Upekee wa Lugha Katika Mikahawa ya Eastlands

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorAhutah, Tony Munyasa
dc.date.accessioned2018-02-16T06:51:12Z
dc.date.available2018-02-16T06:51:12Z
dc.date.issued2012
dc.descriptionTasnifu hii imetolewa ill kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Kenyattaen_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kutambua na kubainisha sifa zinazoifanya lugha ya mikahawani- Eastlands kuwa na upekee fulani. Hizi ni sifa ambazo zimekita hadi kiwango cha kuifanya lugha hii ielekee kuwa namna ya sajili ya mikahawa hii inayopatikana mashariki mwa jiji la Nairobi. Tumechanganua data kutoka kwa mikahawa sita inayopatikana katika mitaa ya Jericho, Maringo, Bahati; eneo la mashariki mwa Nairobi. Utafiti huu ulikuwa na malengo matatu. Malengo haya yalikuwa: kubainisha sifa zinazobainisha lugha ya mikahawa ya Eastlands, kutambua maana zinazowasilishwa na lugha inayotumiwa mikahawani na jinsi lugha asili za wakazi zinavyoathiri lugha inayotumiwa mikahawani humo. Katika utafiti wetu tumeongozwa na nadharia ya sarufi amilifu mfumo iliyoasisiwa na Halliday miaka ya 1960. Nadharia hii huchunguza lugha kimuktadha. Kwa mujibu wa nadharia hii ya sarufi amilifu mfumo, lugha ina dhima ya kuelezea tajiriba zetu na kuzipatanisha tajiriba hizo ili kuunda matini inayoleta maana inayokusudiwa. Tumeitumia nadharia hiyo kuchanganua maana katika muktadha wa mazingira ya mikahawani, muundo na mwingiliano wa matini. Ripoti ya utafiti huu imepangwa katika sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi, ya pili imeshughulikia sajili kwa jumla, na ya tatu imeangazia lugha mikahawani Eastlands. Sura ya nne imeshughulikia maana mbalimbali zinazojitokeza katika matini na ya mwisho ni mahitimisho, matokeo ya utafiti na mapendekezo. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwa lugha ya mikahawa Eastlands ina sifa bainifu kama vile: utohozi wa maneno, kuchanganya msimbo, kubuni nomina kutoka kwa vitenzi na kuunganisha nomino kuvitaja vyakula. Aidha, utafiti huu umeonyesha kuwa lugha ya mkahawani ina maana tatu tofauti. Maana hizi ni maana dhanishi, maana tagusani na maana matinishi. Katika muundo wa matini kauli za kuamuru, maswali, ufupisho maagizo na vishazi vinatumiwa. VIen_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/18211
dc.titleUpekee wa Lugha Katika Mikahawa ya Eastlandsen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Upekee wa lugha katika mikahawa ya Eastlands.pdf
Size:
43.18 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
fulltext thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: