Upekee wa Lugha Katika Mikahawa ya Eastlands
Loading...
Date
2012
Authors
Ahutah, Tony Munyasa
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu ulilenga kutambua na kubainisha sifa zinazoifanya lugha ya mikahawani-
Eastlands kuwa na upekee fulani. Hizi ni sifa ambazo zimekita hadi kiwango cha kuifanya
lugha hii ielekee kuwa namna ya sajili ya mikahawa hii inayopatikana mashariki mwa jiji la
Nairobi. Tumechanganua data kutoka kwa mikahawa sita inayopatikana katika mitaa ya
Jericho, Maringo, Bahati; eneo la mashariki mwa Nairobi. Utafiti huu ulikuwa na malengo
matatu. Malengo haya yalikuwa: kubainisha sifa zinazobainisha lugha ya mikahawa ya
Eastlands, kutambua maana zinazowasilishwa na lugha inayotumiwa mikahawani na jinsi
lugha asili za wakazi zinavyoathiri lugha inayotumiwa mikahawani humo. Katika utafiti wetu
tumeongozwa na nadharia ya sarufi amilifu mfumo iliyoasisiwa na Halliday miaka ya 1960.
Nadharia hii huchunguza lugha kimuktadha. Kwa mujibu wa nadharia hii ya sarufi amilifu
mfumo, lugha ina dhima ya kuelezea tajiriba zetu na kuzipatanisha tajiriba hizo ili kuunda
matini inayoleta maana inayokusudiwa. Tumeitumia nadharia hiyo kuchanganua maana
katika muktadha wa mazingira ya mikahawani, muundo na mwingiliano wa matini. Ripoti ya
utafiti huu imepangwa katika sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi, ya pili imeshughulikia
sajili kwa jumla, na ya tatu imeangazia lugha mikahawani Eastlands. Sura ya nne
imeshughulikia maana mbalimbali zinazojitokeza katika matini na ya mwisho ni
mahitimisho, matokeo ya utafiti na mapendekezo. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwa
lugha ya mikahawa Eastlands ina sifa bainifu kama vile: utohozi wa maneno, kuchanganya
msimbo, kubuni nomina kutoka kwa vitenzi na kuunganisha nomino kuvitaja vyakula. Aidha,
utafiti huu umeonyesha kuwa lugha ya mkahawani ina maana tatu tofauti. Maana hizi ni
maana dhanishi, maana tagusani na maana matinishi. Katika muundo wa matini kauli za
kuamuru, maswali, ufupisho maagizo na vishazi vinatumiwa.
VI
Description
Tasnifu hii imetolewa ill kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Kenyatta