Fasihi ya Watoto katika Ufundishaji wa Kiswahili katika Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki
Loading...
Date
2019
Authors
Ngugi, Pamela
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
KAKAMA
Abstract
Utafiti uliofanywa na shirika la Uwezo - Kenya kuanzia mwaka wa 2014 hadi 2016 kuhusu "Are our Children
Reading?" umethibitisha kuwa watoto wengi hasa katika shule za msingi hawajui kusoma na kuandika kwa mujibu wa
viwango vya madarasa waliyomo. Kwa sababu hiyo, shirika hili limependekeza mabadiliko katika ufundishaji na
kupendekeza kuturnika kwa mkabala jumuishi wa elimu iwapo sekta ya elimu inatarajia kupata maendeleo thabiti. Mkabala
jumuishi huhimiza wanafunzi kushiriki katika ujifunzaji wao na hivyo basi, kusaidia katika ukuzaji wa maarifa ya kufikiria
kwa kiwango kikubwa. Katika kufanya hivi, ujifunzaji huwa wa maana kwa mwanafunzi na huchangia katika kujenga stadi
nne za lugha ambazo ni: kusikiliza, kuongea, kusoma na kuandika, kusikiliza na kuongea kwa kiwango cha juu.
Lengo la makala hii ni kujadili na kubainisha namna ambavyo fasihi ya watoto inaweza kutumika kama kichocheo
cha kujua kusoma na kuandika, hasa pale ambapo wanafunzi wanapewa nafasi ya kujenga maana kutokana na usomaji wao.
Fasihi ya watoto inaweza kuchangia katika kuinua maarifa, stadi na milelekeo chanya miongoni mwa wanafunzi
kuhusiana na masuala ya kusoma na kuandika hali ambayo itachangia katika kufikia lengo la 4 la Malengo ya Maendeleo
Endelevu katika sekta ya elimu kuhusiana na kuhakikisha Mitaala ya Kiswahili katika Vyuo Vikuu rya Afrika Mashariki I 212
kuwa watoto wanapata elimu bora na yenye usawa kwa wote na kutoa furs a kwa wote kujiendeleza (UN, 2015) katika
Jumuiya ya Afrika Mashariki. Fasihi ya Watoto katika Elimu
Description
Book Chapter