MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Subject "Ahmad, Nassir., Malenga wa Mvita --History and criticism"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Ufumbuaji wa mashairi ya Kiswahili: mfano wa malenga wa Mvita na malenga wa Vumba(2012-03-29) Mung'athia, Robert; Geofrey K. King'ei; Masinde, E. W.Tasnifu hii imejadili suala Ia ufumbuaji wa mashairi ya Kiswahili ikizingatia diwani za Malenga wa Mvita na Malenga wa Vumba. Mashairi kumi kutoka diwani zote mbili yaliteuliwa kwa kuzingatia mada za unyumba, lugha na maliwazo,majonzi na maliwazo. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni nadharia changamano iliyotokana na nadharia mbili: nadharia ya uhistoria mpya na nadharia ya udenguzi. Mihimili ya nadharia hii changamano ilitumika kama dira ya kuongoza utafiti huu katika kuyafikia malengo yake. Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni pamoja na kubainisha kuwa mashairi kadha ni mafumbo, kubainisha vipengele vya lugha vilivyochangia kufumba maana au ujumbe wa mwandishi na kudhihirisha jinsi ya kupata fasiri tofauti za maana ya shairi iii kufanikisha uwasilishaji wa maudhui. Data iliyotumika katika utafiti huu ilikusanywamaktabani. Tulipitia diwani mbalimbali za mashairi pamoja na vitabu vingine vya fasihi na nadharia, tasnifu na majarida yaliyochangia kuupa msingi utafiti huu kinadharia na kimpangilio wa clata.Matokeo ya uchanganuzi wa data yalidhihirisha kwamba mashairi kadha ya Kiswahili ni mafumbo. Aidha, ucladisi wa kina wa macla, vipengele vya lugha vilivyotumika katika shairi, mtiririko wa ujumbe wa mwandishi kutoka ubeti wa kwanza hacli ubeti mwisho na kibwagizo hufanikisha ufumbuaji wa ujumbe. wa mwandishi. Mwisho, mapendekezo ya utafiti zaidi yalitolewa kuhusiana na matokeo ya utafiti huu.