Fani na maudhui katika mashairi ya magazeti ya taifa leo

Loading...
Thumbnail Image
Date
2015
Authors
Mogeni, Erick Magoma
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia fani na maudhui katika mashairi ya magazeti ya Taifa Leo Jumamosi na Taifa Jumapili katika kipindi cha mwaka 2010-2012. Katika fasihi ya Kiswahili kila mwandishi ana njia yake ya kipekee ya kuwasilisha kazi yake. Kuna wale wanaoeleza yaliyotendeka katika jamii kwa uaminifu na kwa namna ambayo atakayesoma kazi yake ataona ni mambo ya kuaminika au yaliyo na uwezo wa kutendeka katika jamii. Pia, kuna wasanii wengine ambao huelezea matukio halisi lakini kwa njia ya kiubunifu. Ingawa hivyo wasanii hawa wote hulenga kupitisha ujumbe kwa hadhira yao. Magazeti ya Taifa Leo huendeleza maudhui mengi kupitia mashairi yake; kwa mfano siasa, uchumi, utamaduni, mazingira, elimu, dini na mengine mengi. Hivyo utafiti huu umechunguza fani na maudhui yaliyoshughulikiwa na Magazeti ya Taifa Leo mwaka 2010-2012. Ulilenga kubainisha maudhui ya Magazeti ya Taifa Leo usawiri wao na hatimaye kuonyesha nafasi ya Magazeti ya Taifa Leo katika maendeleo ya mashairi nchini Kenya. Nadharia iliyotumiwa ni ile ya kimtindo ya kirasimi iliyoasisiwa na Leech na Short (1981). Nadharia hii imeteuliwa kwa msingi kuwa mihimili yake ilituwezesha kuchunguza maudhui tuliyoteua katika mashairi ya Magazeti ya Taifa Leo ili kuafiki malengo yetu. Data iliyotumiwa katika utafiti huu ilikusanywa maktabani ambapo mapitio ya vitabu, majarida, magazeti na tasnifu yalisaidia katika kuupa msingi utafiti huu. Magazeti teule ya Taifa Leo Jumamosi na Taifa Jumapili yaliteuliwa kwa msingi kuwa yalikuwa na mashairi yenye maudhui ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Uchanganuzi na uwasilishaji wa data ulifanywa kupitia maelezo.
Description
Tasnifu iliyowasilishwa katika idara ya kiswahili na lugha za kiafrika katika chuo kikuu cha Kenyatta kwa minajili ya kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili
Keywords
Citation