Mikakati ya Uchambuzi wa Fasihi ya Watoto: Mtazamo wa Upokezi wa Msomaji
Loading...
Date
2016
Authors
Ngugi, Pamela M.Y.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
AJOL
Abstract
Fasihi ni kama ndovu, nasi kama wafasili tunaweza kugusa sehemu mbalimbali za mwili
wake kujua alivyo ndovu huyu. Kila mara tunapofanya hivyo, tunagundua jambo jipya.
Unapomgusa ndovu huyu leo wakati mikono yako imejaa maji au ina unyevunyevu au
hata baada yo miaka mingi, unapata kumjua kwa njia tofauti. Fasihi ni kama ndovu huyu,
kila mara unapoisoma unagundua jambo jipya ... (Maoni yaliyotolewa no Prof Ngugi
katika mahojiano baina yoke no Dkt. Tom Odhiambo na Julias Sigei, Juni, 2, 2015). Kauli
hii aliyotoa Prof Ngugi inadhihirisha ukweli kuwa msomaji wa kazi yoyote yo fasihi ana
nafasi kuu katika harakati ya kuipa maana kazi ya kifasihi. Kilo mara msomaji
anaposoma kazi ya kifasihi huvyaza maana mpya. Maana hizi anazopata kutoka kazi
hiyo hutokana na mazingira ya msomaji, ufahamu wake na uzoefu wa kiusomaji pamoja
na muktadha wa msomaji. Makala haya yanalenga kubainisha mikakati ya uchambuzi wa
fasihi ya watoto kwa kuegemea mkabala wa Upokezi wa Msomaji hasa kwa kuegemea
msimamo wa Rosenblatt (1995) wa "Mapatano katika usomaji." Mtazamo huu
unachukulia kwamba msomaji wa kazi fulani ana mchango mkubwa katika harakati za
kuipa maana kazi ya kifasihi.
Description
Article
Keywords
Citation
Ngugi, P. M. (2016). Mikakati ya Uchambuzi wa Fasihi ya Watoto: Mtazamo wa Upokezi wa Msomaji. Kiswahili, 79(1), 43-52.