MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Author "Asiko, Beverlyne Ambuyo"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Uamilishi dhima katika sentensi za luloogoli : mtazamo wa sintaksia finyizi(2011-12-02) Asiko, Beverlyne Ambuyo; Mwihaki, A. N.; Mbatha MathookoUtafiti huu unaamilisha dhima kupitia muundo na uhamisho wa katika sentensi za Luloogoli. Dhima inabainika kupitia uhusiano wa kisintaksia baina ya virai nomino na kiarifu katika sentensi moja. Dhima zilizoshughulikiwa ni Ale za kiima na shamirisho, pamoja na kanuni bia na kanuni bayana zinazotawala matumizi. Misingi ya kinadharia ya utafiti huu ni Sintaksia Finyizi kwa mujibu wa Chomsky (1995) aliporahisisha hatua changamano zaidi zilizokuwepo kwenye vijinadharia sita vya Utawala na Ufungami. Sintaksia Finyizi inatambua hatua tatu muhimu idadishi ya maneno kupitia majopo ya kisarufi muungano wa maumbo ili kuunda sentensi sanifu, na uhamisho wa vijenzi hivyo katika kugeuza muundo wa sentensi. Data ilikusanywa nyanjani na maktabani; kupitia kwa vitabu mahsusi vya Luloogoli na mazungumzo mahsusi. Mbinu ya kusampuli data kwa lengo maalum ilitumiwa ili kupata data iliyokuwa ikidhihirisha dhima mahsusi. Uhamisho wa dhima hizi umeelezwa na kudhihirishwa namna unavyotokea kwa kutumia michoro matawi, utafiti huu umeelezwa kwa sura tano. Ya kwanza inashughulikia maswala msingi na nadharia ya utafiti, ikifuatiwa na maelezo ya vijenzi vya sentensi za Luloogoli. Sura ya tatu inaangazia wazi zaidi na kubainisha dhima katika sentensi. Taratibu za uhamisho na kanuni zinazotawala uhamisho wa dhima hizi umeelezwa kwenye sura ya nne na mwisho kuna matokeo na mahitimisho ya utafiti. Suala muhimu linalojitokeza ni kuwa uhamisho hautokei to kiholela bali hutawaliwa na kanuni mahsusi. Kwa jumla, utafiti huu umependekeza kuwa sintaksia ya uhamisho ifanywe katika lugha nyinginezo ili kuendeleza uwanja huu kwa nadharia za kisasa zaidi.