Fani na maudhui katika mashairi ya magazeti ya taifa leo
dc.contributor.advisor | King'ei, Kitula Osore, Miriam | |
dc.contributor.author | Mogeni, Erick Magoma | |
dc.date.accessioned | 2016-03-10T08:11:49Z | |
dc.date.available | 2016-03-10T08:11:49Z | |
dc.date.issued | 2015 | |
dc.description | Tasnifu iliyowasilishwa katika idara ya kiswahili na lugha za kiafrika katika chuo kikuu cha Kenyatta kwa minajili ya kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili | en_US |
dc.description.abstract | Utafiti huu umeshughulikia fani na maudhui katika mashairi ya magazeti ya Taifa Leo Jumamosi na Taifa Jumapili katika kipindi cha mwaka 2010-2012. Katika fasihi ya Kiswahili kila mwandishi ana njia yake ya kipekee ya kuwasilisha kazi yake. Kuna wale wanaoeleza yaliyotendeka katika jamii kwa uaminifu na kwa namna ambayo atakayesoma kazi yake ataona ni mambo ya kuaminika au yaliyo na uwezo wa kutendeka katika jamii. Pia, kuna wasanii wengine ambao huelezea matukio halisi lakini kwa njia ya kiubunifu. Ingawa hivyo wasanii hawa wote hulenga kupitisha ujumbe kwa hadhira yao. Magazeti ya Taifa Leo huendeleza maudhui mengi kupitia mashairi yake; kwa mfano siasa, uchumi, utamaduni, mazingira, elimu, dini na mengine mengi. Hivyo utafiti huu umechunguza fani na maudhui yaliyoshughulikiwa na Magazeti ya Taifa Leo mwaka 2010-2012. Ulilenga kubainisha maudhui ya Magazeti ya Taifa Leo usawiri wao na hatimaye kuonyesha nafasi ya Magazeti ya Taifa Leo katika maendeleo ya mashairi nchini Kenya. Nadharia iliyotumiwa ni ile ya kimtindo ya kirasimi iliyoasisiwa na Leech na Short (1981). Nadharia hii imeteuliwa kwa msingi kuwa mihimili yake ilituwezesha kuchunguza maudhui tuliyoteua katika mashairi ya Magazeti ya Taifa Leo ili kuafiki malengo yetu. Data iliyotumiwa katika utafiti huu ilikusanywa maktabani ambapo mapitio ya vitabu, majarida, magazeti na tasnifu yalisaidia katika kuupa msingi utafiti huu. Magazeti teule ya Taifa Leo Jumamosi na Taifa Jumapili yaliteuliwa kwa msingi kuwa yalikuwa na mashairi yenye maudhui ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Uchanganuzi na uwasilishaji wa data ulifanywa kupitia maelezo. | en_US |
dc.identifier.uri | http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/14408 | |
dc.language.iso | en | en_US |
dc.publisher | Kenyatta University | en_US |
dc.title | Fani na maudhui katika mashairi ya magazeti ya taifa leo | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |
Files
Original bundle
1 - 1 of 1
Loading...
- Name:
- Fani na maudhui katika mashairi ya magazeti ya taifa leo .pdf
- Size:
- 610.83 KB
- Format:
- Adobe Portable Document Format
- Description:
- Full Text Thesis
License bundle
1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
- Name:
- license.txt
- Size:
- 1.71 KB
- Format:
- Item-specific license agreed upon to submission
- Description: