Fasihi ya Watoto katika Ufundishaji wa Kiswahili katika Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki
dc.contributor.author | Ngugi, Pamela | |
dc.date.accessioned | 2024-02-09T07:44:49Z | |
dc.date.available | 2024-02-09T07:44:49Z | |
dc.date.issued | 2019 | |
dc.description | Book Chapter | en_US |
dc.description.abstract | Utafiti uliofanywa na shirika la Uwezo - Kenya kuanzia mwaka wa 2014 hadi 2016 kuhusu "Are our Children Reading?" umethibitisha kuwa watoto wengi hasa katika shule za msingi hawajui kusoma na kuandika kwa mujibu wa viwango vya madarasa waliyomo. Kwa sababu hiyo, shirika hili limependekeza mabadiliko katika ufundishaji na kupendekeza kuturnika kwa mkabala jumuishi wa elimu iwapo sekta ya elimu inatarajia kupata maendeleo thabiti. Mkabala jumuishi huhimiza wanafunzi kushiriki katika ujifunzaji wao na hivyo basi, kusaidia katika ukuzaji wa maarifa ya kufikiria kwa kiwango kikubwa. Katika kufanya hivi, ujifunzaji huwa wa maana kwa mwanafunzi na huchangia katika kujenga stadi nne za lugha ambazo ni: kusikiliza, kuongea, kusoma na kuandika, kusikiliza na kuongea kwa kiwango cha juu. Lengo la makala hii ni kujadili na kubainisha namna ambavyo fasihi ya watoto inaweza kutumika kama kichocheo cha kujua kusoma na kuandika, hasa pale ambapo wanafunzi wanapewa nafasi ya kujenga maana kutokana na usomaji wao. Fasihi ya watoto inaweza kuchangia katika kuinua maarifa, stadi na milelekeo chanya miongoni mwa wanafunzi kuhusiana na masuala ya kusoma na kuandika hali ambayo itachangia katika kufikia lengo la 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu katika sekta ya elimu kuhusiana na kuhakikisha Mitaala ya Kiswahili katika Vyuo Vikuu rya Afrika Mashariki I 212 kuwa watoto wanapata elimu bora na yenye usawa kwa wote na kutoa furs a kwa wote kujiendeleza (UN, 2015) katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Fasihi ya Watoto katika Elimu | en_US |
dc.identifier.isbn | 9789976516500 | |
dc.identifier.uri | https://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/27617 | |
dc.language.iso | en | en_US |
dc.publisher | KAKAMA | en_US |
dc.title | Fasihi ya Watoto katika Ufundishaji wa Kiswahili katika Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki | en_US |
dc.type | Book chapter | en_US |
Files
Original bundle
1 - 1 of 1
Loading...
- Name:
- Fasihi ya Watoto katika Ufundishaji wa Kiswahili katika Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki.pdf
- Size:
- 11.05 MB
- Format:
- Adobe Portable Document Format
- Description:
- Full text book chapter
License bundle
1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
- Name:
- license.txt
- Size:
- 1.71 KB
- Format:
- Item-specific license agreed upon to submission
- Description: