili kinatambulika kama mojawapo ya lugha rasmi nchini Kenya kupitia kwa Sura ya Pili Ibara ya Saba. Hali hii inaungwa mkono na vipengele vingine katika katiba hiyo. Katika kipengele cha I na 2 cha sura hiyo, katiba inasisitiza kwamba serikali inajukumu la kuimarisha na kuendeleza lugha rasmi na za kikenya. Aidha katika Sura ya 8 Ibara ya 120, katiba inasema kwamba lugha rasmi za bunge la
Uwezeshwaji wa Kiswahili kama Wen::o wa Maarifa
Kenya ni Kiswahili na Kiingereza na lugha ya ishara ya Kenya. Nayo Sura ya 4 Ibara ya 44 inasisitiza kwamba kila raia wa Kenya ana haki ya kutumia lugha anayotaka na kushiriki katika shughuli za kitamaduni anazotaka. Vipengele vingine katika Katiba vinavyohusiana na lugha ni Sura ya 33 kipengele cha ) ambacho kinahimiza uhuru wa Mkenya kujieleza huku Sura ya 4, Ibara ya 35 ikilenga haki ya mwananchi kupata taarifa. Haki ya kusikizwa mahakamani inasisitizwa katika sura ya 4, ibara ya 50 vipengele hivi vyote vya Katiba vinaonyesha umuhimu wa kuendeleza matumizi ya Kiswahii na Kiingereza katika shughuli zote za serikali ili kuhakikisha kwamba mwananchi anahudumiwa na kuelezwa kinachoendelea katika nchi yake kupitia lugha anayofahamu vizuri. Kwa vile kwa miaka mingi Kiingereza kimekuwa lugha rasmi, tafsiri na ukalimani ndizo taaluma zitakazohitajika kwa kiwango kikubwa katika utekelezaji wa katiba hiyo. Kabla ya kuangazia jinsi hili litafanyika ni muhimu kutambua kwamba uteuzi wa lugha rasmi nchini ni mchakato unaofuata hatua mahsusi za upangaji wa lugha
Description
Book Chapter
Keywords
Citation
Miriam Osore (2019): ‘Mchango wa Tafsiri na Ukalimani katika Utekelezaji wa Katiba ya Kenya, 2010’ in Uwezeshwaji wa Kiswahili kama Wenzo wa Maarifa edited by Kobia, J. M., Kandagor, M., Mwita, L. M., Maitaria J. N., and Simwa, S.P.W. Eldoret, Moi University Press. pp. 61-67