Athari ya Mazingira Asilia ya Mtunzi katika Matumizi ya Kujibadilisha Kimazingaombwe: Uchunguzi wa Riwaya Teule za S. Robert na E. Kezilahabi
Loading...
Date
2022-08
Authors
Maggati, Charles N.
Osore, Miriam
Wafula, Richard
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
AJOL
Abstract
Makala haya yalikusudia kuchunguza athari ya mazingira asilia ya mtunzi
katika matumizi ya kujibadilisha kimazingaombwe. Ili kulifikia lengo hilo,
makala yameangazia jinsi mazingira asilia ya watunzi wawili yaani, Shaaban
Robert na Euphrase Kezilahabi yalivyoathiri suala la matumizi ya mbinu ya
kujibadilisha kimazingaombwe. Kazi za Shaaban Robert zilizoteuliwa ni
riwaya za Adili na Nduguze (1952) na Kufikirika (1946) na kazi za Euphrase
Kezilahabi zilijumuisha riwaya za Nagona (1990) na Mzingile (1991).
Kujibadilisha kimazingaombwe ni mbinu ya kisanaa inayoonekana kuwa
mashuhuri katika kazi za kifasihi za mihula mbalimbali. Mathalani, mbinu hii
inapatikana siyo tu katika kazi za kifasihi zilizojitokeza katika kipindi cha
usasabaadaye, bali pia mbinu hii inaonekana hata kwenye kazi za kale zaidi,
hususani kipindi cha kabla ya usasabaadaye. Kutokana na usuli huo, riwaya
za Shaaban Robert zilizoteuliwa zimewakilisha kipindi kabla ya
usasabaadaye ilhali riwaya za Kezilahabi ni za kipindi cha usasa na
usasabaadaye. Tumechagua riwaya zilizoandikwa katika vipindi hivyo tofauti
ili kuthibitisha kuwa mbinu ya kujibadilisha kimazingaombwe ni ya kale,
ilikuwako hata kabla ya kipindi cha usasabaadaye. Matokeo yanaonesha
kwamba tafsiri ya dhana au wazo katika kazi ya kifasihi imefungamana mno
na muktadha wa kijamii uliozaa kazi hiyo. Kutokana na athari ya muktadha
wa kijamii, dhana, wazo, suala au tukio fulani linaweza kuonekana la
kimazingaombwe katika kazi ya kipindi fulani ilhali dhana, wazo, suala au
tukio hilohilo linaweza kuonekana kuwa la kawaida (lisilo la
kimazingaombwe). Mabadiliko hayo yanaweza kusababishwa na maendeleo
ya sayansi na teknolojia au na maingiliano ya jamii kiutamaduni na
kiimani. Kwa kuongozwa na mtazamo huu, kujibadilisha kimazingaombwe kumebainishwa katika riwaya teule na kisha
imeelezwa jinsi ujitokezaji wa mbinu hii ulivyofungamana na uhalisia
wa maisha ya wanajamii kadiri ya mazingira asilia yaliyowazaa,
kuwalea na kuwakuza watunzi wa riwaya teule.
Description
Article
Keywords
Citation
Maggati, C. N., Osore, M., & Wafula, R. (2022). Athari ya Mazingira Asilia ya Mtunzi katika Matumizi ya Kujibadilisha Kimazingaombwe: Uchunguzi wa Riwaya Teule za S. Robert na E. Kezilahabi. Mulika Journal, 40(2).