MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Author "Aloo, Salome Njeri"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Uchanganuzi wa matangazo ya biashara katika redio na televisheni: mtazamo wa kipragmatiki(2012-01-31) Aloo, Salome NjeriUtafiti huu ni uchanganuzi wa usemi wa matangazo ya biashara kutoka vituo vya televisheni na vile vya redio. Umeshugulikia matangazo katika lugha ya Kiswahili. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza mbinu mbali mbali za ushawaishi zilizotumiwa na watangazaji ili kuziadhiri hadhira zao na kuendeleza mauzo ya bidhaa waliokuwa wanatangaza. Utafiti huu pia ulidhamiria kuchunguza mbinu mbali mbali za lugha zilizotumiwa na watangazaji hawa na ambazo zinaibainisha sajili hii. Utangulizi, swala la utafiti, malengo ya utafiti, sababu za kuchagua mada, yaliyoandikwa kuhusiana na mada, upeo na mipaka pamoja na mbinu za utafiti zinajumuisha sura ya kwanza. Misingi ya nadharia pamoja na maelezo kuhusu nadharia iliyotumiwa katika utafiti huu imejadiliwa katika sura ya pili. Katika Sura ya Tatu, mbinu mbali mbali za ushawishi kama vile matumizi ya picha na muziki, madai kuhusu bidhaa zinazotangazwa, upuuzaji wa bidhaa zingine pamoja na mikakati ya ulengaji hadhira imeshughulikiwa. Mbinu za lugha zinazopatikana katika matangazo yale zimejadiliwa katika sura ya nne pale ambapo Sura ya Tano imehitimisha utafiti huo na kutoa mapendekezo kwa utafiti wa baadaye.