Utohozi fonolojia wa maneno - mkopo ya dholuo kutoka kwa Kiswahili

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorOmondi, Olal Anne
dc.date.accessioned2016-09-07T14:34:21Z
dc.date.available2016-09-07T14:34:21Z
dc.date.issued2008-11
dc.descriptionTasnifu hii imetolewa kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika idara ya kiswahili na lugha za kiafrika kwenye Chuo Kikuu Cha Kenyattaen_US
dc.description.abstractKazi hii inatekeleza madhumuni ya kuchambua maneno-mkopo ya Dholuo yanayotokana na lugha ya Kiswahili. Kuwepo kwa maneno mageni yanayoshabihiana na Kiswahili kulizua haja ya kueleza vipi Dholuo inavyoyaruhusu maneno hayo kutumika sawia na leksia zake asilia. Tatizo hili ndilo linaloshughulikiwa katika uchanganuzi wetu kama namna ya kuangaza jinsi Dholuo inavyoelekeza fonolojia yake kudhihirisha ukubalifu na usarufi wa utohozi ndanimwe. IIi kufanikisha uchambuzi wa mantiki ya mada yetu, tumeteua nadharia inayoafiki malengo ya utafiti wetu. Nadharia tulizotambua kutufaa ni Fonolojia Tenganishi na Fonolojia Mizanishi. Hali kadhalika tumewajibika kutumia mbinu husishi zitakazowajumuisha watafitiwa na mtafiti na kufanikisha utambuzi wa maneno-mkopo kutoka kwa Kiswahili yanayotumika katika uzungumzaji Dholuo. Mbinu hizo ni uchunguzi-ushiriki na mahojiano. Kijumla, mpangilio wa kazi hii umewasilishwa kwenye sura nne. Sura ya kwanza inatanguliza usuli wa mada pamoja na nyenzo za kimsingi zinazodhibiti kaida za uchanganuzi. Sura ya pili inaingilia vigezo vya Fonolojia ya Dholuo kwa maksudi ya kuangaza kanuni zinazoongoza lugha hii, ili kumulika jinsi zinavyoweza kuathiri maneno kutoka kwa lugha nyingine. Kitovu cha mada yetu kinashughulikiwa katika sura ya tatu ambapo uchambuzi unazingatia utohozi kifonolojia. Hapa ndipo panapo maelezo ya maumbo mbalimbali yanayotokana na utohozi pamoja na usawiri wa vielelezo vya sura dhahiri za maneno-mkopo. Sura ya nne ni tamati inayotoa muhtasari wa kazi yote.en_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/14924
dc.language.isootheren_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleUtohozi fonolojia wa maneno - mkopo ya dholuo kutoka kwa Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Utohozi fonolojia wa maneno mkopo.pdf
Size:
39.62 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: