Uchanganuzi wa Miundo ya Aristotle Katika Tamthilia ya Kinjeketile
Loading...
Date
2021
Authors
Wafula, Richard
Ngugi, Pamela
Okwena, Sophie
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu Cha Dar es salaam
Abstract
Makala haya yanalenga kuweka wazi miundo ya Aristotle katika
tamthilia ya Kinjeketile (1969). Kinjeketile ni tamthilia ya Kiswahili
ambayo iliandikwa mwishoni mwa miaka ya 1960 wakati ambapo
maigizo mengi yalichukua miundo ya Kimagharibi moja kwa moja. Huu
ni wakati ambapo Waingereza walileta drama kwa madhumuni ya
kujifurahisha wao wenyewe na kujikumbusha maisha ya kwao. Katika
kufanya hivi, waliwatumia Watanzania hasa, watoto wa shule katika
kuonesha tamthilia za akina Aristotle. Watanzania waliathiriwa kiasi cha
kuweza kujishirikisha kikamilifu katika kutunga tamthilia na kuzionesha.
Ebrahim Hussein aliandika Kinjeketile akitumia miundo ya kina Aristole,
hasa tanzia ya Kigiriki ambayo hasa ndiyo msingi wa sheria za kiAristotle. Kutokana na masomo yake, Hussein aliweza kuiga miundo ya
Aristotle katika utunzi wake.
Description
Article
Keywords
Citation
Wafula, R., Ngugi, P., & Okwena, S. (2021). Uchanganuzi wa Miundo ya Aristotle katika Tamthilia ya Kinjeketile. Mulika Journal, 39.