MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Subject "Children literature"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Uhalisi na mtindo wa Ken Walibora katika fasihi ya watoto(2011-12-22) Kairu, Winnifred Mukami; Momanyi, C.; Mukobwa, J.Utafiti huu umeshughulikia uhalisi na mtindo wa Ken Walibora katika vitabu vya Ndoto ya Amerika (2001), Mgomba Changaraweni (2003), na Mtu wa Mvua (2003). Utafiti huu uliongozwa na nadharia mseto ya mtindo, maadili na uhalisia. Nadharia hizi zilifaa katika utafiti huu, huku ikichukuliwa ya kwamba kazi za watoto zinahitaji kuangaliwa katika mikabala mbalimbali. Tasnifu hii ina jumla ya sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa ndipo mada ya utafiti, malengo ya utafiti, tahadhania, sababu za kuchagua mada na misingi ya nadharia zimefafanuliwa. Aidha, yaliyoandikwa kuhusu mada hii na fasihi ya watoto yamejadiliwa ili kushadidia pengo la utafiti huu. Upeo na mipaka ya utafiti imefafanuliwa. Hali kadhalika, mbinu za utafiti ukiwemo utafiti wa maktabani pamoja na uchanganuzi wa data muhimu zimefafanuliwa. Sura ya pili imejadili fasihi ya watoto na maendeleo yake nchini Kenya. Vilevile, uhakiki katika fasihi ya watoto na sifa zake bainifu zimefafanuliwa. Aidha, majukumu ya mhakiki wa fasihi ya watoto pia yamefafanuliwa. Sura ya tatu ya utafiti huu imejadili, dhamira, maudhui na mafunzo ya kimaadili katika hadithi fupi za mwandishi Walibora. Sura ya nne imejadili mtindo wa uandishi wa Walibora kwa mujibu wa fasihi ya watoto. Vigezo mbalimbali vya kimtindo vya fasihi ya watoto vimezingatiwa katika kuchanganua vitabu vya mwandishi. Sura ya tano na ya mwisho ni hitimisho. Matokeo ya utafiti yamefafanuliwa. Mchango, matatizo na mapendekezo ya utafiti wa baadaye yameangaziwa.