MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Subject "Catherine N. M. Mama wa kambo"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Tathmini ya ufaafu wa vitabu vy kusoma kwa madarasa ya 5 na 6 katika shule za msingi: mifano ya waandishi wanne(2012-07-06) Maria, Kaari Ruthiiri; King'ei, K.; Ryanga, C.Utafiti huu unalenga kutathmini vitabu vya hadithi vilivyopendekezwa na Taasisi ya Elimu Kenya kusomwa katika madarasa ya 5 na 6 iwapo vinatosheleza mahitaji yaliyokusudiwa. Vitabu vilivyofanyiwa uchambuzi ni Zawadi ya Rangi na R.W. Karani, Mwepesi wa Kusahau na Bitungi Matundura, Mama wa Kambo na C.N.M. Kisovi na Tumbili na Mkia Wake na W.E. Mkufya. Tasnifu hii ina jumla ya sura nne. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapo ndipo mada ya utafiti, maswali ya utafiti, malengo ya utafiti, sababu za kuchagua mada na misingi ya nadharia zimefafanuliwa.Yaliyoandikwa kuhusu mada hii na fasihi ya watoto yamejadiliwa. Upeo na mipaka ya utafiti imefafanuliwa. Mbinu za utafiti ukiwemo utafiti wa maktabani pamoja na uchanganuzi wa data muhimu zimefafanuliwa. Sura ya pili imafafanua vigezo mbalimbali vinavyoongoza uteuzi wa vi tabu vya kusoma kama fasihi ya watoto. Pia fasihi ya watoto ni gani imechunguzwa. Katika sura hii vigezo maalum vya uteuzi wa fasihi ya watoto vikiwemo maudhui,wahusika, ploti, mtindo, umbo, mandhari, lugha na vigezo vya kijumla vimeshughulikiwa .Sura ya tatu imeshughulikia ufaafu wa vitabu vya kusoma vya ziada katika madarasa ya 5 na 6 katika shule za msingi. Ufaafu wa vitabu umetathminiwa kwa kuzingatia vigezo vya wakuza mitalaa vya uteuzi wa vitabu vya ziada. Vile vile maoni ya wasomi wengine kuhusu fasihi ya watoto yamezingatiwa. Baadhi ya maudhui ambayo yamechunguzwa ni maudhui ya wivu, bidii, uzembe, mapenzi ya mzazi kwa mtoto na hila. Aina za ploti pia zimeshughulikiwa. Aina za wahusika zimechunguzwa. Vigezo vya kawaida kama vile umbo . la kitabu, urefuJ ukubwa wa kitabu, taipografia na ubora wa karatasi vimechunguzwa. Sura ya nne ni hitimisho la tasnifu hii. Hitimisho hili limetoa muhtasari wa kila sura. Maelezo ya matokeo ya utafiti yamefafanuliwa kulingana na malengo ya utafiti. Sura hii imeangazia matatizo, mchango,na mapendekezo ya tafiti zinazoweza kufanywa siku za usoni katika fasihi ya watoto.