Uwezo wa Lugha katika Matini ya Siasa Nchini Kenya Kuanzia Mwaka 2002 hadi 2005.
Loading...
Date
2014-03-13
Authors
Adero, Margan, Carlpeters
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu unaangazia uwezo wa iugha katika matini ya siasa nchini Kenya.
Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kudhihirisha vile lugha hutumiwa na
wanasiasa ili waweze kuonyesha itikadi zao na pia kupata mamlaka. IIi
kuonyesha uwezo wa lugha katika matini za siasa nadharia ya uchanganuzi
usemi hakiki ndio imetumiwa.
Katika utafiti huu sura ya kwanza ambayo ni utangulizi wa tasnifu inashughulikia
swala la utafiti, sababu za kuchagua mada, nadharia, madhumuni, upeo wa
utafiti, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Sura ya pili inaangazia na
kueleza dhana muhimu zilizotumiwa katika utafiti. Pia inaelezea mwingiliano
uliopo kati ya lugha, siasa, mamlaka na itikadi.
Sura ya tatu inahusu uchanganuzi wa data ya hotuba za kisiasa na
kuzichanganua kimuktadha na kimaana. Inatoa maelezo ya hotuba zilizotolewa
katika kipindi cha siasa kinachozungumziwa. Sura ya nne ni uchanganuzi wa
data na kueleza uwezo huo wa lugha katika hotuba za kisiasa nchini Kenya. Sura
ya tano ni matokeo ya utafiti, mapendekezo ya utafiti mwingine na matatizo
yaliyoukumba utafiti.
Description
Department of Kiswahili and African Languages, 83p. The PL 8702 .A3 2005
Keywords
Kenya --Politics and government --2002-2005 --Terminology, Kiswahili language --Political aspects --Kenya, Political science --Kenya --Language, Politicians --Kenya --Slang